Sakamaleko Ankali
Ebwana naomba vichwa vyangu vya khabiri viache kama vilivyo, maaana nna hasira ya kufa mtu wallahi. Unajua leo siku ya tatu kwangu umeme hakuna. Na sio kwamba kuna mgao, la hasha. Nimeshindwa kupata LUKU kwa sababu eti hakuna netweki kama tangazo hapo juu lenye mwandiko wa ngumbaru linavyoonesha. Mie na akina yakhe wenzangu wenye kutumia LUKU ya mwaka 47 (ile ya kadi na sio digito), unaambiwa hata kwa MPesa tunashindwa kununua. Kisa hakuna netweki. Yaani soooo! Uliza uliza yangu kwa hawa jamaa zako wa TANESKO wanasema ati wao sio wenye tatizo ila TTCL wanayotumia mtandao wao (tena wa kisasa wa faiba!) umebuma hivyo wao hawana ujanja!! Yaani jikampuni kubwa kama TANESKO hawanaga fall-back, na TTCL ikibuma ina maana hakuna huduma. HII inaingia akilini kweli. Haya na hao TTCL waliobwagiwa mpira nao wako kimya. Na kama kawa wanangoja mambo yajipe yenyewe. Huyu mchawi aliyturoga wabongo kafa nini. Maana angekuwa hai tungeenda kumuangukia. 


Naomba Ankal hili dukuduku langu usibanie maana nawewe umezoeaga kubania mambo kama haya. Usibanie ninaposema kwamba wote TANESKO na TTCL ni wazembe na lazima wawajibishwe. Mie imeniuma sana jana nimekosa kuangalia gemu kibao, naambulia kusoma nusunusu magazetini kuwa Man Yu kaua na Man City ndio hivyo tena.Kisa? ati TANESKO hawana netweki na TTCL imebuma. Jamani, siku tatuuu?? Kungekuwa na mgao (ambao sasa wamerudisha umeme kisailensa) ningeelewa. Sasa netweki bila kuwa na hatua mbadala ina maana gani kama si uzembe! Allllaaaaaah!


Mdau
Darisalama




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. TTCL lazima ibinafsishwe sasa hakuna wanachokifanya!

    ReplyDelete
  2. pole sanasana kwanza hiyo luku ingetakiwa iondoke kwa sababu ilikuwa kwa ajili ya ndugu zetu wa soweto na wachimba madini wakati wa ubaguzi wa rangi sababu ya migomo ,waje na mbinu mpya ya kukusanya mapato ambayo ni rahisi sana kuliko mambo ya kununua umeme kama nyanya na hata huduma hawajui,ni rahisiwangenunua satellite dish yao kupata mtandao mojakwamoja bila kumtegemea mtu dollar 10,000 tu

    ReplyDelete
  3. Mdau pole sana Wewe na wote tunaopatwa na tatizo kama lako Kaka naona una Hasira mpaka Ujumbe unajieleza Ancle Michuzi Naona siku hizi No Editing SAMAKAMALEKO mdau alikuwa na hasira ilibidi uiweke ASALAAM ALAYKUM MDAU CAIRO.

    ReplyDelete
  4. Yani hasila yote unaaka umeme kwa ajiri ya GAME ! kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  5. Hayo majamaa ya TANESCO ma*******zao sasa kampuni kubwa kama hiyo mnashindwa kuwa na net zenu eti TTCL,hiyo TTCL yenyewe kimeo.
    Kuweni makini bwana,sasa hiyo net ikikata hata wiki kwa hiyo inakuwaje sasa.Nyinyi vipi tafuteni njia mbadala bana siyo kila siku mara maji hakuna sijui Mteja sasa maji yapo tena unasikia ooh Network hakuna sasa lipi ni lipi???.

    ReplyDelete
  6. These stations are connected to the vodacomtz network, yo can get LUKU from either of them

    Ilala
    1
    ONLINE TABATA SEGEREA VENDING STATION
    2
    ONLINE KARIAKOO MSIMBAZI (GAPCO) VENDING STATION
    3
    ONLINE KARIAKOO UHURU GAPCO VENDING STATION
     
    Kinondoni North
    1
    ONLINE TANGI BOVU VENDING STATION
    2
    ONLINE KAWE OILCOM VENDING STATION
    3
    ONLINE VICTORIA OILCOM VENDING STATION
    4
    ONLINE BOKO OILCOM VENDING STATION
     
    Kinondoni South
    1
    ONLINE MANZESE VENDING STATION
    2
    ONLINE MANZESE DARAJANI VENDING STATION
    3
    ONLINE MANZESE OILCOM VENDING STATION
    4
    ONLINE MAGOMENI KAGERA MAK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...