Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na jitihada zetu tumefanikiwa kumsafirisha marehemu HAROUN ABDALLAH OTHMAN (Maarufu kwa jina la JAMHURI) ili akazikwe nyumbani.Mwili wa Marehemu utawasili Dar Alhamisi 01/03 saa nane na nusu usiku kwa ndege ya Turkish airline (TK603)

Pamoja na hali ngumu inayoendelea kutukabili watanzania tunaoishi Ugiriki ugumu huo haukuweza kutuzuwia kutekeleza ada na mazowea ya kumsafirisha mtanzania yeyote anaefariki hapa.

Jumuiya ya watanzania ugiriki, inawashukuru wale wote walioshiriki kwa hali na mali katika kumsafirisha mwenzetu.

Tunapenda kutoa shukurani maalum kwa Kaimu Balozi wetu Rome Italy kwa kututumia haraka mno "barua ya uthibitisho" iliyoturahisishia kwa kiasi kikubwa harakati zote za kumsafirisha Marehemu.(N.B. Huduma zote za kibalozi kwa hapa yatubidi tuwasiliane na Italy)
Tunamuomba Allah amlaze Marehemu mahala pema peponi.(Amin)

INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN

Kayu Ligopora
Katibu Mkuu
Jumuiya ya watanzania ugiriki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. "Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajioon" Mwenzetu katangulia nasi sote hiyo ndiyo khatma yetu. Mwenyeez Mungu amughufirie kwa yote na amlaze pema PEPONI ameen!

    ReplyDelete
  2. INNA LILLAH WA INNA ILAYH RAJIUUUUN

    Na kila mmoja wetu ataonja Umauti, Ndio Amri ya ALLAH S.W.T,,,AMIIIN.

    ReplyDelete
  3. Innalilahi Wainna Ilayhi Rajiuun...Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kurejea kwake ni haki...Mwenyezi Mungu.Awape subra wafiwa wote Mzee Abdullah shtoto na ndugu wote...Bila kusahau kutoa shukrani zangu za dhati kwa ndugu zangu nyote mliokuweko Ugiriki kwa juhudi na jitihada zetu za kumstiri ndugu yetu huyu. Mwenyezi Mungu akusahilishieni katika maisha yenu nyote na akuzidishieni wepesi kwa kila hali...Udumu udugu wenu na imani zenu.

    ReplyDelete
  4. Inna Lillah Waina Ilayhi Rajoon

    ReplyDelete
  5. Mungu amlaze pema my man Karabi.
    Ni mmoja wa vijana waliofanya mtaa wa Kikwajuni kuwa kikwajuni enzi hizo.RIP bro.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...