Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Viti Maalumu, Hilda Ngoye (CCM) ameitaka Serikali kuandaa muswada wa sheria itayakayodhibiti wanaofungua mitandao ya intaneti kiholela na kuitumia kwa ajili ya kutukana na kudhalilisha baadhi ya watu wakiwemo viongozi nchini.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni ambapo alisisitiza kuwa kwa sasa baadhi ya mitandao, maudhui yake yamejaa matusi na udhalilishaji kwa viongozi, jambo ambalo ni kinyume na utamaduni wa kitanzania.
“Pamoja na mitandao hiyo inayodhalilisha pia siku hizi katika vibanda vinavyotoa huduma za intaneti watoto wamekuwa wakiruhusiwa kuingia na kufungua mitandao yenye maudhui yaliyo chini ya umri wao,” alisema Ngoye.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga alisema tayari Serikali iko katika hatua ya juu ya mchakato wa kuwasilisha Sheria ya Habari bungeni ambayo itagusa pia eneo la matumizi ya mitandao.
“Sheria hii itazingatia mambo mengi kwa kuwa suala la habari linapatikana popote na kuwasilishwa kwa jamii kwa njia mbalimbali kama vile hiyo mitandao, magazeti, televisheni, vijarida na redio. Tutaangalia zaidi kama habari zenyewe zinaleta tija kwa nchi yetu,” alisema.
Kuhusu suala la vibanda vya huduma ya intaneti kuruhusu watoto, Naibu Waziri huyo alisema jambo la msingi ni kwa wazazi kuwadhibiti watoto wao kukaa mbali na masuala yanayokwenda kinyume na maadili.
Kuna mambo ya msingi mheshimiwa mnatakiwa kuyajadili bungeni achana na mambo ya mitandao.
ReplyDeleteNi sawasawa na kutunga sheria ya kuzuia watu wasi comment matusi katika facebook.
ReplyDeletehakuna mtu anayewatukana mnajishtukia tu mkianikwa ufisadi wenu mitandaoni, mama dunia ya sasa ni full utandawazi hata ikifungwa tuaamia huko facebook na tutatoa madukuduku yetu kama kawa, muwe mnatumikia wananchi kama mnavyoaidi wakati wa kuomba kura aka kula, inauma sana nyie wabunge mnaishi kama mko peponi wakati wananchi wana hali ngumu, halafu mnataka tukae kimya ili iweje? mmesahau hizi ni zama za ukweli na uwazi? tunaomba mchangie hoja za msingi jinsi ya kuondokana na umaskini uliokubuhu na sio mambo ya mitandao hapa, haya sio mambo tuliyowatuma huko bungeni. michu chonde chonde hakuna kubana utajeruhi hisia zangu!
ReplyDeletewe mama achana na mambo ya maadili kutotukana viongozi, fanyeni kazi na muwe na maadili ya kiuongozi uone kama kuna mtu atakutukana! full stop, acha woga seems hufanyi kazi kwa maadili ya kiuongozi, na uwe unatoa constructive points bungeni!
ReplyDeleteSASA WEWE MAMA INA MAANA HAMTAKI KUAMBIWA UKWELI? MKIAMBIWA UKQWELI MARA MMEISHA ANZA KFUNGIA MITANDAO , SASA HIO NDIO DEMOKRASIA YA CCM? HIVI SASA DFUNIA NI HURU MAMBO YA UDIKTETA YAMEKWISHA KILA MTU ANA UHURU WA KUSEMA LOLOTE SASA KAMA HATUSEMI LINI MTATUSIKILIZA? aCHENI UBABE WETU WA TISHA TOTO NINYI MMEKUWA KINA NANI MSIOMBIWA KITU. AU BADO MNAMSUPPORT NDUGU YENU GADDAFI? ANGALIENI KINACHOENDELEA KATIKA NCHI ZA WENZETU YOTE HIO NI KWA SABABU WANANCHI HAWAKUPEWA NAFASI ZA KUSIKILIZWA NDIO MAANA NA MATUSI YAMEKUWA MENGI.
ReplyDeleteMDAU HOLLAND
SOMEBODY SHOULD EDUCATE THIS WOMAN ON HOW THE INTERNET WORKS....WENGINE WANAROPOKA TU HUKO BUNGENI...HIVI WEWE MAMA HUKO INTERNET ILIKOANZIA WAMESHINDWA KUDHIBITI HILO NYIE MTAWEZA?WACHENI WATU WAJIMWAGE,MKISHINDWA KAZI TUTAWATUKANA TU,TENA SIO MITANDAONI TENA BALI LIVE........MICHUZI SIJATUKANA NI MAONI TU.
ReplyDeletembunge usiachwe na wakati,kama kuna maoni toka kwa mwananchi akieleza hali halisi si kutukana,zamani ilikuwa hakuna njia ya wazi au moja kwa moja ya kujieleza lakini sasa ipo.
ReplyDeletewewe mama acha kuingilia uhuru wa mtu aseme anachokitaka,unataka kuleta udikteta wako,na watu wasiwe na haki ya kusema ukweli?utawala wa kumzuia mtu asiseme ukweli umeshapitwa na wakati!sasa tupo mwaka wa 2012 ni ukweli na uwazi tu hakuna kurudi nyuma!
ReplyDeleteBinafsi sijaona mtandao wowote unaotoa lugha za matusi na mbunge huyu anatakiwa arejee KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uhuru wa maoni Sheria ya 2005 Na.1 ib.5 Inasema
ReplyDelete18. kila mtu:-
(a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake;
(b)anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila kujali mipaka ya nchi
(c)anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake; na
(d)anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu ya jamii.
Mkumbushe mbuge huyu kupitia kifungu hichi cha sheria. Mitandao ya sasa inaeleza ukweli halisi wa maisha ya mtanzania, na hii inaonyesha ukomavu wa demokrasia unakua nchini. Inabidi akubaliane na teknolojia ya sasa. Sijaona blog au facebook imemtukana mtu yeyote, anatakiwa afute kauli yake ni amedanganya na alete ushahidi kuonyesha nani katukanwa au ametoa lugha ya matusi! Labda huwa anawaruhusu watoto wake kuangalia porn online hiyo ipo nje ya uwezo wa taifa anachotakiwa aweke filter kwenye computer yake na kublock porn sites sio kushambulia mitandao isiyo husika. Alaaaaaa!
JAMANI KAMA MIMI SIKUELEWA NAOMBA MNIFAHAMISHE MSINIPIGE VIGONGO VYA MANENO, NILICHOELEWA MIMI NI KWAMBA HUYU MAMA AMESEMA KUZUIA MATUSI KWENYE MITANDAO NA SIO KUKANYANA AU KUAMBIANA KWELI KWA LUGHA YA KIUSTAARABU, MIMI NAUNGA MKONO KUWA MATUSI HAYAFAI HATA KWENYE FACEBOOK, ILA KUAMBIANA NI LAZIMA NA MUHIMU KABISA, SASA KAMA MTU UNAMJUA NA AMEKUUDHI KWA NINI USIMKABILI ANA KWA ANA, NA KAMA KUTUKANA NI SAWA MBONA HAO WATUKANAJI WANAFICHA MAJINA YAO? MIMI MSEMAJI SANA HASA KWENYE JAMII FORUM, LAKINI MATUSI SIKUBALIANI NAYO, MWENYE DUKUDUKU LA MATUSI AMKABILI ANAYEMKUSUDIA USO KWA USO, AU ANAPOANDIKA MATUSI YAKE BASI NA JINA LAKE KAMILI ATAJE.
ReplyDeleteJAMANI EH MSISHAMBULIE HUYU MAMA BURE - MMEMUELEWA????? MNAJUA TOFAUTI KATI YA MATUSI NA KWELI????? KWELI SEMENI RUKSA, TENA MNAPOSEMA KWELI TAJENI MAJINA YENU YA KWELI NA JINA LA HUYO UNAEMPA UKWELI JAPO UNAUMA, NA MNAPOTUKANA HALIKADHALIKA TAJENI MAJINA YENU YA KWELI, SIO MARA JOKA LA MDIMU MARA SAMAKI MCHANGA, KAMA MATUSI NI SAWA KWA NINI MNAFICHA MAJINA YENU?
ReplyDeleteWewe anony wa Mon Feb 06, 07:37:00 PM 2012
ReplyDeleteuna point ila umekurupuka...mitandao kibao imejaa matusi...jifunze kujenga hoja...acha ushabiki! Uhuru wa kutoa mawazo hauna ubishi kwenye zama za utandawazi, swala unawasilishaje mawazo yako, wakati gani, mahali gani, yakimlemga nani, na kwa lengo gani (namaanisha yakiwa na madhara gani)...by the way hata mama pamoja na kupitwa na wakati nae alikuwa anatumia uhuru wake kutoa maoni!...tembelea na uchuje mawazo yako kabla hujawasilisha kwa hadhira!
Eddy
Vancouver
Huyu mama kama yeye kiongozi anatakiwa kuchukua matusi kama changa moto, ajirekibishe. kwa nini watu wanatukana?!! Kwa vile wamechoka na siasa zisizo na maendeleo kwao. Watu wanatakiwa kuwa na uhuru wa kuongea wanayotaka, utafilter vipi mtandao? Jamani twende na wakati. Ukianza kukataza watu wasiongee basi ndiyo mwisho wa uhuru. Mama tumwambie vizuri atabana mpaka ataachia tu. Kwenye uhuru tunasema ingawa wengi wameshinda, lakini wachache vile vile wana haki ya kusikilizwa, kwani maamuzi yanawagusa wote.
ReplyDeleteNakubaliana na wadau wanaosema kuwa huyu mama hajui Internet inavyofanya kazi. Hapa ameonyesha 'ignorance' ya hali ya juu na kwa bahati mbaya sana waziri amemjibu kisiasa. Kuzuia watu wasitukane mtandaoni is easier said than done.
ReplyDeleteMimi ninakubaliana na wadau wanaounga mkono alichosema mama. Lazima tuelewe kuwa hoja, ukweli, mawazo, michango na mapendekezo ni TOFAUTI na matusi au kudhalilisha. Wewe anony wa Mon Feb 06, 02:05:00 PM 2012 inaonekana una jazba na pengine ni mmoja wa wale wanaotumia lugha zisizofaa kufikisha ujumbe. Huwezi kusema kuna wengine 'wanaropoka' huko bungeni - mimi binafsi nafikiri comments kama hizi ndizo ambazo huyu mama amelenga. Hata huko ilikoanzia Internet watu hawadhalilishi wenzao, wanatoa michango inayojenga na mara nyingi iliyofanyiwa upembuzi yakinifu - kama ni data zinakuwa well researched. Sasa sisi huku nyumbani tunaiga mambo halafu tuna-overdo! ndiyo sababu hata facebook unakuta mtu anaweka private matters ambayo kimsingi ni tofauti na isiyostahili kuweko katika social networks. Tujaribuni kujifunza jamani na kuona hii mitandao inatumikaje kule ilikoanzia. Tuache kuiga mambo ki-limbukeni. Kabla ya kudhalilisha mtu au kutukana, kumbuka unayemtendea hivyo ni aidha, Baba, Mama, Mme, Mke, Mzazi, Kaka, Dada, Mjomba, Shangazi nk wa mwenzako - na sijui ukijitoa alikokanyaga yeye ukajiweka hapo unajisikiaje? Zaidi: kumbuka pia kuwa unapofikiri umejificha ktk ANONYMOUS au Ngedere Mweusi n.k ni sawa na kuvua nguo kisha unajifunika kwa mikono - kwa taarifa yako hakuna siri katika compyuter yoyote duniani - wakikutaka utapatikana tu! Heshima ni kitu cha bure na umfanyiapo mwenzako ubaya iko siku yatadunda Mungu atakuadhibu maradufu.
ReplyDeleteAnonymous wa Wed Feb 08, 02:25:00 AM 2012-Unachoongea ni ukweli na naomba ungerudia tena kusema ili watu wa kwetu, Bongo, waelewe,"kumbuka pia kuwa unapofikiri umejificha ktk ANONYMOUS au Ngedere Mweusi n.k ni sawa na kuvua nguo kisha unajifunika kwa mikono - kwa taarifa yako hakuna siri katika compyuter yoyote duniani - wakikutaka utapatikana tu!" Ila natofautina na wewe kwa kusema siye kama watu wapenda haki tumechoka na hawa viongozi kutuambia mbofu mbofu. Sidhani kama watu wanajali kama wanajulikana au hawajulikani. Ndio maana nasema kiongozi mzuri angechukua hayo matusi kama changa moto, kwa mfano mashabiki wanaweza kuzomea timu yao kwa mchezo mbovu, lakini wakibadilika utaona mashabiki wanaishangilia. Timu inakuwa imechukua mawaidha vizuri toka kwa mashabiki kujirekebisha na siyo timu kutishia mashabiki wake.
ReplyDelete