Mchekeshaji Maarufu Nchini,Evans Bukuku akikafanya vitu vyake usiku huu katika kiota cha maraha cha Nyumbani Lounge,Namanga jiji Dar wakati wa Shoo yake ya kuvunja mbavu za watu (kucheka) iliyomalizika muda mfupi uliopita.
Dogo Pepe nae kama kawaida yake,akipanda jukaani lazima mkome wenyewe kwa vituko vyake.
Enika akiimba nyimbo zake za kuchekesha.
MC Taji Liundi akiwa Libenekeni usiku huu.
Mtangazaji wa Radio Clouds FM,Adam Mchomvu a.k.a Baba John nae alipata wasaha wa kupanda jukwaani na kutoa hadithi yake ya kuchekesha.
Kila Mtu alieingia kwenye shoo hiyo ya Evans Bukuku alifurahi sana na kuongeza siku zake za uhai (maana wanasema kuka ni uhai pia).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Michuzi hivi kiingilio TSH ngapi nami niende siku moja nikacheke

    ReplyDelete
  2. Michuzi naomba utupe ratiba yake ili tuweze kuhudhuria showw zijazo

    ReplyDelete
  3. jamani kiswahili kigumu.. alipata "wasaha" maana yake nini? ungesema "wasaa" japo nacho sio kiswahili sanifu

    ReplyDelete
  4. Ankal, nimewahi kutoa maoni ya kukosoa onyesho hili lakini hukuyatoa, labda tunatakiwa tuwe tunatoa maoni ya kusifia tu ili yaweze kuwekwa humu. UKWELI NI KWAMBA WAZO LA ONYESHO NI NZURI MNO NA KWAKWELI TUNAPASWA KUMPONGEZA MWENZETU EVANS BUKUKU KWA KUWA MTANZANIA WA KWANZA HAPA BONGO KULETA NA KUISIMAMIA SANAA HII. LAKINI PIA KUNA MENGI YANAKERA KATIKA ONYESHO HILI AMBAYO YANAPASWA KUONDOLEWA ILI KUBORESHA NA HATA WALE AMBAO HAWAKUFIKA KATIKA ONYESHO WAJUE KWAMBA SIO KILA KITU KINAVUTIA KAMA AMBAVYO INASISITIZWA HAPA. KWA MFANO ONYESHO LA JANA NA MENGINE KADHAA NILIYOKWISHAWAHI KUhUDHURIA, KIJANA DOGO PEPE NDIYO AMBAYE SIKU ZOTE ANATIA FORA NA KUWAFUNIKA WENGI AKIWEMO EVANS BUKUKU MWENYEWE. KADIRI SIKU ZINAVYOKWENDA UBUNIFU NA UMAKINI WA EVANS UNAZIDI KUPUNGUA, SIJUI NI NINI LABDA AMELEWA SIFA, LAKINI ANAONEKANA KABISA KWAMBA AMECHOKA NA HAKIDHI MATARAJIO YA WENGI WANAOFIKA PALE. JANA NILIONDOKA KATIKATI YA ONYESHO WAKATI EVANS AKIWA JUKWAANI, HAKUWA NA JIPYA NA KWA KWELI ALIKUWA ANACHOSHA KUMWANGALIA. INABIDI ABADILIKE HARAKA. AONGEZE WASANII WENGINE HASA CHIPUKIZI. NA PIA AJENGE UTAMADUNI WA KUWAKARIBISHA WASANII/WACHEKESHAJI WAALIKWA HURU. ONYESHO LINACHELEWESHWA NA KUVUTWA MNO, NA PIA YANAWEKWA MAMBO MENGI YASIYO YA LAZIMA ILI MRADI KUPOTEZA MUDA.
    MC NAYE, ANATAKIWA AFANYE KAZI YAKE - LAKINI BADALA YAKE ANAKERA KWA KUJARIBU KUTAKA KUWACHEZEA WATAZAMAJI KAMA WATOTO WADOGO, WANAOKWENDA PALE NI WATU WAZIMA WALIOLIPA FEDHA ZAO KWA AJILI YA KUPATA BURUDANI YA VICHEKESHO, HIVYO MC ASILAZIMISHE VITU KWA WATAZAMAJI. KAMA TUNATAKA KUJENGA ANKAL UKWELI NAO LAZIMA USEMWE.

    ReplyDelete
  5. Michuzi, hivi kwanini huweki maoni yanayokosoa na unaweka yanayosifia tu!!!!!! hiyo si sawa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...