Familia ya Mwanamuziki Whitney Houston ambaye alifariki Dunia Jumamosi ya wiki iliyopita,imewasikitisha maelfu ya mashabiki wa mwanamuziki huyo kutokana na utaratibu wa maziko ya mwanamuziki huyo kuwa ambayo yanafanyika leo kwa kuhusisha familia na wale watakaopewa mwaliko maalum tu.
Sehemu waliyopanga yafanyike mazishi hayo ina uwezo wa kuchukuwa watu 1,500 wakati awali kulikuwa na taarifa kuwa zoezi la kuuaga mwili lilikuwa lifanyike katika Ukumbi wa Prudential Center unaochukuwa watu 18,000.
Mume wa zamani wa marehemu, Bobby Brown ana uwezekano wa kukosa kuhudhuria maziko kwa kile kinachodaiwa kuwa familia haimuhitaji tena kwa sababu alishatengana na Whitney Houston.
Bado kuna wingu kubwa la maswali likiwa limetanda juu ya kifo chake kwani watu wa karibu na marehemu wameeleza kuwa siku chache kabla ya umauti kumfika alisema anataka kuonana na Yesu na alikuwa akisisitiza juu ya hilo pia shoo yake ya Mwisho kuifanya alivaa nguo nyeusi tupu.
Peter Tatchell ambaye ni mtetezi wa haki za watu wa jinsia moja wenye uhusiano wa kimapenzi aliandika katika mtandao wake kuwa, Whitney aliwahi kuwa mmoja wao lakini alifanya hivyo kwa siri miaka ya nyuma.
Ila huyu dada alikuwa 'mkali' enzi za ujana wake hey??
ReplyDeleteR.I.P Whitney...
R.I.P Whitney. We will always deeply missing you.
ReplyDeleteYou touched so many hearts across the world through your magical voice in your songs!
@2,"We will always deeply miss you"
ReplyDeleteanazikwa Sunday 19th February 2012
ReplyDelete