Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi kwa wabunge leo mjini Dodoma baada ya kuzuia hoja ya mgomo wa madaktari bingwa kujadiliwa Bungeni iliyoibuliwa na mbunge wa Mbozi Magharibi Godfrey Zambi  na kufafanua kuwa suala hilo tayari limeshaanza kufanyiwa kazi na Bunge ikiwemo kuiagiza kamati ya huduma za jamii kulifuatilia suala hilo kwa kukutana na pande zinazohusika  na kupeleka majibu bungeni.
Naibu waziri , Ofisi ya Waziri mkuu Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Aggrey Mwanri  akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge  kwenye ofisi ya waziri mkuu yakiwemo masuala ya migogoro ya mipaka ya viwanja kwenye Halmashauri  na manispaa ya Kigoma –Ujiji pamoja na suala la kuongeza madaktari bingwa na manesi katika manispaa ya Dodoma kufuatia ongezeko la watu na vyuo mbalimbali leo mjini Dodoma.
Mawaziri na wabunge wakifuatilia kwa makini mkutano wa sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni  Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi  Zanzbar  Balozi Seif Ali Idd ,mbunge wa Songea Jenista  Mhagama na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samueli Sitta (kulia), wengine waliokaa nyuma ni Waziri ,Ofisi ya Waziri mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dkt. Mary Nagu, Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi na Naibu waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga.
 Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa) wakitekeleza majukumu yao  ndani ya ukumbi wa Bunge kwa kuhakikisha kuwa watanzania wanayapata matangazo ya Bunge kupitia TBC Taifa moja kwa moja kutoka mjini Dodoma.
Raia wa kigeni ambao wako nchini  wakiwa ndani ya Bunge wakifuatilia kipindi cha Maswali na majibu cha mkutano wa sita wa Bunge kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamaa wageni hawa wenzetu wako makini na hata hawatumii mtafsiri (translator) kupitia headphones! Kiswahili oye!

    ReplyDelete
  2. Wekeni siasa kwenye mgomo wa madaktari mtaona mwisho wake.Hilo ni bomu linafuka moshi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...