Semina ya UNHCR - Protection Induction iliyofanyika Mpanda tarehe 25/01/2012 kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya maji wilaya ya mpanda na kushirikisha Asasi za kiserikali, mashirika ya kitaifa na kimataifa na wadau mbali mbali.
Mwendeshaji mkuu wa semina Wakili Godlove Kifikiro ambaye ni Protection Associate wa UNHCR field office mpanda, akiendesha semina ambapo aligusia juu ya shughuli za UNHCR, maana ya mkimbizi, haki na wajibu wa mkimbizi na sheria ya mkimbizi ya Tanzania ya mwaka 1998
Mwendeshaji mkuu wa semina Wakili Godlove Kifikiro ambaye ni Protection Associate wa UNHCR field office mpanda, akiendesha semina ambapo aligusia juu ya shughuli za UNHCR, maana ya mkimbizi, haki na wajibu wa mkimbizi na sheria ya mkimbizi ya Tanzania ya mwaka 1998
Ndugu Michael Kiimbila, ambaye pia ni mshauri wa maswala ya kiusalama UNHCR Mpanda akitoa mada juu ya kusikiliza na kupeleleza matukio ya kihalifu kwenye kambi za wakimbizi
Baadhi ya washiriki wa semina wakipata msosi
Huyo jamaa picha ya pili kutoka chini mbona ana sahani mbili za msosi? Au kuna mtu kamchukulia?
ReplyDeletesasa wewe mdau wa hapo juu swali gani unauliza kama kajipendelea sahani mbili au kamchukulia mtu inasaidia nini?
ReplyDeletemwache mtu ajinafasi maisha mafupi sana angalia watoto wa kova wenyewe wanajiwahi maana ofisi zao hazina hata restaurant wenyewe wanakula kwa mama ntilie wakiwa kazini.
Hizi ndio Semina zinazo rubuni watu wetu kuendelea kukubali sera za Shirika la Wakimbizi bila kujali maslahi ya nchi yetu. Watu wetu hawana budi kuamka na kuacha kutapeliwa na watu waojali tu ajira zao. Wakimbizi warudi kwao. Nchi yetu ndio nchi pekee duniani inayotoa uraia wa halaiki kwa Wakimbizi. Wazungu hawadhubutu huko kwao lakini wanauza sera hiyo kwetu kwakutumia pesa yao na wenzetu wenye njaa.
ReplyDeletejamaa ame-bust! nakumbuka enzi za JKT...
ReplyDeletesio ubishi, ame-bust. ingekuwa sivyo then tungeona chupa mbili za soda hapo pembeni, but ni moja inaonyesha share zote ni zake....
mwenye sahani ya pili kaenda kunawa mikono.
ReplyDeleteHi hi hi hi hiiiii......Jamani jamani, kaa mnaona kweli kweli...yaani mimi nisingewaza kabisa kuwa; jamaa ana sahani 2.
ReplyDeleteIla inaonekana ni yakwake kabisa, maana ipo karibu sana nae. Maisha magumu Bongo, acha ale maisha mtu wa watu anapopata chanzi ndo hapo hapo.
Hapo Wabongo ndo mnapobolonga,
ReplyDeleteyaani huyo mchangiaji wa hapo juu yeye kaona wakimbizi tu.
mbona wazungu wanakuja wanachukuwa kila kitu hapo TZ na hamsemi kitu,,, waafrica wenzenu kuomba ukimbizi nchini kwenu ndo imekuwa nongwa.
mkiwa mnatoa maoni fikilieni kwanza hata kama TZ hakuna vita ila watZ wanauana wenyewe,, angalia mambo mangapi yanatokea na waTz mmekaa kimya, umeme, Madini na mambo mengi kila siku mtanzania anazidi kuwa masikini kwa sababu ya uongozi mbovu.
hicho ndo cha kuongelea na siyo ooh wakimpizi,,, nyambafu kabisa..
Annony wa Feb 04, 10:47:00 PM aonyesha kuwa ni mkimbizi! Anadai waTZ tunauana wenyewe kwa wenyewe!! Huyu kweli kasahau kilichomtoa kwao; kuuana wao kwa wao! Nakubaliana na Annony wa Feb 04, 04:39:00 PM wazungu wanaturubuni tu. Hakuna shida ya kukaa na wakimbizi tena nchi zao zone sasa kuna akheri; warudi!
ReplyDeleteKula siyo mpaka uandikiwe na Daktari ukizingatia madaktari wenyewe wamekataa kazi. Ninyi mmeona sahani mbili na soda moja je lita 1.5 ya maji ya k'njaro hamjaiona? nahisi nyuma yake kuna CHARLES GLASS, TEHE TEHE TEHE!
ReplyDelete