Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa mpango wa kupambana na magonjwa yaliyopewa kipaumbele ukiwemo wa usubi ,mabusha na macho , ambao ni pamoja na Madaktari , Wataalamu ,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (hayupo pichani)  wakiwa katika ufungua mkutano huo wa siku mbili unaoendelea kufanyika mkoa Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kati kati waliokaa) akiwa na Dk Frida Mokiti ( kushoto) ambaye ni Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na ( kulia ) ni Mkurugenzi Mkazi nchini wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Sightsavers ,Dk Ibrahim Kabole, wakiwa katika picha ya pamoja na Madaktari, Wataalamu na wadau wa mpango wa kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele nchini, mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa mpango huo, Februari 20, mwaka huu mjini hapa.Picha zote na John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kuna watu akili zao zimekuwa tuned kuwa wakati wowote wanapopigwa picha ni lazima watabasamu. Mimi huwa siwaelewi kabisa zaidi ya kuwaona feki.

    ReplyDelete
  2. Unapopigwa picha ni lazima utabasamu kama hiyo shughuli inayohusisha hiyo picha si ya kulia au kusikitisha.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa pili, naungana na mdau wa kwanza japo kidogo tu kwa kuhoji furaha iliyomo katika magonjwa. Jamani!

    ReplyDelete
  4. Wadau sioni tatizo la mtu kutabasamu, unajua ni nini kilikua kinaongelewa wakati picha inachukuliwa?tusipende kukosoa kwa kila tunachokiona. Naungana na mdau wa pili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...