Hicho kimti kinachoonekana hapo ndio kitasa cha mlango huo na mambo yanakwenda kama kawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Bongo tambarare, kazi kweli kweli!!!
    Na Polisi wa usalama barabarani wanaona tu, ila wanabinya macho tu!
    Ikitokea ajali, eti ni bahati mbaya. Huo mlango unaweza ukasababisha ajali tena mbaya tu!

    ReplyDelete
  2. Ndio umasikini. Hata huko ughaibuni walianza kwa magari ya farasi!!

    ReplyDelete
  3. Hilo lazima litakuwa ni gari la taka,ndo zao hao,gari kama Taka zenyewe,na maisha wanayafanya kama Taka!
    Ahlam UK

    ReplyDelete
  4. Hizi Isuzu za miaka ya 1960 hazina 'spea' tena nadhani au spea zake ni adimu.Hizo kwa Dar zinaokota TAKA.Kuna na Land Rover 109 na Bedford...Ndizo zilikuwa gari za serikali miaka ile na zilikua zinaandikwa vizuri milangoni na zilikuwa zinafanya kazi kweli za serikali.

    OFISI YA MKUU WA WILAYA-KILIMO
    OFISI YA MKUU WA WILAYA-AFYA
    OFISI YA MKUU WA WILAYA-MIFUGO
    OFISI YA MKUU WA WILAYA-AFYA
    OFISI YA MKUU WA WILAYA-ELIMU

    ReplyDelete
  5. Ubunifu kaka,wee piga domo tu au ulitaka kitasa cha digital? Tuache na mambo yetu kwani maisha yanasonga mbele bila shaka.

    ReplyDelete
  6. Gari za kuwasha mbele hizi teh-teh-teh ikikosa break hii huwa wanaizamisha pembeni kwa watembea miguu mtakoma.

    ReplyDelete
  7. Unajuwa Nyerere alikuwa zamani akilalamika nasikia kuhusu Magari ya Punda Mjini ni mengi yaanze kupotezwa ila ile tabia imerudi kwa njia nyengine ya Mkokoteni haina tofauti kabisa.

    ReplyDelete
  8. Hizi ndio zile zile za kuwasha kwa kuzungusha chuma mbele kupiga hendel!

    ReplyDelete
  9. Imenikumbusha kitabu cha kiswahili sijui darasa la ngapi vile miaka ya nyuma kidogo. Kulikua na hadithi moja ya askari aliyesimamisha gari, mlango wa dereva haufunguki,kuangalia akaona msumari umeegeshwa kiaina,alipouvuta duu! Mlango mzima ukadondoka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...