Ankal,
Habari za leo.
Kwa masikitiko makubwa sisi wananchi tunaoishi maeneo ya karibu au pembezoni mwa kiwanda cha saruji cha wazo hill, tunaathirika na uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na moshi wa kiwanda hicho.
kama unavyoona katika picha zote mbili,tunaomba kufahamishwa kupiti blog yako kama kuna hatua zozote zinazochukuliwa au kudhibitiwa na mamlaka husika hususani NEMC.
Jamani je,tutapona kwa hali kama hii.
Mdau.
Mwanamazingira
nani alifuata mwenzie kiwanda au wakazi?
ReplyDeletekwa hili wa kulaumiwa ni mamlaka zinazohusika pamoja na nyinyi wananchi wenyewe mliokifuata kiwanja kwa kujenga jirani yake, kwani kiwanda kilipojengwa walizingatia masharti kuwa kijengwe nje ya makazi ya watu, miaka hiyo kiwanda kilikuwa porini kabisaa mbali na makazi ya watu, lakini kwa mshangao wananchi wakaanza kusogea kidogo kidogo na mamlaka zinazohusika zikaliachia, sasa wakuhama ni nani kiwanda au wakazi, jibu wanalo wataalamu wetu wa mipango miji kama wapo!!!
ReplyDeleteKunatakiwa kuwe na buffer zone ili kupunguza athari ya mambo kama hayo.
ReplyDeleteSamahani lakini kiwanda hicho kimejengwa miaka mingi sana na nyinyi ndiyo mulivamia maeneo hayo. Na hata kiwanda cha saruji kilipojitetea kuwa hilo ni eneo lake siasa zikaingia kati. Leo consequences zake ndiyo hizo.
Ningewashauri wananchi wote kutokubali kununua maeneo karibu na viwanda, maeneo ya bondeni au karibu na kingo za mito ili kuepuka athari za kimazingira.
Haya ni maoni yangu binafsi.
Naishi hapa Wazo. Runabadilisha shuka kila baada ya saa mbili,
ReplyDeleteNaishi hapa Wazo. Tuunabadilisha shuka kila baada ya saa mbili,
ReplyDeletena mimi nilitaka kumuliza swali hilo hilo mdau mleta mada, mlitumwa kujenga karibu na kiwanda hicho?ni nyie wenyewe mmenunua viwanja bila idhini ya serikali karibu na kiwanda ondokeni nyie, eti mnajenga huko kisa muonekane mpo mbezi beach, kula vumbi sasa.
ReplyDeletenyie ndio mchukuliwe hatua ya kuhama
Kweli akili ni nywele. Kila mtu ana zake!
DeleteHili ni tatizo kubwa sana kwetu,,,Tahadhari ya Maafa ya Kimazingira licha ya maendeleo ya makazi.
ReplyDeleteNi kweli Kiwanda kilijengwa wakati eneo la Wazo Hill kukiwa Porini kabisa isipokuwa Makazi yakafuatia kutokana na maendeleo ya Makazi na Ustawi wa Jamii.
Nimesoma High School Ununio Boys Islamic Seminary from 1992-1994 moshi huo tuliukoga kwa miaka hiyo miwili.
HIVYO ilitakiwa suala la tahadhari ya athari za mazingira kwa Wakazi zichukuliwe sambamba na Maendeleo ya Makazi yaliyopelekea kufikia eneo hilo.
Tatizo sio kujenga karibu na kiwanda na wala issue hapa sio kuhamisha kiwanda.. Cha msingi ni kiwanda kukinga moshi wote na kuushusha chini ku-recycle kama walivyofanya kwa kiwanda kipya cha hapo hapo wazo . Kwa nini wasiweke system ya kukinga moshi kama ya kiwanda kipya??? Au rushwa imetawala NEMC katika kufuatilia?? Tanzania bana kweli ni kichwa cha mwendewazimu... Kazi kuunda regulatory authority milioni 7, laki 9 arobaini na 2 lakini hamna hata moja inayofanya kazi ila SIHASA (siasa)
ReplyDeleteWabongo kwa kulalamika tu! kupona hamponi ng'o, cha msingi mhame tu maana mmekifata kiwanda wenyewe kwa raha zenu. leo hii mnamtaka eti NEMC ichukue hatua, aarghhh...inakera!
ReplyDeleteInawezekana kweli Kiwanda kilitangulia kujengwa,na watu wamekifuata Kiwanda, bila shaka athari hii ni shule kwao, lakini shule hii iwe pia kwa Mamlaka husika kwani viwanja katika maeneo haya vipo vilivyopimwa, sasa swali ni kuwa Mamlaka husika ilipima na kugawa viwanja katika maeneo hatarishi? Manispaa ya Kinondoni iweke kumbukumbuku zake wazi tuzione. Nadhani kuna ukosefu wa uadilifu mahali fulani!
ReplyDeleteyaani nasupport kwa asilimia 200!! ni mchosho mkubwa sana mavumbi usiseme watoto ni kukohoa kila kukicha jamani tunashindwa kuelewa hali hii, mambo ya kujenga karibia na kiwanda sisi wengine tuko mbali lakini lile vumbi linatembea umbali mrefu sana jamani msiseme hali ni mbaya mno!!!
ReplyDeleteTusiwe na mtazamo finyu kuhusiana la hili suala, cha msingi kile kiwanda kinatakiwa kuwa na mfumo unao contain moshi usitoke na kusambaa, hivi unaposema kwamba watu walikifuata kiwanda, unafikiri ni kwa umbali gani watu wanatakiwa kuishi toka kwenye kiwanda hicho, hii ni kwa sababu yale mavumbi yanasambaa kwenye eneo kubwa mno, wakati mwingine huenda mpaka sala sala. kama ni suala la kutokifuata kiwanda inabidi watu wasiishi kwenye km za mraba kubwa sana zinazokizungukz kiwanda. pili kuna suala la kuharibu ozone layer, na yenyewe itatakiwa kukikimbia kiwanda? au madhala yatokanayo na kutoboka kwa ozone yanawapata wanaoishi karibu na waharibu ozone?
ReplyDelete