Na Mwandishi Maalum – Ruvuma
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kuwa uchimbaji wa madini ya uranium hauna madhara.
Dk. Bilal ametoa kauli hiyo baada ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kueleza kwenye mkutano wa hadhara kuwa pamoja na nia nzuri ya serikali ya kuanzisha mradi huo baadhi ya watu wamekuwa wakipita kwenye vijiji kikiwemo cha Likuyu Sekamaganga wakipotosha wananchi kwamba madini hayo
yana mionzi ambayo yana athari kwa binadamu na hasa kwa wanaume.
Makamu wa Rais alipata fursa ya kuzungumza na wananchi hao wa Likuyu Sekamaganga wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Namtumbo baada ya kutembelea kampuni ya MANTRA inayotekeleza mradi huo na kujionea shughuli za utafiti wa uranium zinavyoendelea.
Dk. Bilal ambaye amebobea katika masuala ya nyuklia alisema ni kweli kuwa madini hayo ambayo yako chini ya ardhi yanatoa mionzi lakini aina hiyo ya mionzi haina nguvu sana na inazuilika kitalaamu.
Hapa tulipo kuna mionzi. Watalaamu wameweka kiwango cha mionzi binadamu anaweza kuhimili. Mtu unapougua unaenda kufanyiwa X-Ray ni mionzi, ma-TV ya zamani yale ni mionzi, hewa hii tunaivuta inatoa mionzi, mionzi ni maumbile ya kiulimwengu,” alisema na kuongeza.
Alisema kwa hapa Tanzania kuna Tume ya Atomiki yenye makao yake makuu kule Arusha ambayo imekabidhiwa kazi ya kuhakikisha wananchi wako salama kutokana na mionzi ya madini na vifaa.
“Msiwe na hofu ye yote. Sisi tunasimamia usalama wenu. Tuna watalaamu wa kutosha, taasisi za uhakika. Kama kuna hatari mimi nitakuwa wa kwanza kusema. Watalaamu wapo watashirikiana na wa wilaya na mkoa kuhakikisha usalama wenu,” alidokeza
Dk. Bilal aliwataka wananchi kupuuza upotoshaji huo kwa kuwa mradi huo una faida nyingi ikiwemo ya kuzalisha umeme kwa urahisi na kutoa ajira jambo ambalo litasaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wenyewe, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Kampuni ya MANTRA Assah Mwaipopo kazi ya upembuzi yakinifu imekamilika, sasa hivi kinachoendelea, wanasubiri kupata majibu ya maombi ya leseni kutoka UNESCO kutokana na eneo hilo kuwa chini ya urithi wa dunia ili shughuli za kujenga mgodi zianze na hatimaye
wafanikishe matarajio yao ya kuanza kuchimba madini hayo ya uranium ifikapo mwaka 2014.
Dk. Bilal ambaye amemaliza ziara yake katika wilaya za songea na Namtumbo,leo Feb 16, pamoja na mambo mengine atatembelea na kukagua mradi wa makaa ya mawe huko Mbinga.
Atakamilisha ziara yake ya mkoa wa Ruvuma kesho Feb 17 kwa kufanya majumuisho na viongozi wa chama na serikali wa mkoa huo kwenye ukumbi wa UMATI mjini Mbinga na baadaye ataelekea mkoani Rukwa.
Sawa Dkt. Bilal, madini hayana madhara isipokuwa Mradi uwe unaakisi faida za Kiuchumi kwa Wakazi wa hapo na Taifa kwa Ujumla badala ya kuwafaidisha Wawekezaji pekee na watu wachache karibu nao.
ReplyDeleteTatizo hawa Wageni wanaichukulia Afrika na Tanzania ikiwemo kama Shamba la bibi na Msitu wa kuvuna Rasilimali za bure.
Unakuta sehemu inachimbwa Dhahabu, lakini Kijiji kinacho pakana na Mgodi wa Mwekezaji huyo aliyewekeza Mradi wa Mabilioni ya Shilingi (HUKU AKIVUNA MABILIONI YA FEDHA) Nyumba za wakazi ni duni za nyasi,Zahanati mgogoro,Maisha magumu na duni, huku Shule ya Kijiji ikiwa ya Udongo kuta zinataka kuanguka!
IMETOSHA,,,YA NAMNA HII TANZANIA YETU TASITOKEE TENA!
duh sihamini kabisa
ReplyDeleteTatizo kubwa mtu anaweza kuwa Msomi, Mhandisi, Mwanasheria ,Dakitari kama wewe, na kada za Taaluma kadha wa kadha lakini akikutokea katika Staili ya Kisiasa anakuwa kama vile hajasoma!
ReplyDeleteTumeona ktk kadhia kadhaa zilizojiri ilikuwa ni vigumu kuoanisha Mtazamo na Msimamo wa mtu huyo Kisiasa inakua havifanani kabisa.
Anakuwa na Mtazamo ambao ni Mzungu wa nne (Msimo wa kinyume nyume) tofauti na jinsi unavyofikiria au kumtegemea yeye kuwa.
KIUFAFANUZI NI KUWA MTU AKIWA KISIASA ANAKUWA NA SHABAHA YA KUFIKIA MAAZIMIO AU MALENGO KWA NJIA YA MKATO TU HAANGALII UPANDE WA PILI AU HATA KAMA AKIJUA ANA KAA KIMYA.
Hivi nyie viongozi mliopo madarakani sasa, mnadhani kuwa baada ya ninyi hakutakuwa na maisha tena, au kutakuwa kiama? Bkoz inaonyesha mmejiapiza kubinafsha, kuchimba kwa ubia sekta zote za madini ili kwamba kizazi kijacho shauri yao.
ReplyDeleteUchimbaji wa madini unaoendelea hauna tija kwa watanzania, hakuna improvrmnt yeyote ktk mikataba ili kuboresha mapato yetu.
Swali, kuna haja gani ya kusaini uchimbaji mwingine hasa uranium kabla ya kuboresha mikataba iliopo? Mmerekebisha kipi kilichokuwa na kasoro kwenye mikataba mingine ambacho kitaleta ufanisi katika mikataba ya uranium?
Nyerere alijua uranium gold nk tunavyo, lakini hakukubali kuchimba kwakua alijua wawekezaji walikuwa na nia ya kujineemesha wao kuliko sisi. Macho yenu hayayaoni haya? Au ni nini kinawaziba macho na masikio kutoka kwa wawekezaji wanyonyaji? Lets love our country.
Kibanga Msese
Nimesoma website hii inayoitwa www.worker-health.org/org ambayo inaelezea kuwa hayo madini ya uranium yanakuwa na madhara kwa binadamu kama vile kuharibu figo,moyo na kuongeza pressure.
ReplyDeleteBwana Mhariri ,Je hii habari ni kweli au watu wafuate huu msimamo huu uliopo katika hii makala yako??
mdau
Dr.Bilal hao wameingia kwenye anga zako mkuu enzi za UDSM.Mambo ya Radioactivity,mambo ya Half-life time&decay....dN/dt=-λN.Ilikuwa balaa.Kama hujaongea kisiasa basi ulichokisema ni ukweli,tulieni wananchi wa Ruvuma,huyo ndiye mwenyewe kwenye hayo masuala.MANTRA na nyie jitahidini kufuata taratibu za uchimbaji wa madini hayo.
ReplyDeleteDavid V
hata kama ina madhara mutasema na hela za watu mumesha kula,
ReplyDeleteHuo uzalishaji wa umeme wa Uranium unahitaji Nuclear technology ambayo mataifa mengi duniani yanazuiwa kuitumia...sasa ninyi viongozi mnapoongelea kuwa tutafaidika manataka kuniambia tumeruhusiwa kuweka umeme wa Nuclear? vibali na technologia mnavyo au USA watawakatalia kuwa wao wataichimba wabebe wapeleke kwao sisi watuachie madhara tu na pesa tusizione? Hebu jamani tufungueni macho msitudanganye. Mdau-NYC, USA
ReplyDeleteHuo uzalishaji wa umeme wa Uranium unahitaji Nuclear technology ambayo mataifa mengi duniani yanazuiwa kuitumia...sasa ninyi viongozi mnapoongelea kuwa tutafaidika manataka kuniambia tumeruhusiwa kuweka umeme wa Nuclear? vibali na technologia mnavyo au USA watawakatalia kuwa wao wataichimba wabebe wapeleke kwao sisi watuachie madhara tu na pesa tusizione? Hebu jamani tufungueni macho msitudanganye. Mdau-NYC, USA
ReplyDeleteHuyu Dr, Bilal ni Dr. wa physics sasa kama hamumuamini yeye sasa sijui mtamuamini nani? Watu si walituambia tusitumie cellphones tutapata cancer ya ubongo? Yako wapi? ChimbaChimbaChimba mungu ametupa hayo... hata kama hatutafaidi sisi, wazungu watafaidi au tutaufuata umeme huko huko.
ReplyDeleteHahahahahhhhaaaaaaaaaaaaa, eti tutaufuata huko huko.. kazi kweikwei
ReplyDelete