UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Amina Saidi Mrisho kuwa Kamishna wa Sensa ya Mwaka 2012.
Aidha, Rais Kikwete amemteua Bibi Seraphia R. Mgembe kuwa Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Raslimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Taarifa iliyotolewa na kutiwa saini Dar es Salaam leo, Jumanne, Februari 21, 2012, na Kaimu Katibu Kiongozi, Bwana Peniel Lyimo imesema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Februari 20, mwaka huu, 2012.
Taarifa ya Bwana Lyimo imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bibi Amina Mrisho aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Katika taarifa tofauti iliyotolewa na kutiwa saini pia mjini Dar es Salaam leo,  Jumanne, Februari 21, 2012, na Katibu Mkuu Ikulu, Bwana Peter Ilomo, imesema kuwa uteuzi huo wa Bibi Mgembe umeanza pia jana, Jumatatu, Februari 20, 2012.
Bwana Ilomo amesema katika taarifa yake kuwa kabla ya uteuzi wake Bibi Mgembe alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa MKURABITA. 
Bibi Mgembe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Ladislaus Salema ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
 Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Februari, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wanawake wanaweza kwa vitendo. Vijana nao wanaweza wapewe nafasi.

    ReplyDelete
  2. labda sielewi mie,kabla ya uteuzi wakeBi Amina Mrisho alikuwa mkuu wa mkoa wa Pwani.!!! Hivi Mwantumu ni mkuu wa mkoa gani. nakwama hapo nisaidieni jameni.

    ReplyDelete
  3. Taarifa ya ikulu sio sahihi, Amina Mrisho hakuwa mkuu wa mkoa wa Pwani. hii ni hatari sana kwa ofisi kuu kutoa taarifa yenye makosa ya wazi kama haya. Tutawaamini kwa lipi?

    ReplyDelete
  4. We mtoa maoni wa saa 11:39:00am unaendeshwa na hisia zaidi kuliko hali halisi, kama hufahamu mambo ni bora kukaa kimya kuliko kuandika off points wasomaji wote wakakuona zoba. Sentensi inayoelezea kuhusu mama amina ni 'aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa pwani' upo kaka?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...