Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la enzi za Mwakimu wakijiandaa kuondoka mjini Dar es Salaam kuelekea Mjini Dodoma kwa kutumia usafiri wa Basi la Kampuni ya Mabasi ya Pwani Tour Mwaka,wakiongozwa na Naibu Spika,Chifu Kasusura (aliyesimama mlangoni) wakati akiagana na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo ya Mabasi,Ndg. Babu Isaac.hii ilikuwa ni Mwaka 1984.
Home
Unlabelled
kutoka maktaba yetu leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mmmmmmmHHHHH!!! ni kama vile walikua hawajaomba mikopo kununulia magari ya kifahari toka Japan.... MMMHH? hapana ni kama vile walikua wanajaribu kuweka maslahi ya wananchi wanao wa wakilisha mbele??? au walikua wanamuogopa teacher.....??
ReplyDeleteTumetoka mbali eh! Halfu tunalalamika maendeleo yamedidimia kweli? Special coach hilo loh!
ReplyDeleteinakuwaje enzi hizi zirudi tena jamani ili pesa zooote za kununulia mashangingi zitumike katika sekta zingine za maendeleo kwa taifa letu "changa"!!! sijui wabunge watakubali.....
ReplyDeletesasahivi utawaweza wapi wabunge wanatumia mishangingi ya mamilioni ya hela wakati wananchi wanatembea kwa miguu na kandambili zilizofungwa kwa pini
ReplyDeletenchi yetu inaongoza kwa uongozi mbovu na wenye kujipendelea binafsi sana wala hawajali shida za mlalahoi
ipo siku tutapata kiongozi mwenye uchungu na nchi na huruma za wananchi atakaerudisha mipango kama hiyo ya usafiri wa pamoja katika kuokoa uchumi wa nchi.
We miss you Nyerere..where are you..you..youuuuuuuuuu
ReplyDeleteDavid V
miaka 28 iliyopita leo katika historia.maendeleo makubwa hayo leo kila mbunge ana usafiri wake tena wa nguvu na sijui kama hali ya Mtanzania wa kawaida ikoje?Ingefurahisha sana siku moja waheshimiwa wangeamua kuchangia vita dhidi ya umasikini kwa kutumia usafiri wa pamoja....itawezekana?
ReplyDeleteDuhhh Wah. wa Bunge la sasa wapo Peponi!!!
ReplyDeleteWanatumia Toyota VX V8 New Model kila mmoja!
Wenzao kipindi kile kitambo walikuwa wanalikwea PIPA ''Leyland CD kata shingo'' KWENDA DODOMA!
Hahahah kipindi kile kitambo, ama kweli tumetoka mbali sana!
ReplyDelete-Hapo Dereva kukata kona mpaka anyonge!,
-Kusimama hadi Hand brake ya bakora!,
-Juu ya Malango wa abiria kuna kengele!,
-Spring za mapanga hakuna suspension!,
-Viti 'kata shingo' hakuna viegemeo!,
-Nyuma ya mlango wa abiria kuna kipande cha gogo basi likipanda mlima likoishindwa Konda anaruka chini na gogo anapachika tairi la nyuma basi lisirudi nyuma!
siku hizi ni V8 tuuu........ kiasi gani cha mafuta kimeokolewa hapo
ReplyDeleteNafikiri hii irudishwe tena.
ReplyDeleteBy Andendekisye Mbije-0718563311
Hapo namba za Usajili wa basi ni TZ 51743 Model Leyland CD viti vyake 'kata shingo'!
ReplyDeleteGia ya basi imepinda kama namba 7 pembeni ya Dereva.
Muziki spika zipo kiti cha nyuma juu.
Hapo ndio unasikia Muziki wa Wana Paselepa-JWTZ,JKT-Kimulimuli Jazz,Diamond Cutting-Iringa, Moja One,Les-Wanyika,Lokassa ya Mbongo-Kenya.
Enzi za Mwl mambo yalikuwa safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sana so siku hizi v8
ReplyDeleteKwa wanasiasa wanafiki na wabinafsi wa siku hizi hakuna atakayekubali kuwekwa kwenye basi la pamoja. Kwenye Corolla tu anaweza kataa kupanda.
ReplyDeleteKipindi kile mwaka 47 !!!
ReplyDelete-Juu ya mlango wa abiria ndani pameandikwa:
*Abiria chunga mzigo wako
*Usiteme mate ndani
-Mlango wa Dereva kwa nje pameandikwa:
*Abiria 65
*85 KPH
-Dirisha kubwa la nyuma kwa ndani pameandikwa:
*Mlango wa Dharura
Maandishi ni rangi nyekundu.
Duhh Wabunge siku hizo walikuwa Wajamaa na Binaadam kweli kweli,
ReplyDeleteHivi sasa kwa magari wanyotumia peke yake Waheshimiwa ni MIUNGU WATU!
KILA KITU KINA UZURI WAKE NA UBAYA WAKE:
NDIO MAANA NI KUWA:
UJAMAA NI UTU NA UBEPARI NI UNYAMA!!!
Michuzi,
ReplyDeleteTafadhali sana HII PICHA INABIDI IKUZWE NA IBANDIKWE NDANI YA BUNGE KAMA KUMBUKUMBU NA HESHIMA YA UTUMISHI ULIOTUKUKA WA WABUNGE WA AWAMU YA KWANZA!
Hahahah Mdau wa 8 hapo ju Anonymous Fri Feb 24, 07:57:00 AM 2012
ReplyDelete...Nyuma ya mlango wa abiria kuna kipande cha gogo basi likipanda mlima likishindwa Konda naruka chini anapachika gogo tairi la nyuma basi lisirudi nyuma...!
Ebo, ndio kusema ma Konda wa siku hizo ilikuwa hakuna kulala!
Ina maana kwa Sheria za Trafiki za miaka hiyo ya 1984 kuwa na kigogo nyuma ya mlango ktk Basi la abiria,,,ilikuwa ni Sheria au Dharura?
ReplyDeleteItabidi Spika na Wabunge ili kulienzi Bunge la Zamani siku ipangwe litafutwe basi la Leyland CD lenye viti vya 'kata shingo' Waheshimiwa wapande basi hilo kutoka Dodoma hadi Dar au Dar hadi Dodoma!.
ReplyDeleteLakini hii ingefaa zaidi siku baada ya Uchaguzi Wabunge kwenda kuapishwa Dodoma na Raisi ingefaa safari ianzie Dar hadi Dodoma kwa basi hilo la kata shingo, ili kuwatoa jeuri wasilete zao za kutaka Magari ya kifahari baada ya Kuapishwa.
Hili bus itabidi litafutwe hata kama limekufa lifanyiwe ukarabati na Linunuliwe na Bunge kwa Mabilioni ya fedha za Walipa kodi zinazoelekezwa kwao.
ReplyDeleteAu kama halipo, litafutwe la mfano wake na litumike kwa Makumbusho ya Wabunge.
Inabidi hawa Waheshimiwa wakumbuke kuwa wakati wao wakitu gharimu MABILIONI ya shilingi kwa magari ya anasa na kutuletea jeuri ktk Utawala wenzao waliowatangulia walikuwa wanatumia usafiri wa Bus kwenda Bungeni Dodoma!
Kwa gharama zote bus hili la abiria 65 tunamwomba Mhe. Raisi atoe amri Bunge ilinunue tena litafaa sana kubana matumizi ya Waheshimiwa ni vile Brief case zao za Documents wataweka kwenye carrier juu!
ReplyDeleteDereva wa Bus atakuwa Naibu Spika (kwa vile ni mwanaume) na Kondakta atakuwa Spika mwenyewe Bibie!
ReplyDeleteItabidi iwe hivi kwa kuwa Naibu Spika Chifu Kasusura aliambatana na Wabunge akiwa kwenye Bus.
Sasa je kama Naibu Spika alikuwa ana Hadhi na Heshima ya U-Chifu akapanda bus kwenda Bungeni Dodoma itakuwa Ma Spika na Manaibu Spika wetu wa sasa ambao sio Machifu?
Aisee hili bus litafaa sana:
ReplyDelete1.Dereva: Naibu Spika
2.Kondakta:Spika mwenyewe Bibie
3.Tandiboi:Atafutwe Mbunge yeyote ambaye ni Fisadi apewe kazi ka kupandisha mizigo juu ya carrier na kushusha kama adhabu.
Hii ndio ile ile Leyland Albion, gea za kutafuta na breki za kupampu,,,ikikataa kuwaka kwa stata inapigwa 'hendel kwa mbele',,,kona mpaka upige resi kwanza ndio ikubali,,,ikiwa inapanda mlima ukiwa unatembea kwa miguu unaenda nayo sambamba!
ReplyDelete1984 siku zile Maisha yalikuwa simple sana, inawezekana Bajeti ya mwaka mzima ingetosha kwa chini ya Bilioni 10 tu!
ReplyDeleteWaheshimiwa na Kisasa wanatufilisi sana.
Hii aina ya usafiri wa magari ya Wabunge wa Kisasa Toyota VX V8 Mwananchi unaweza kuogopa hata kusalimiana na Mbunge wako!
ReplyDeleteKwa Bunge letu la sasa, angekuwepo NAIBU SPIKA CHIFU KASUSURA wa mwaka 1984 angeagiza anunuliwe Helikopta kabisaaa!!!.
ReplyDeleteKwa nini?
Kwa vile yeye zaidi ya Naibu Spika ni Chifu!
Baada ya kifo cha Nyerere nchi imepata Watawala Vijogoo.
ReplyDeleteLicha ya bus, Wabunge walikuwa wanasafiri kwenda Bungeni Dodoma kwa Treni!
Du kumbe wabunge wote wa TZ kubanana Dar es salaam wameanza siku nyingi sana. Au kila mkoa kulikuwa na Bus la kuwapeleka Dodoma?
ReplyDeleteHa ha haaaa! Hii imenikumbusha mbali sana. Hili ni Leyland CD. Hapo hakuna power steering wala nini na kubadilisha gia lazima ukanyage klachi mara mbili. Kelele inayotoka kwenye injini ni balaa. Ukisafiri safari ndefu kama umekaa mbele pembeni ya injini utafika mwisho wa safari yako kichwa kinauma na husikii vizuri.
ReplyDelete