Polisi wakiwa katika gari lao wakati wa kutuliza vurugu zinazoendelea wakati huu mjini songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo kuandamana kupinga mauaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na watu wasiojulikana.
Polisi wakiwatawanya na kuwakamata baadhi ya waandamanaji hao katika manispaa ya Songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki kuandamana hadi ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma kupinga mauaji ya watu yanayoendelea kwa kasi mjini humo ambao hadi sasa jeshi la polisi halijafanikiwa kuwakamata wauaji.
MADEREVA PIKIPIKI WAKIWA WAMEFUNGA BARABARA YA SONGEA KWEWNDA TUNDURU KARIBU NA MLANGO WA KUINGILIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA Ruvuma,wakilitaka jeshi la polisi mkoa huo kuchukua hatua dhidi ya mauaji ya watu yanayoendelea mjini songea ambapo hadi sasa zaidi ya watu 8 wameuawa na watu wasiojulikana wengi wao wakiwa ni madereva wa pikpiki.
NA MUHIDIN AMRI,SONGEA
JESHI la polisi mkoani Ruvuma limelazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya wananchi waliokuwa wakiandamana kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma na kituo kikuu cha polisi Songea mjini hali iliyopelekea shughuli mbalimbali kusimama.
Hali hiyo ilianza kujitokeza majira ya asubuhi ambapo wananchi wa mtaa wa Lizaboni wengi wakiwa ni madereva wa pikpiki walianza kujikusanya na kuanza maandamano kuelekea kituo kikuu cha polisi kilichopo karibu na uwanja wa majimaji mjini hapa.
Wananchi hao walikuwa wakiimba nyimbo za kulaumu jeshi la polisi wakidai kuwa limeshindwa kudhibiti mauaji yanayoendelea kujitokeza mjini hapa kila mara ambapo hadi sasa zaidi ya watu kumi wameshauawa na watu wasiojulikana.
“Tumeamua kuandamana kwani kimsingi mauaji yamezidi kutokea mjini hapa jana ameuwawa mtu,juzi na usiku wa kuamkia leo ameuwawa mwendesha pikipiki na abiria wake”walisikika wakisema.
Baada ya wananchi hao kukaribia kituo cha polisi walianza kurusha mawe na ndipo polisi walijihami kwa kutumia mabomu ya machozi ambapo wananchi hao na waendesha pikipiki walianza kukimbia ovyo na kupeleka maduka kufungwa kwa hofu ya kuibiwa.
Licha ya biashara mbalimbali kusimama pia ofisi za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa na ya mkuu wa wilaya Songea zilifungwa kwa kuhofia waandamanaji kuingia kwenye ofisi hizo na kufanya uharibifu.
Kabla ya maandamano ya leo februari 20 mwaka huu wananchi kutoka kata ya Lizabon waliandamana hadi kwa mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Ole Sabaya kulalamikia kukithiri kwa mauaji katani humo ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wasiojulikana.
Akijibu malalamiko hayo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa serikali itahakikisha ulinzi unaimarishwa na kwamba aliwataka kuimarisha ulinzi shirikishi ili kukabiliana na matukio hayo maovu.
Februari 19 mwaka huu mkazi wa Lizaboni Bakary Ally(20) aliuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojulikana ambapo februari 20 mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku mtu mmoja mkazi wa mtaa wa Kipera shekhe Jamari(65) alikutwa ameuwawa kwa kukatwa mapanga kichwani na watu wasiojulikana wakati alipokuwa akielekea nyumbani kwake.
Marehemu Jamari alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wa msikiti uliopo katika eneo hilo la Kipera.
Mauaji hayo yameendelea kujitokeza ambapo mwendesha pikipiki ambaye jina lake halikufahamika mara moja ameuwawa na watu wasiojulikana katika mtaa wa Mji Mwema mjini hapa usiku wa februari 22 mwaka huu na kupelekea wananchi mjini hapa kuishi kwa hofu kubwa.
SIYO MIMI PEKE YANGU NIAYELISHANGA JESHI LA POLISI TOKA VIONGOZI WAKE WA JUU HADI POLICE CONSTABLE.
ReplyDeleteHili nalisema kwa sababu sijui kama wanaongozwa na code of ethics zinazowaongoza watumishi wote wa serikali ama wanaongozwa na emotional instability feelings zinazosababisha wafanye maamuzi yasiyo sahihi ya nguvu na kulitia doa jeshi hilo na taifa kwa ujumla.
Kama kuna chombo cha dola kinachopoteza mwelekeo kwa kasi ndani ya Tanzania,basi ni jeshi la polisi vingine vinafuatia eg,executive.
Viongozi wake wakuu hata hawakemei haya mauaji ya raia na wala kukemea matumizi ya nguvu na silaha za moto kuzuia maandamano ya wananchi.Walicho kariri hawa vijana ni virungu,mateke,makofi na bunduki basi mambo mengine ya kudhibiti raia kwa kutumia njia mbadala ya kuwaruhusu wafikishe maoni yao ngazi husika ni mwiko na ndicho kiapo huko depo.
SASA WAZIRI NAODHA USHAURI.
1.Pitisha mafunzo kwa askari wako ya kutotumia virungu,mateke,makofi na silaha za moto.
2.Wakanye mara moja na kupewa adhabu pale wanapofanya vitendo vya unyanyasaji kwa raia visivyoendana na code of ethics za jeshi la polisi.
3.Wawe na rational decisions na kutumia diplomatic approach ya kuzuia maandamano na kero za wananchi rather than using extraordinary brutal forces zinazotafsiriwa kama uonevu na unyanyasaji wa haki za binadamu eti kwa sababu tu wamebeba silaha za moto.
kitu hiki ni rahisi sana kufanya utatuzi wake, ningekuwa mimi ndo mkuu wa mkoa wa Ruvuma ningea anza na Tangazo la spika juu ya gari kuwatangazia wananchi watembee wawiliwawili na saa 12 jioni kila mtu ndani ya nyumba yake, halafu ningeita mkutano na wajumbe wa nyumba kumikumi, na kufanya sensa ya haraka kutafuta wageni hao wanaotoka msumbiji na kuwakamata na kuwahoji kuhusu jambo hili wakati huohuo polisi wangu wangefanya doria usikukucha wakishiriliana na wananchi. habari ingeisha, sasa naona ungozi wa mkoa umepumzika unasuburi kuletewa idadi ya walouawa, huo ndo upumbavu walio nao.
ReplyDeleteBusara ya hali ya juu itumike katika kurudisha hali ya amani.
ReplyDeletePolisi watawakamataje wanaoua watu wakati hao polisi wanasubiri ofisini wapelekewe ushahidi wa kutosha wa hao majambazi ndio wakawakamate?
ReplyDeletePolisi nawashangaa, wananchi wanaandamana kwa sababu watu wanauliwa kila siku lkn polisi hawajachukua hatua madhubuti, lkn cha kushangaza polisi nao wanawaua hao wanaopinga wenzao kuuawa. Sasa je hayo mauaji ya raia, polisi wanayaunga mkono? Napata shaka hapa.
ReplyDeletepolisi na raia shirikianeni kumaliza tatizo hili kwa busara bila kuongeza kumwagika kwa damu
ReplyDeleteDuh! kweli kimenuka!
ReplyDeleteHiyo picha ya kwanza juu km sikosei hapo ni mtaa wa mabatini (chini kidogo ya soko la manzese)
Km kichapo kimefika hadi mitaa ya mbali hivo kweli ni balaa.
Busara itumike vurugu hazimalizwi kwa vurugu!
Kuandamana Ok, lakini kurusha mawe polisi?! Nao si watarusha mawe ya kwao? Anyway, Poleni Songea.
ReplyDeleteUlinzi shirikishi ndio utakaosaidia kumaliza matatizo yote yanayopelekea uhalifu wa namna yeyote. Polisi peke yao hawawezi kwani idadi yao ni ndogo ukilinganisha na raia, tusikurupuke kuwalaumu polisi kushindwa kulitafutia ufumbuzi suala hili kwani ni kubwa kiasi chake na linaonekana kufanywa na genge la wahalifu wajuzi. Bado hatujawekwa wazi kama kuna mahusiano ya mauaji na unyang'anyi au ushirikina. Wananchi wa maeneo husika wanapaswa kutembea kwa vikundi na kuilinda mitaa yao wakishirikiana na polisi, pengine wanaweza kukamatwa watu ikawa ndio mwanzo wa kulifichua genge zima.
ReplyDeleteKimea
Z'bar
Ni wakati muafaka sasa Jeshi la Polisi likawa la Kijamii zaidi kwa kuzingatia thamani ya Utu wa watu, Haki za Kibinaadamu na Misingi ya Demokrasia.
ReplyDeleteKama Polisi imeweza kuasisi jinsi ya kuifikia Jamii, kuwa karibu nayo na kutafuta Ushirikiano nayo kupitia ''POLISI JAMII'' kama ilivyo.
JE HAPA KUNA ''POLISI JAMII'' AU ''POLISI UADUI?''
Kuna sababu gani Polisi hiyo hiyo IKATUMIA DHIDI YA WANANCHI NGUVU, JAZBA NA UMWAMBA?
RAIA HAWANA KOSA LOLOTE KWA KUANDAMANA. NASHANGAA POLISI KUTUMIA NGUVU NYINGI KIASI HIKI, WANANCHI WANA HAKI YA KUANDAMANA BAADA YA KUONA MAUAJI YANAENDELEA BILA KUPUNGUA NA HAKUNA ANAYEKAMATWA.NI WAZI POLISI WAMESHINDWA KAZI...WATU WANANE (8) WANAUAWA WAO WAPO WAPO WANATOA VISINGIZIO VYA WIVU WA KIMAPENZI...HATA KAMA NI WIVU WA KIMAPENZI INA MAANA WANAPASWA MWANANCHI MTANZANIA ANA HAKI YA KUUAWA? KWA NINI WASIPELELEZE? KIMSINGI POLISI WAMESHINDWA KAZI HAWANA TECHNIQUES NA HAWAJUI JINSI YA KUPELELEZA, WANACHOJUA NI KUCHUKUA RUSHWA NA KUKAMATA WAPINZANI...NAAMINI HATA DCI MANUMBA ANAMTISHIA SAMWEL SITTA BAADA YA SITTA KUMWELEZA UKWELI KUWA POLISI HAWAFANYI UCHUNGUZI WANATEGEMEA HABARI ZA KULETEWA NA KUTOA MAJIBU MEPESI MEPESI.MUBARAK ALIUA WATU HIVI AKAPELEKWA MAHAKAMANI AKIWA KWENYE MACHELA. TUNATAKA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZULU NA MKUU WA POLISI HAKUNA WANACHOFANYA ZAIDI YA KUONGEA. TUMECHOKA!!
ReplyDeletePolisi wanatumia nguvu kutatua matatizo yanayohitaji ufuatiliaji. Wao wameshindwa kuweka doria ila wanaweza kuwakamata waandamanaji kwa sababu ndiyo wanaoweza kuwaona mbele yao.
ReplyDeleteHata polisi wenyewe wauaji, utamipigaje binadamu hivyo wakati hana hata silaha? Stupid narudia stupid na ni waoga kama nini, wakuu wa polisi watafutiwe visa ya kuja kwa malkia waone tukiwa na makosa wanavyotueleza kwa upendo makosa yetu na kusema ndio tumekosea bila kigugumizi. Mbona hata J.K anaonaga huku
ReplyDeleteKwa Polisi nadhani nguvu iliyotumika ni kubwa sana kiasi cha kuua watu kwa risasi za moto kwa kisingizio cha maandamano haramu,
ReplyDeleteHii ni changamoto kubwa kwa serikali na vyombo vyake vya usalama kuhakikisha zinapatikana njia mbadala pindi hali km hii inapotokea
MUNGU IREHEMU TANZANIA NA UIKOMBOE.
ReplyDeletePolisi embu kuweni na moyo wa huruma na mtende haki.