Home
Unlabelled
ngoma imekolea.....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Haya ndo mambo tunayoyaweza. Hapo juu wawekezaji wanadai hawapati wataalamu wa kuendesha mitambo, hapa watu wamekalia kucheza ngoma. Haya twendeni tutafika.
ReplyDeletehii picha ya wapi jamani? hizi sura kama nazifahamu za mwitongo
ReplyDeletehawa wameshakunywa pombe za TBS-less
ReplyDeleteMambo ya bongo hayo jamani karne ya ishirini na moja! kwa hali hii je tutafika kweli? si wacheza ngoma pekee hata hao wanaowashangaa pia walitakiwa wawe wakiendelea na shughuli zao za kila siku.yawezekana ni burudani baada ya kazi!!
ReplyDeleteNiburudani wakati wa kazi ,maana ni mchana kweupeeee!labda iwe Jmosi au Jpili.
ReplyDeleteHalafu tunaomba misaada kwa wazungu na mataifa yenye wananchi wanaofanyakazi.
Mbaya zaidi kuna vijana wadogo tele nao wanamsherehekea huyo jamaa ambaye ni selebriti wao.
Poa tu ndio tamaduni zetu hizi!
Mi sioni tatizo, huenda ilikuwa sherehe ya kujipongeza baada ya kufanyakazi kwa mwaka mzima. Halafu kusema amelewa mnamuonea, huyu jamaa anakunywa pepsi. Kilichowazingua ni style yake ya kucheza naona kaweka manjonjo sana.
ReplyDeletehaya kweli ndio tunayoyajua na kubaki kulalamika eti wazungu wanatunyanyasa, wasitunyanyase kwa nini wakati wa kufanya kazi na kujifunza tunacheza ngoma, angalia umati uliojaa nyuma yao,hao wote wangekuwa wanafanya kazi na kujifunza si tungekuwa mbali,tuamke jamani tuache kulalamika dunia ya sasa si ile ya zamani
ReplyDeleteTufikie hatua ya kudharau ngoma zetu kihivyo. Kwani kuna ubaya gani wa kucheza au kuangalia ngoma kama hizi hasa kama ni baada ya kazi au wkend. Wazungu walisema ngoma zetu ni za kishenzi. Na sisi tumeanza kuona kwamba walikuwa sahihi?
ReplyDeleteMkurugenzi wa PPTL Tanga analalamika kuwa hakuna wataalamu wa kufanya kazi za kiwandani kwake wengine wanaburudika kwa ngoma tu . Lahaula!!!Kwa ngoma na mambo yasiyo na tija Bongo tupo juu. Ama kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
ReplyDeleteYote tisa, kumi angalia suruali ya jamaa hapo magotini!
ReplyDeleteJamani hawa jamaa walikuwa wanatangaza Pepsi dare for more.
ReplyDeleteJamaa wameona bora wafanye Tangazo la Pepsi bure manake makampuni yanawalipa matozi na masista duu tu!
ReplyDeleteJamani ni burudani tu baada ya kazi. Wazungu huwa wana stress tu kila wakati hawana sehemu ya kuondolea mawazo(socialize) wanajifungia ndani tu na kijutia maisha.
ReplyDeleteHiyo ndiyo Tanzania ya karne ya 21 (Karne ya Sayansi na Teknolojia). Haya bora tufike.
ReplyDeleteebu acheni kuponda naona wadau wote mmeuwa sana kila nchi ina tamaduni na mila zake hata ulaya wanacheza ngoma zao
ReplyDeleteDuhhh Bwana mkubwa hapo anacheza nyuma ya Shangazi kama hataki vile, anarusha mikono kwa kususa!
ReplyDeleteKIPAJI CHETU:
ReplyDeleteNa hiki Wakonongo Watanzania ndio kipaji chetu!
-Uwezo wa kuendesha Mitambo,
-Kusaini mikataba ya Faida na Wawekezaji,
-Kuendesha Makampuni kwa Faida,
-Uendeshaji wenye ufanisi kibiashara HAYO TUPO WEUPEEE HATUNA UWEZO KABISAAAA!
Kazi yetu ni Mchiriku, Kiduku na Pekecha pekecha kukesha usiku kucha mpaka asubuhi,
Hapo cha kunogesha ngoma ni:
ReplyDeleteMkono wa kushoto glasi ya maji meupe!,
Mkono wa kulia msokoto!
Ahhhh Dunia ipo ndani ya ubongo hakuna kulala!
Suruali ya ' Bush Celebrity' yaani Nyota wa Shamba IMECHAKAA NA KUCHANIKA MAGOTINI KUTOKANA NA MIELEKA ANAYOPIGA AKIANGUKA KWA GONGO ANALOLEWA!
ReplyDeleteDuhh hapo Kaka Mkubwa akiwa Kijijini Kaliua Tabora rumba amelicheza huku akiwa bwiiii...
ReplyDeleteHakuna balaa la kimaisha kama kupigika ukiwa nyumbani Kijijini,,,ndio haya hapa...au itokee mambo yamekataa ,yaharibike Mjini ukimbilie nyumbani Kijijini,,,ndio haya hapa!
ReplyDeleteMasikini weee inaonekana nguo 'pamba' alizopiga Msela ndio alizokuja nazo kitambo akitokea Mjini na sasa zinachakaa zikiwa mwilini,,,kilicho baki anajiliwaza kwa Gongo na kushukuru Promosheni ya PEPSI Kijijini iliyolileta gari kumwezesha kucheza Sebene!
Hapa sio pengine, inawezekana ni maeneo ya Lugoba, Chalinze au Chanika Kijijini Mwisho wa lami!
ReplyDelete