Habari Ankal Michuzi,

Natumai uko vyema wewe pamoja na Timu yako nzima inayowajibika kuliendeleza libeneke la Globu ya Jamii vyema kabisa,tunawapongeza sana kwa hilo.leo nimekuja na hili,yaani Ninaandika hili nikiwa nnahasira sana na pia kujulisha umma na kuiomba serikali kufanya linalowezekana kabla hali haijawa mbaya kwa wananchi kuchukua hatua mikononi baada ya kuchoshwa na usumbufu, karaha na unyama wanaofanyiwa na kijana anayeitwa shizi ambaye yupo maeneo ya makutano ya barabara ya nyerere,pugu na kawawa.

Huu ni ushuhuda na pia nimeshuhudia mwenyewe kwa kijana huyo kupanda juu ya bonet ya gari yangu, kisha juu ya roof na kisha kunivunjia side mirror ya gari yangu. Nimeripoti Kituo cha karume na pia Usalama wa barabarani Taifa na hakuna lililotendeka. Hadi sasa hivi mchana kijana huyu anatamba maeneo ya darajani karibu na ofisi za makao makuu ya wizara ya maliasili na utalii. 

Kijana huyu anabeba chuma maalum cha kuvunja kioo cha mbele ya gari lako akilazimisha kusafisha kioo cha gari yako bila ya ridhaa yako na kama hautampatia fedha anazohitaji yeye basi huna kioo. Kijana huyu siyo kichaa, kwani anaongea na wenyeji wa hapo darajani maneno ya kebehi ukishuka kwenye gari lako kumfuata anakimbia.

 Amevalia kaptula bila ya shati wala viatu. Hununua maji ya kilimanjaro akichoshwa na jua na kuinywa taratibu. wakati magari yakianza kuondoka huondoka barabarani na kukaa kivulini.

 hupenda kwenda hotelini hapo bondeni Karibu na Wizara ya maliasili na utalii na kula chakula cha kutosha. Hulipia chakula hicho na hana ubabe kwa watu wanaomfahamu. Sasa naomba maaskari wa Jeshi la Polisi wamshughulikie kijana huyo kabla wananchi uvumilivu haujawaisha. 

Pia ni vyema kutambua kuwa kijana huyu alikuwa maeneo ya mataa ya ubungo kabla ya wananchi kumpiga na kuhamia maeneo haya.

Mdau Wa Globu ya Jamii,
Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Naungana na mdau juu ya hili kwa kweli hali imekuwa mbaya na kila mmoja analalamikia juu ya matendo ya huyo chizi, kwa kweli jitihada za haraka zinahitajika kuchukuliwa. Kwani hata mimi ameniharibia bonet ya gari yangu kwa kupanda juu yake. Tunaomba mamlaka husika ikiwemo polisi zitusaidie kumuondosha huyu jamaa, ukizingatia anapofanya hayo unakuwa katikati ya foleni na huwezi kumuepuka wala kukimbia.

    ReplyDelete
  2. Aise hii ni hatari.Huyu atakuwa zimefyatuka kidogo,mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya hivyo.Kuna vichaa vya aina nyingi.Madaktari wa neurone watatusaidia.Lakini ni jukumu la wahusika kumwondoa maeneo hayo.

    David V

    ReplyDelete
  3. Nafasi yake huyo ni kukaa Jela na kula bure huko, kwa vile Uraiani watu hula kwa kutumia bidii, kujiheshimu na akili.

    ReplyDelete
  4. Nafasi yake huyo ni kukaa Jela na kula bure huko, kwa vile Uraiani watu hula kwa kutumia bidii, kujiheshimu na akili.

    ReplyDelete
  5. Tuwekeeni picha yake ashughulikiwe.

    ReplyDelete
  6. Akamatwe na apate kichapo halafu bila huruma unamsafirisha kijiji kilicho mbali na mji wa Dar yaani ikiwezekana mipakani huko akaishi na akirudi mjini basi adabu itakuwepo.

    ReplyDelete
  7. Huyu ni wa kuchoma moto tu full stop.

    ReplyDelete
  8. akamatwe kisha wampeleke hospitali ya vichaa huenda ana matatizo ya akili..... Kabla watu hawajatumia chuma chake maalumu kumtia majeraha au kifo

    ReplyDelete
  9. Police jamanni sasa huwa inafanya nini?hawa watu wanaosafisha magari ya watu hairuhusiwi kwakweli kisheria barabarani kwakweli tanzania inachekesha police hata hawajui sheria wao wenyewe!huyo mtoto watu waungane wakate mkono wake kwanza wakulia itakuwa mfano kwa wengine na mimi ilitokea pale magomeni wanalazimisha kuosha kioo vipi hii nchi jamani?

    ReplyDelete
  10. Kwa haraka haraka naona ni mtoto mwenyewe ugonjwa wa akili. Unaweza ukawa conduct disorder au antisocial personality disorder.
    Tunaona ni ukorofi lakini huo ni ugonjwa unaohitaji matibabu. Unatibika

    ReplyDelete
  11. wizara zetu zimekuwa hazifatilii majukumu yao, sijajua watu wanategeana kuchukua maamuzi, wanangoja amri, wanadhalau au vipi? Wizara yaulinzi imekuwa hovyo sana, askari wetu wamekuwa nadhalau wakiskia mtu kama huyo kijana wanajua hana pesa, Michuzi we wapime tu, piga simu waambie kuna mzigo wakontena wamagendo apa, wamuhindi, mwarabu au m2 flani wa hadhi ivi dakika 0 tu washafika cz wanajua watapata mlungula, niujinga tu hakuna kingine. Hatujui tunauwa nchi yetu wenyewe. huko road kuna wageni wengi wanapita wanaona na wanaathiliwa nahao vijana bt sisi hatujali me inaniuma kuona wengi wetu hatujali taifa letu bali tunaja5i umeme na cent tunazopata ktk lushwa i hate these..

    ReplyDelete
  12. Kuna rafiki yangu aliwahi kukutwa na huyo mtu anaedaiwa kichaa pale ubungo mataa. Akamuharibia wipers zote alaf akapanda kwenye bonet,rafiki yangu akawa amepatwa wasiwasi hali ambayo angeweza kusababisha ajali na hakukuwa na msaada kutoka kwa mtu yoyote.
    Pia kuna watu wanadaiwa kuwa "mateja" wanaodai hela kwa nguvu kutoka kwa makondakta wa daladala,wanatembea na silaha kama bisibisi,wembe n.k na kwa anaebisha kutoa hela wanayoitaka wao basi wanamuumiza na ivo vitu na kuiba simu na kwa raia pia ambae atajaribu kuongea wakati huo. Kuna mmoja anajulikana kama "DAME" kule barabara ya mwananyamala kuelekea victoria. Kwakweli usalama wa raia uko hatarini kwa mambo kama haya. Sasa sijui tukaombe msaada wapi au tukimbilie wapi ambapo tutapata ulinzi wa miili yetu na mali zetu.
    Naomba polisi wajaribu kuchunguza hili na kumshika hao watu,kwa sisi tunategemea usafiri wa umma ama daladala tunakosa amani tukipita njia hiyo,maana ukiwa umekaakaribu yao anything might happen na kujikuta unaumia,kuibiwa n.k.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...