Habari Ankal Michuzi,Natumai unaendelea vyema wewe na timu yako nzima inayoliendesha libeneke la Globu ya Jamii.Mungu awajaalie zaidi na zaidi kwa mnatujuza mambo kwa haraka sana.

Naomba uwafikishie hili Wadau wa Globu ya Jamii,Nimeamua kutoa msaada mdogo tu kwa watanzania wawili au watatu ambao wamepata greencard ya kwenda USA lakini wanakosa mwenyeji/pakufikia mpaka pale wanapokuwa tayari kujitegemea. Nina nafasi ndogo nyumbani kwangu ambayo nimeamua kuitumia kwa jinsi hiyo.

Kama umepata greencard ya kukuwezesha kuishi na kufanya kazi Marekani na unahitaji mwenyeji tafadhali nitumie email kwa dartous@gmail.com

Kwa ajili ya ufinyu wa nafasi, nitaweza kuchukua watu walio single tu bila mke/mume/watoto.
Kama ungependa pia msaada kutafuta kazi tafadhali weka Jina, Umri, Mke/Mme, Elimu, au hata CV kama unayo.

Ahsante Sana na Lidumu Libeneke la Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. mambo ya misaada toka ughaibuni bila masharti,yawezekanaaa?

    ReplyDelete
  2. Mdau hongera sana kwa maamuzi mazito uliyoyafikia hasa wakati huu nchi inapokuwa kwenye recovery baada ya kuyumba kwa uchumi. Hakika wewe ni mfano wa kuigwa na Mungu atakubariki na kukuongezea pale utakapopunguza.

    ReplyDelete
  3. Mmmhh, ni kweli unatoa nafasi ya mtu/watu kuishi bure au kuna agenda ya siri? Pengine kwanza tukujue zaidi, Criminal records, employment, or business zako, etc! Si unajua hao watu unaowakaribisha ughaibuni watakuwa wageni kwa kila kitu, wasije kuingizwa mtoni. Kama kweli ni msamalia mwema,nadhani hautaona shida kushare hizo brief particular!

    ReplyDelete
  4. mmh!!!!! Mbona hajajilisha. Na hamna full address

    ReplyDelete
  5. sasa kama unatoa msaada CV ya mtu ya nini?

    ReplyDelete
  6. popobawa mzee wa majunguFebruary 23, 2012

    Hatimayeeee madalali waanza kuvuka mipakaaaa, na kuendelea kufanya mambo kwa madahaaaaa( kwa sauti ya Masako au John Maratu wa ITV).

    ReplyDelete
  7. That's true America spirit.

    Keep up brother or sister.

    ReplyDelete
  8. Nakufagilia mno mdau wa moyo wako wa upendo. Mungu akuzidishie pale ulipo-pungukiwa.
    Mdau - South Korea

    ReplyDelete
  9. Ningependa kumpongeza mdau huyu wa marekani aliyejitolea kusaidia watanzania wenzake. Kujitolea kama hivi kwa kweli mi nadra sana kutokea na ningependa kuona mfano huu mzuri unaigwa na watanzania wengine walio ughaibuni kwani kusaidiana ndio kufikishana pazuri. Wenzetu wa nchi za magharibi wanasaidiana sana kwa hiyo na sisi watanzania hasa wale walio ughaibuni tuige mifano kama hii. Bila shaka mdau huyu pia alipata msaada kama huu na yeye akaona ni vizuri asaidie wengine. Tuzidi kusaidiana. Asante.

    ReplyDelete
  10. Hongera sana Mdau wa Marekani unaye waalikwa wandugu kuja kuishi na wewe wakiwa Uhamishoni.

    Ni watu wacheche sana katika zama hizi wenye moyo kama wako.

    Mungu Akuzidishie Baraka, Amiiiin!!

    ReplyDelete
  11. mshikaji rent imekushinda unataka watu uwaviligize,wao wameweza kuomba wakapata,watashindwa kujua pa kufikia.fanya kazi ulipe kodi zako usitafute watu ukajifanya uwatunzie na dollar zao.

    ReplyDelete
  12. Mhhhh Mdau tupo pamoja naomba nimnukuu mwenye tangazo "nimeamua kutoa msaada mdogo tuu kwa watanzania wawili ama watatu" Mdau Nadhani hapa ungekua a bit specific maana mtu anaweza kurupuka na green card yake hapa akifika huko hajajipanga vyema kumbe anatakiwa alipe. Hebu kua more specific uNgeweka "with No Fee" ingeleta maana zaidi. au kwa bei ya Kusaidiana kama wanyumbani. Ingeeleweka.Maana hii misaada hata tunayopokea toka nchi zilizoendelea kama huko ailipo mdau anayetoa huu msaada.Zikitoa misaada inamasharti sana. So mdau Be specific.Ni hilo tuu.

    ReplyDelete
  13. Mdau,

    Mungu akuzidishie... ni kweli watu wengine hushindwa sehemu ya kufikia.. mimi binafsi nimeshasaidia mara mbili na wala haichukui muda kwa mtu kupata green card yake na kuanza maisha USA. wageni wangu wote 2 walikaa nami kwa miezi 3 tuu wakawa na kazi na wakawa na kwao. Watanzania tuendelee kusaidiana.

    Mzalendo

    ReplyDelete
  14. This sounds like a truly altruistic offer, unless mdau has other ulterior motives, well done mdau, tufuate nyayo wajameni.

    ReplyDelete
  15. Tunashukuru kwa msaada wako ni bure au kunamalipo na kama inawezekana tunaomba utupe makadirio pls Asante sana

    ReplyDelete
  16. doubtful aid. anyway, be blessed.

    ReplyDelete
  17. kutoa ni moyo, mungu atakulipa maradufu...kuna watu wana ma-mansion lakini hata kukaribisha kwa chai hawawezi wanaogopa kuchafuliwa ma-carpet

    ReplyDelete
  18. Sasa hujatueleza uko state na city gani huko US. Vile vile kazi za za ina gani unaweza kuwasaidia hawa jamaa utakaowakubali kufukia kwako.
    Na kwa hisani yako tunaomba jina lako kamili na sio email peke yake. Maana ya kuuliza hivyo ni kwa sababu hayo unayosema mimi binafsi yananipa wasiwasi, na kwa ninavyoifahamu US. "nisifahamike vibaya" tafadhalini.

    ReplyDelete
  19. Mdau wa kwnza,
    Hakuna kitu kibaya kama kufikia ughaibuni kwa mtu usiemjua. They will always try to take advantage. Kaeni chonjo.

    ReplyDelete
  20. mmmh yaani single tuu? Naona umeshau jinsia.

    ReplyDelete
  21. Huyu bwana anatafuta watu wakumsaidia kulipa mortgage

    ReplyDelete
  22. Hongera ila nina mashaka na dhamira yako.

    ReplyDelete
  23. Huyu jamaa ana walakini!!! nakwambia msikubaliii hata kidogo... Nina mashaka naye sanaaaa tuuuuuuu... Nawaambie, don't fall for it!!

    ReplyDelete
  24. Du, huo wema wa kuhost waTZ wenzako umeuanza lini?Au kuna vested interest over the mission

    ReplyDelete
  25. Anony wa Thu Feb 23, 02:20:00 PM 2012

    Nami napata mashaka kawaida huwa hivyo ulivyosema...Msaada hivi hivi tu!?

    ReplyDelete
  26. kaka marekani ni nchi kubwa sanaa,mji gani?

    ReplyDelete
  27. I didnt know angels still exist!! Ni hayo tu. Mlavumbi Orijino

    ReplyDelete
  28. jamani wabongo msikubali,mnakumbuka miaka michache iliyopita,kuna msichanna wa kitanzania alipata msaada na mtanzania huku US?matokeo yake mwenyeji wake alimchinja dada wa watu nakutupa mwili kama taka.njoo na shida zako kwenye ubalozi wa Tanzania,watakuelekezo utapa msaada tuu.mdau US.

    ReplyDelete
  29. hata mimi natia shaka na huu msaada wa huyu muungwana yaani sasa hivi marekani kulivyo na shida ya kupata kazi halafu mtu aseme atakusaidia mpaka hapo utakapo pata kazi na hali ya maisha ilivyo gali hii aiingii akilini kabisa hapa lazima kuna kitu ambacho sio cha kawaida huu wema sio bure otherwise km hakuna kijume na alivyoandika ni jambo jema

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...