Wafanyabiashara wa kuuza Kuku katika soko kuu la Arusha ambao hawakufahamika majina yao wakiwa wamewabeba kuku hao kwa kuwaning'iniza vichwa chiki,huku wakikatiza mitaani bila hata wasi wasi wowote.Wadau mnalizungumziaje hili la ubebaji wa namna hii??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. asante sana kwa kuleta hili suala , jamani huu ni unyama, unyama, unyama, ningekuwa na uwezo ningebadilisha sheria , pia watu wanahitaji kuelimiswa nimefurahi sana kwa kulitoa suala hili . naomba usichoke sio kwa kuku tuu na wanyama wengine wote .

    ReplyDelete
  2. ndio maana ikifika kupika huyo kuku unamchemsha masaa 3 haivi kwa ajili ya mateso aliyoyapata....

    ReplyDelete
  3. Hivi hawa wabebaji hawakufika hata darasa la tatu na kusoma kile kitabu cha kiswahili, hatua ya kwanza, chenye hadithi ya "Jogoo Aliyesema"? Au ile hadithi haikufandusha chochote?

    ReplyDelete
  4. kama watoto wa binadamu na albino wananyanyaswa hakuna anayejali sembuse kuku!!
    Arusha kuna TSPCA cha ajabu hawajui kazi zao inabidi kuku mvumilie tu kwani hata mpelekwako sulba iko pale pale!

    ReplyDelete
  5. hakika umesema kweli muschi b.c, binadamu wananyanyaswa na binadamu wenzao na wanatakiwa kukaripia au kuzuia hilo wako kimyaaa kama hawajui kitu chochote...sembuse kuku? au wanyama wengine?...njoo utembelee pemba uone ng'ombe wanavyosulubiwa huku, ukiwa huna ujasiri unaweza kulia wakati mwingine...ni mazoea sijui ni kitu gani, mimi binafsi siwezi kabisa kumsulubu mnyama yeyote yule ingawa naweza kuchinja lakini kwa kum-handle vizuri....nawaalika watu wanaoshughulikia mambo ya haki za wanyama waje pemba wajifunze..wanyama tumepewa ili tuwatumie lakini lazima kuwe na mipaka ya huruma jamani.

    ni mtazamo tu

    ahsante
    hsm

    ReplyDelete
  6. ukiona hivyo huyo mbebaji hana huruma hata kumnyayasa mwanadamu mwenzie kwke ni kitu rahisi sana. kichwa juu miguuu chini kutwa nzima!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...