Rais Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mbunge wa Wawi, Hamad Rashid baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Mwanza leo.
Rais Jakaya Kikwete akiteta na mbunge wa Wawi, Hamad Rashid baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo akitokea Mwanza.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Mbona huyu Hamad Rashid anaonekana kama hana matatizo yeyote na ratiba zake zinaendelea kama kawaida?
ReplyDeleteIna maana CUF hawana ubavu wa kumdhibiti?
mmmh hapa itakua muheshimiwa hamad anamuliza mkuu wa kaya kama anaweza kuhamia ccm !
ReplyDeleteHamad, labda tu nianze kwa heshima yake. Mheshimiwa Hamad Rashid hongera kwa kuonyesha mfano juu ya ile siasa ya kileo na kitaalamu, bila matusi wala kejeli unafanya shughuli zako na kuwacha vyombo vya sheria kupitisha maamuzi yake. Hongera mheshimiwa Tanzania inahitaji watu wa mfano wako.
ReplyDeleteHuyu hamad anaonekana ni kweli ndumilakuwili
ReplyDeleteanataka kuuza chama kwa ccm
bora aende CCM kama CUF hawamtaki. Halafu huyu Lipumba, wenzake wanagombana yeye kimya, au mwenyekiti wa CUF ni Maalim Seif?
ReplyDeleteAmuulize kama anaweza kuhamia CCM wakati yeye siku nyingi ni wa CCM.
ReplyDeleteMh. Hamad ametoka kweli utafikiri yeye ndie PM.
ReplyDeleteLipumba yuko UK kwa mapumziko ya mwaka mmoja, baada ya uchaguzi mdogo wa Igunga, anatafakari jinsi ya kukiimarisha chama. Mahakama ni janja sana, tena yaelekea si muhimili imara, yaongozwa na serikali ya sisiemu. Haitatoa maamuzi ya hamad rashid wala ya kafulila mpaka juni 2015. Wakitoa ya hamad pekee bila ya kafulila nccr watalalamika. Wakitoa ya kafulila, utaitishwa uchaguzi mdogo, halafu jimbo la kafulila litaenda chadema. Halafu serikali haina pesa. kwa hiyo mahakama ina wabunge wawili hadi juni 2015.Hii ndio demokrasia.
ReplyDeleteLipumba katisha kula maraha UK. Rudi kusimamia mambo ya Chama. Au chama kimekushinda? UK na Chadema nani zaidi?
ReplyDelete