Mwanamama anaejihusisha na shughuli ya kuomba omba Barabarani akijiandaa kunyanyuka kwenda kuomba fedha katika magari yaliokuwa yamesimama kwenye mataa ya Barabara ya Bibi Titi Mohamed huku mwanae mgogo akiwa amemuweka kwenye kibaraza kilichopo barabarani hapo mchana wa leo.Mwanamama huyu na wengine wengi wamekuwa wakijihushisha na shughuli hii ya kuomba omba huku wakiwa na watoto wadogo kama aonekanavyo huyu.
Home
Unlabelled
Mama na Mwana na shughuli ya kuomba omba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Haya ni mawazo yangu tu, na bila shaka wajuzi watanipinga ua kama wapendavyo kusema, ni USHAMBA tu.Miye nimeamka na kuanza kutia fikira kwamba wengi wetu, yaani mimi na wengine pia hatujui umasikini ni nini.We have never been really poor, may be we have been relatively poor, compared to those we see in their michumas etc.Umasikini waja kwa rangi mbalimbali, kuna umasikini unamfanya mtu akose hata kujiona kama yeye ni BinAdam na aanza kufikiria what am I doing here (In this world) Kuna pain moyoni zinazokufanya ukufuru,eg waanza kuwaza,why has He abandoned me.The pain can be suffocating.There are those of us who see poor people and say(audhubillah) if HE WANTED HE WOULD HAVE FED THEM HIMSELF.Check surat Yasin.So next time you see someone like this mother,try and feel her pains.
ReplyDeleteI know I am going straight to the kikapu, I love it there..
Hao hawana tofauti na Serikali yetu. Serikali yetu kila leo inakesha kuomba misaada ambayo hatuoni inafanya lolote la maana kwa wananchi. Afadhali huyu mama vijipesa atakavyopata atamlisha mtoto wake.
ReplyDeleteMdau wa kwanza, kwa heshima na taadhima, suala la umasikini si rahisi sana kulielewa. Kwa mfano, unapomuona huyu mama hapa katika hali yake ya kimasikini unaweza amini ana background ya shida ya kipesa na ndio maana yupo hapo. Mwingine ataingia deeper kwa kufanya research ('straight to the kikapu' or not, I'm not sure what you meant by that)na kugundua kuwa kumbe tatizo ni la kisaikolojia, na msaada wa kweli unaotakiwa ni matibabu na uangalizi wa karibu. Ama pengine vyote, umasikini na tatizo la kisaikolojia.
ReplyDeleteSikushambulii, ila nazidi kugundua mengi katika fikra zetu, na huwa tunakosea sana mara nyingi. Ni lazima tulijue tatizo ndio tuweze kulitatua, ni makosa kulihisi tatizo (jumping into conclusions). Tunafikiri masikini kule kijijini anachohitaji ni mkopo mdogo mdogo, kumbe hana hobi na biashara na anachohitaji ni kuajiriwa (si kila mtu anaweza kujiajiri hata akiwezeshwa). Leo hii tunampa mkopo kesho biashara imekufa, na anabaki na madeni na kuishia kunyang'anywa hata kile kidogo alichokuwa nacho awali.
Au tunadhani kila mfanyabiashara anahitaji nyongeza ya mtaji na mafunzo zaidi ya kibiashara, kumbe anachohitaji ni ulinzi na usalama wa biashara yake (yote hayasaidii kama kesho tu atavamiwa na wala mali yake isipatikane tena). Ama pengine anahitaji vyote kwa wakati mmoja. Ni lazima tujue kwanza ishu ni nini ndio tuikabili.
Pengine ungeshauri apatiwe chakula na malazi (huduma ya kwanza, which is not necessarily a solution to her PROBLEM/S), na utafiti ufanyike kuhusu shida aliyonayo ili asaidiwe kwa dhati. But I support your advise kulingana na hali halisi ya kinachoweza kufanywa nchini kwetu. Kwa nchi za wenzetu wangeingia deep zaidi, na ndivyo wanavyoweza kufikiria pia.