TAMASHA la Pasaka litakalofanyika Aprili 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam limepangwa  kurindima kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema kuwa, kamati yake ilipokea maoni kutoka kwa wadau wa muziki huo na kuamua kufanyia tamasha hilo katika uwanja huo.

"Lengo letu ni kufanya tamasha letu katika sehemu kubwa ambayo itamwezesha kila mtu  atakayekwenda kushuhudia, aridhike," alisema.  Mwaka jana, tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo wadau wa muziki huo walifurika na wengine kushindwa kuingia ndani.

Msama alisema baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es Salaam, tamasha hilo litahamia mkoani Mwanza, katika Uwanja wa CCM Kirumba.  Kutokana na tamasha hilo kuwa la kimataifa, Mwenyekiti huyo wa kamati ya maandalizi,   aliwataka wafanyabiasha kujitokeza kudhamini tamasha hilo kubwa nchini.

Mpaka sasa, baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na nje ya nchi wamethibitisha kushiriki, lakini kwa sasa wanaendelea na taratibu za kupata kibali cha kufanya kazi.  "Tayari baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na nje waliopelekewa mialiko, wamethibitisha kushiriki, kilichobaki ni kushughulishia vibali vyao," alisema.

"Bado tunapokea maoni kutoka kwa wadau wetu, tunaomba mzidi kututumia ili tuyafanyie kazi kabla ya tarehe ya tamasha hilo," alisema.  Tamasha la Pasaka mwaka huu litafanyika Aprili 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Aprili 9 litafanyika mkoani Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hili tamasha imekuwa biashara? Mbona hatuoni popote kama injili itahubiriwa? Au mnaalika waimbaji ili watumbuize na kuburudisha watu tu? After all katika tangazo lote hili sijaona kutajwa YESU au MUNGU, nina wasi wasi kama tamasha hili linahusu kuujenga ufalme wa Mungu.

    ReplyDelete
  2. sio wote wanaosema bwana bwana watakoaingia paradiso.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...