Na Mary Ayo,ARUSHA

MAMLAKA ya chakula na dawa mkoa wa Arusha (TFDA) imeteketeza bidhaa
  vikiwemo vipodozi mbalimbali visivyofaa  kwa matumizi ya binadamu ,zilizokuwa kwenye mzunguko wa kibiashara zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20.

Bidhaa  hizo ni pamoja na vyakula mbalimbali vilivyoisha muda wake,
vipodozi vilivyopigwa marufuku , madawa bandia ya binadamu  na bidhaa zisizosajiliwa.

Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi mara baada ya kuteketeza
  bidhaa hizo, katika dampo la manispaa lililopo Muriet jijini hapa , Mkaguzi wa dawa wa TFDA kanda ya kaskazini, Bw Elia  Nyeura alisema kuwa,kupatikana kwa bidhaa hizo ni  kutokana na operesheni waliyoifanya kati ya januari 3 hadi 25 mwaka huu,katika wilaya tatu zilizopo mkoani  Arusha.

Alisema  operesheni hiyo imefanyika katika wilaya tatu ambazo ni
Arusha mjini,Arumeru na karatu na  kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo walifanyatathimini na kujiridhisha kuwa maeneo hayo yamekuwa kichaka cha  bidhaa hizo zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

Aidha alieleza kuwa  jumla ya vituo vya afya na maduka ya madawa ya
  binadamu 131 wameyafanyia ukaguzi, pamoja na maduka ya vyakula 60 yaliyopo katika wilaya hizo yalikaguliwa.

Aliongeza kuwa miongoni mwa dawa zilizoteketezwa ni pamoja na dawa za
kuongeza makalio aina mbalimbali , kwa upande wa  baadhi ya vipodozi vilivyozuiwa na serikali ni pamoja ,G$ G  Cream,Carottene,Bio Carote,Carolight,Mekako ,Maxi light na vinginevyo ambapo alifafanua kuwa vipodozi hivyo vimegundulika kutengenezwa na madini hatari , aina ya Hyroguinine,Steroids,Bithionol,mercury (Zebeki).

Alieleza kuwa  athari kubwa kwa matumizi wa vipodozi hivyo ni pamoja
  na kupatwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi, akina mama kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na kupatwa na athari ya uharibifu wa ini na figo na kwamba athari hizo humpata mtumiaji kwa muda mrefu bila yeye kujitambua.
 Amewataka  wafanyabaishara kuwa makini na bidhaa bandia nazile zilizoisha muda wake ,kadhalika  kuwacha kuingiza nchini bidhaa zilizopigwa marufuku na serikali ,kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria na taratibu za nchi na wahusika watachukuliwa hatua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tatizo siyo kuteketeza,wakati umefika kwa watanzania kusikia ni watu wanagapi kesi zao ziko mahakamni na wamefungiwa biashara zao.Ukiteketeza kuna watu wana store nyingi,unakamata ukishaondoka tu,in 1 hour anrudisha dukani-hadi urudi mwakani tena ameshaathiri watu wengi.
    Tunataka sheria na utendaji viendane.Hiyo ni sawa na kumkamata muuza dawa za kulebya unasema nimempokonya na hivyo hazikuingia sokoni huku nadunda mtaani.
    Kazi tunayo na kazima kieleiweke.Mbona wenzetu Ulya wameweza??

    ReplyDelete
  2. huwa zinaingiaje nchini??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...