Ubalozi wa Tanzania Brussels (Ubelgiji) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania, Chuo Kikuu cha Gent na sponser(VLIR) wanasikitika kutangaza kifo cha Mwanafunzi Ndugu William Lufundisha, kilichotokea tarehe 15/02/2012 katika Chuo Kikuu cha Gent , Ubelgiji.
Jumuiya ya Watanzania na marafiki wa marehemu Lufundisha wanafahamishwa kwamba tarehe 23/02/2012 saa 8 kamili alasiri itafanyika ibada ya kumuaga marehemu kwenye kanisa lililopo katika hospitali ya Plafijn Ziekenhuis ( Plafijn hospital), HENRI DUNANTLAAN 5, 9000 GENT .
Ubalozi pamoja na Jumuiya ya Watanzania watafarijika na ujio wa watakaoweza kuhudhuria ibada hii ya kumuaga mpendwa wetu Marehemu William Lufundisha.
Imetolewa na Ubalozi na Jumuiya ya
Watanzania Brussels, Ubelgiji.
Mpendwa, rafiki yetu sana Willy hakika umetuacha ukiwa kijana kabisa na bado tukikuhitaji katika ujenzi wa taifa letu katika fani ya uvuvi hasa ufugaji wa viumbe maji (Aquaculture).
ReplyDeleteMwenyezi Mungu akupe raha ya milele na upumzike kwa amani, AMINA.
Daah, imenigusa sana hii taarifa. RIP man. Uvuvi umepoteza mpiganaji...
ReplyDeleteS. Mgeleka
Kijitonyama, DSM.
RIP William
ReplyDeleteGone too soon , at a very tender age.. RIP William ...RIP
ReplyDeletePoleni sana wazazi, ndugu, marafiki na wafanyakazi wote wa wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. R.I.P William
ReplyDeletekazi ya mungu haina makosa.
ReplyDelete