Nahodha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),Shadrack Nsajigwa akiwatoka mabeki wa timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) katika mchezo uliopigwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Mataifa ya Afrika 2013 nchini yatakayofanyika nchini Afrika Kusini.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Golikipa wa timu ya taifa ya Msumbiji, Joao Raphael akiwa chini huku mshambuliaji wa Stars, John Boko akikosa bao la wazi baada ya kubaki yeye na kipa tu langoni.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa Stars, Vincet Barnabas akimtoka Beki wa Timu ya Taifa ya Msumbiji,Stelio Ernesto.
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa (kushoto) akichuana na beki wa Msumbiji, Almiro Lobo katika mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwinyi Kazimoto akishangilia bao aliloifungia Stars na kuyafanya matokeo ya mechi hiyo kuwa 1-1
Kocha wa Stars Jan Poulsen (kulia) akipeana mkono na Kocha wa Msumbiji, Gert Angels mara baada ya mpira kumalizika.

Na Francis Dande

Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars, leo imeshimdwa kutamba mbele ya timu ya Taifa ya Msumbiji 'Mamba's kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kutoka sare ya 1-1 katika pambano la kuwania kufuzu Mataifa Afrika 2013 nchini Afrika Kusini.

Wiki moja iliyopita, Taifa Stars iliambulia sare ya 0-0 dhidi ya DRC katika mechi ya kujipima nguvu, huku gonjwa sugu la kufumania nyavu likionekana kushindwa kutafutiwa ufumbuzi na Poulsen kiasi cha kukigharimu kikosi hicho leo. 

Pambano hilo lililopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lilikuwa ni la kwanza kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Mataifa Afrika 2013 nchini Afrika Kusini, ambapo Stars imetoka sare ya bao 1-1 na Msumbiji. 

Stars iliyoingia dimbani ikitoka kuchagizwa na wakali kadhaa walioiwezesha Tanzania kufuzu fainali za mwaka 1980, ilionekana dhahiri kutokuwa katika mfumo wa kuweza kuibuka wababe, ikimtumia mshambuliaji mmoja John Boco ambaye alikosa mabao ya wazi.

Pambano lilianza kwa muendelezo wa kosakosa miongoni mwa safu ya mbele ya Stars, ambako dakika ya 15, John Boko alikosa bao, kabla ya kipa wa Stars Juma Kaseja kuokoa shuti la Clesio Bauque aliyekuwa mwiba katika safu ya ulinzi. Bao la Msumbiji lilifungwa na Clesio Bauque dakika ya 22, baada ya kuwatoka mabeki wa Stars kumpoteza Juma Kaseja langoni, kabla ya Mwinyi Kazimoto kusawazisha dakika ya 40. 

Kazimoto alifunga bao hilo kwa shuti la nje ya boksi, akimalizia pasi safi ya Vicent Barnabas. Hadi mwamuzi Moahammed Farouk Misri anapuliza filimbi ya mapumziko, timu zilikuwa sare kwa bao 1-1. 

Kipindi cha pili licha ya Stars kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Nozar Khalfan, Abdi Kasim na Vicent Barnabas na kuwaingiza Mrisho Ngasa, Salum Aboubakar na Husein Javu, bado iliendelea kukosa mabao kiashi cha Boco kuzomewa na pambano kumalizika kwa sare hiyo inayoweka shakani nafasi ya Tanzania kusonga mbele.

Taifa Stars: Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa, Stepheno Mwasyika, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Shabani Nditi, Nizar Khalfan, Mwinyi Kazimoto, John Bocco, Abdi Kassim ‘Babi’ na Vincent Barnabas.

Msumbiji: Joao Raphael, Edson Sitoe, Zainadine Junior, Eduardo Jumisse, Jerenias Sitoe, Elias Pelembe, Clesio Bauque, Francisco Muchanga, Stelio Ernesto, Francisco Massinga na Almiro Mohammed.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ndugu zangu, hata leo tumwite Wenger au Sir Alex afundishe Stars, itakuwa kama ilivyo. Michizi kubali ukweli post nachosema.

    1. Hata Jakaya hana imani tena na Tenga, yupo tff kwa maslahi yake na sio ya taifa. Leo mpira wa Tz haukuwa mbaya sana, lakini tujiulize kocha wetu amepewa mechi ngapi za majaribio? Wachezaji wanalipwa kiasi gani tangu waingie kambini, kama sio 15,000/- kwa siku?
    2. Wachezaji wazuri tunao wanacheza ndondo, sio kama hawaonwi lakini wanaulizwa wana shilingi ngapi ili majina yao wapendekezwe? ushahidi upo
    3. Fifa wanaleta vifaa na hela chungu mbovu tena original hasa vya waamuzi, kaangalie leo waamuzi wana vaa viatu gani, wengi wamejinunulia au wanavaa vya kichina vilivyo chakachuliwa na tff, hapo siongelei jinsi wanavyo zinguliwa malipom yao finyu.
    4. Makocha nao wanaingiliwa katika maamuzi yao ya kupanga list ama na kuchagua wachezaji, kutoka kwa viongozi wa tff au shinikizo la waandishi wa habari. Kocha wa sasa Paulsen, hajazunguka nchi nzima kuangalia vipaji, lakini huwezi kumlaumu kwani fungu kutoka tff la yeye kufanya hivyo lipo?

    #DAWA
    Watanzania wote tugome kwenda kuangalia meci za Taifa stars hadi pale tutakapo jiridhisha kuona inafanya vizuri.
    #TFF ivunjwe, ofkoz tutafungiwa na FIFA, tunatengeneza katiba mpya ya TFF, tutatengeneza uongozi mpya wa TFF na timu zetu za taifa kuanzia U17, U20 n.k kisha tuanajunga na FIFA watufungulie, kwani nchi nyingi wamefanya hivi ikawa poa.
    #Jezi, jezi yetu nayo nuxi! Jezi mbaya zina marangirangi kama kachumbari.....lol! Tuwe na mipango, mwaka huu tuamue jezi za mwaka huu ziwe nyeupe, kisha rangi za taifa mfn, soxi nyeusi, numb za wachezaji ziwe bluu, striips ziwe njano na kijani. Mwaka unaofuatia jezi ziwe njano, au bluu, au kijani na strips chache na ndogo mabegani au kifuani za rangi zilizobaki. Ili mwaka fulani tuseme kuwamwaka uilovaa jezi nyeupe ulikiuwa wa mafanikio.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  2. Msingeandika yote haya. Yaani habari nzima ingewakilishwa na sentensi moja tu:

    Stars kama kawa, droo.

    Wakishindwa:

    Stars kama kawa, yanyukwa.

    Mengine yote tunayajua, tumeshazoea.

    ReplyDelete
  3. E bana Maximo si tulimtimua kwa sababu ya kuwatosa Kaseja na Boban?
    Vipi babu hatutimui kwa kumtosa Samatta?

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza nakubaliana na wewe. Hata mimi sina imani na tff na taifa stars kwa muda mrefu sana sasa. Kila siku tunasema tuna vipaji, vipaji gani mbona hata huwa hatuvioni??? Mara timu ya uongozi ya tff, uongozi wa namna gani???

    Ni sawa kabisa, tff ivunjwe na taifa stars ivunjwe pia hadi hapo tutakapoweza kuongoza na kucheza soka, sio kuvaa vaa tai na kuchezeshwa soka kila siku.

    Namfahamu bwana mmoja huwa analalamika kila siku juu ya hii timu, huwa anasema angekuwa na mamlaka angeivunja timu ya taifa kwa miaka 5 ili watafakari upya wanatakiwa kufanya nini.

    Nilirudi bongo wakati fulani nikanunua vijezi jezi vya timu ya taifa, niliporudi ng'ambo nikawa navivaa kwa kujidai. Sasa hivi hata sijui viko wapi, naona kama nilijitusi tu kwa hela yangu mwenyewe.

    ReplyDelete
  5. TFF needs to be audited very seriously. And if not found to be a fraudulent scheme then money has no value at all to our national team. We probably need to devise some idiosyncratic theories (unrelated to money) to resuscitate our soccer. Maybe witchcraft, only?! Maybe food?! Or, not surprisingly, maybe no soccer at at this level for us?!

    ReplyDelete
  6. Kwa kuangalia na kulinganisha mpira wa Stars zamani na siku hizi mimi naona tofauti kidogo. Siku hizi Stars inaingia ndani ya kumi na nane ya timu pinzani, ina shots on goal kibao, ina magoli ya kufunga hata ugenini, haichezewi tena nusu uwanja upande wetu. Na hii nimeanza kuiona hata kwenye klabu zetu kubwa kwenye mashindano ya CAF, Yanga na Simba. Wanamiliki mpira, wanaingia ndani ya 18, shots on goal sinaridhisha, wanafunga ugenini.

    Mimi nadhani ni jambo la kutia moyo. Yaani at least binafsi naanza kuona mwanga mwisho wa tanuli.

    Go Taifa Stars! Go Yanga!OK.....Go Simba!

    ReplyDelete
  7. Babu ni Mbishi sana ndio tatizo lake kubwa,,,

    Kwa kawaida Binaadamu yeyote anayetokea kujiona kuwa yeye ndiye sahihi zaidi mara nyingi mwisho hukwama!

    '''''''NO ONE IS PERFECT''''''', WEWE UKIJUA HILI WENZIO WANAJUA LILE NDIO KILIMWENGU,TUTAKE TUSITAKE!

    NDIO MAANA PANAKUWA NA BUSARA YA KUBADILISHANA MAWAZO KUYAFANYIA KAZI NA KUTEKELEZA LINALOFAA KWA FAIDA NA SIO UBISHI USIO NA TIJA.

    RAISI KIKWETE TUMUONEE HURUMA SANA KWA KUWA KAZI ALIKIWISHA IFANYA KTK TASNIA YA MICHEZO HASA SOKA, LAKINI ANARUDISHWA NYUMA NA KUFADHAISHWA KWA HALI KAMA HIZI.

    NI WAKATI WA BABU M DENMARK ARUDI KWAO ZIZINI AKAWATIBU NG'OMBE WA MAZIWA KWA UDAKITARI WAKE WA MIFUGO!

    ReplyDelete
  8. Jezi nyeupe haha England naona wanavaa nyeusi jana wamepigwa bao 3 na jezi zao nyeupe jezi haichezi hata uvae kama brazil hutacheza km wao uongozi mbovu wachezaji wabovu Zambia wanapesa kuliko sisi mbona wanashinda hii timu inatia hasira sana .sitaki hata kusikia

    ReplyDelete
  9. Kuna usemi "numbers don't lie" yaani namba haziongopi. Kama kuna mdau ana uwezo akusanye takwimu zenye kuonesha rekodi ya Maximo ukilinganisha na ya Poulsen tuone nani ana uwiano mzuri zaidi wa kushinda na uwiano mzuri wa kutofungwa.
    Huyu kocha anapapatikiwa kwa vile tu ni mzungu lakini hajawa na msaada kwetu. Kila siku analaumu wachezaji wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...