Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni (mstaafu) Chiku Gallawa akitazama moja ya mifuko ya kufungashia bidhaa inayotengenezwa na kiwanda cha Pee Pee Tanzania Limited (PPTL) kilichopo Jijini Tanga, mfuko huo ni wa kiwanda cha Simba Cement cha Tanga. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa PPTL Bw. Jonathan Lane (kushoto kwa RC), anayemfuata ni Bw. Chetan Taishete (mdhibiti wa fedha PPTL), kulia kwa RC ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi na Bw. Dominick Mtemangwa Meneja wa kiwanda cha PPTL.
Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha PPTL, Bw. Lane akimweleza jambo Mkuu wa mkoa wa Tanga, Mh. Chiku Gallawa alipotembelea kiwanda hicho kuona uzalishaji ambapo hapo alikuta mifuko mingi ya viwanda mbalimbali hapa nchini kama kulia mifuko ya kiwanda cha saruji Mbeya.
Mkuu wa mkoa akitembelea kiwanda cha Arthi-River kuona namna wanavyoendelea na ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kukamilika kwake kutaufanya mkoa wa Tanga uwe na viwanda viwili vinavyozalisha saruji.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Gallawa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kiwanda cha saruji kipya cha Arhi-River kitakachozalisha saruji chapa Rhino-Cement. Kiwanda hicho bado hakijakamilika licha ya ungozi wa kiwanda kumwahidi Rais Jakaya Kikwete alipofungua kiwanda hicho mwaka 2010 kwamba kitamalizika katika kipindi cha miezi 24 lakini hadi sasa ujenzi wake bado haujakamilika ni kiasi cha asilimia 54 kimekamilika na kinatarajiwa kukamilika mapema mwakani.

Na Mashaka Mhando,Tanga

WAWEKEZAJI wa sekta ya viwanda mkoani Tanga, wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa vijana wenye utaalamu wa kuendesha mashine mbalimbali za viwanda vyao.

Akizungumza mara baada ya mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Pee Pee Tanzania Limited (PPTL) Bw. Jonathan Lane alisema kuwa kiwanda chao chenye wafanyakazi wapatao 1,000 wengi wao wakiwa akina mama, kimekuwa kikikabiliwa na wataalamu waendesha mitambo 'Mafundi mchundo' kutokana na kukosekana hapa nchini.

Alisema vijana wengi wanaomaliza elimu ya juu ikiwemo vyuo vikuu wanapofika kufanya usaili katika kiwanda hicho, kwanza wamekuwa na mapungufu makubwa ya lugha ya mawasiliano ikiwemo udhoefu wa kuendesha mitambo ya kiwanda hicho hivyo kushindwa kuwachukua.

"Hapa kiwanda tunakosa wataalamu kutoka hapa Tanzania, tunapowaita vijana wanaomaliza vyuo vikuu kwenye Interview (usaili) wanakuwa lugha tu inakuwa shida na jingine hawawezi kuendesha mashine hizi tunazotumia inakuwa shida kuwaajiri tuna lazimika kuchukua wataalamu kutoka nje kama Kenya," alisema Bw. Lane.

Akichangia suala hilo Meneja wa kiwanda hicho Bw. Dominick Mtemangwa alisema suala kubwa linalosababisha wahitimu wengi wa vyuo vikuu kushindwa kuwa na utaalamu wa kuendesha mashine ni kutoka na kusoma kwa nadharia tofauti na miaka yao ambayo kabla ya kwenda chuo kikuu walikuwa wakipitia katika vyuo vya FTC ambako huko hukutana na mashine mbalimbali zinazowapa urahisi wa kufanya vizuri kwenye mitihani na kivitendo

Halkadhalika Mkuu wa mkoa huyo, alipofika kutembelea kiwanda cha Arthi-River Meneja mradi wa kiwanda hicho Bw. Rajesh Vyas alisema wanatangaza nafasi za vijana wa mkoani Tanga wenye ujuzi wa kazi mablimbali katika kiwanda chao, lakini hakuna anayejitokeza na wakijitokeza wanakuwa hawana ujuzi hivyo kupata wakati mkumu wa kukamilika mapema kiwanda hicho kama walivyoaahidi.

Alisema pamoja na suala hilo tayari wamewafundiusha vijana wapatao 30 kwa fani mbalimbali katika kiwanda hicho ambacho ujenzi wake unakwenda sambasamba na kiwanda chao kingine kilichopo wilayani Mkuranga, Pwani kitakachokuwa na ukubwa sawa na cha tanga.

Akizungumza suala hilo, Mkuu wa mkoa alisema kuwa kwa mpango wa haraka atakutana na Mkuu wa chuo cha VETA mkoani hapa, kuangalia kwa haraka fani ambazo zinatolewa hapo ili kuwawezesha vijana watakaochukua mafunzo hapo waweze kupata ajira katika viwanda hivyo.

Pamoja na kueleza hayo pia, aliwapongeza viongozi wa viwanda vyote viwili kwa kutambua suala uhifadhi wa mazingira katika viwanda vyao kutokana na kemikali wanazotumia na hasa suala la uchimbaji wa mawe na hivyo mashimo yaweza kubaki yakaleta athari za kimazingira lakini kiwanda cha Arthi-River mara baada ya kuchimba mawe hayo wamekuwa wakiyatunza mashimo mengine kwa ajili ya kuhifadhi maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. kwani lugha ndio inafanya ufundi mchundo? wawaajiri vijana wawape OJT!!!chuo kikuu wameambiwa wanafundisha kuendesha mitambo???wasitafute sababu!!!

    ReplyDelete
  2. so wewe mzungu kuchukua vijana waliotoka chuo kikuu ndo waweze kuendesha mitambo yako? acha analysis weak na finyu kama jina la kiwanda chako. so wanafunzi wa vyuo vikuu waje kuoperate machines? na hao kina mama unaosema ndo wengi wao ni graduates pia? crap crap kabisa!

    ReplyDelete
  3. Huyo mwekezaji kakosa la kusema, FTC mwenyewe hafundishwi kuendesha mashine ila kuzifanyia maintanence, na mambo mengine ya kuifundi, sembuse mwenye degree?? huu si wehu huu?? labda awachukue veta huko awafundishe kuendesha hizo mashine kwasababu hata akiletwa nani yule bila kuelekezwa hizo mashine anaweza asione hata pakuwashia)) Na sio kila anayesoma magari basi automatic anaweza kuwa dereva bila kujifunza kuendesha))
    This is none sense

    Kaniharibia siku yangu huyu.

    ReplyDelete
  4. fundi mchundo ni nani? na ukienda chuo kikuu kwa nia ya kutaka kuwa fundi mchudo unatakiwa kuchukuwa shahada gani?

    Kiwanda kipo tanzania, itakuwaje mwanafunzi wa kitanzania ashindwe interview ya mawasiliano? wnashindwa interview kwa sababu interview zinaendeshwa kwa kimombo badala ya kiswahili ambayo ndio lugha ya taifa. Ile sheria ya kuwa mgeni hawezi kufanya kazi tanzania hadi awe anaweza kusema kiswahili imekufa?

    ReplyDelete
  5. hang on! yaani mdogo wangu aliemaliza chuo kikuu na kupata shahada yake hawezi kupata kazi ya kiwandani? Hivi tunadanganywa kiasi gani na hawa watu weupe mpaka wanafika kudharau shahda za vyuo vyetu nchini?

    Mtu umemaliza chuo halafu ukafanye kazi ya kuendesha mashine kiwandani? Hivi kweli hili jamani? sidharau wanaofanya kazi za mashine viwandani, lakini kweli mtu anahitaji kuwa na shahada ya chuo kikuu kufanya kazi za namna hii?

    ReplyDelete
  6. Huo ndiyo ukweli, tunaonekana wabishi wakati huo ni ukweli mtupu! Hao graduates wameajiriwa katika nafasi hizo kutokana na qualification zao za chuo. Na mwekezaji anaona ufanisi na vyeti ni tofauti! Mnasahau kuwa degree zetu ni za madesa na c*p? Engineering gani inafanywa theory tu bila vitendo?

    ReplyDelete
  7. Hawa jamaa wametuzalilisha sisi Wa Tz na wamezalilisha Vyuo na Shule zetu kwa kauli zao!wasomi na mnaosomewa mpo!

    ReplyDelete
  8. Huyu jamaa ni mkoloni.wwaazalendo hao wanahitaji mafunzo tamthilia ya mitambo hiyo kwani wao hawajaietengeza.Hao wakenya wana vibali vya kufanya kazi bongo??????? natoa hoja!!!!!!!!!!!!!
    wizara husika kifuatilieni hiki kiwanda au kifungwe kwa kukashifu waTZ.

    ReplyDelete
  9. NA VIJANA WENYEWE NI KAMA HAO WALIOTOA MAONI HAPO JUU. Watu hawataki kukubali elimu ya Bongo ya kukariri kupasi mtihani haiwasaidii kwenye soko la ajira. Badala ya kuloby system ya elimu ikabadilishwa mnawapigia kelele wanaowastua. Kingine vijana wa KiTZ ni high maintenance, ukitaka afanye kazi kwa ufanisi basi lazima umwekee mnyapara mgongoni otherwise atakuwa yuko busy na mambo yake perfomance ziro. Maneno meengi ndio kazi yao!!

    ReplyDelete
  10. mbona kwao ulaya,tunaoperate mashine zao za boksi bila kuwa na shule???


    Neema.

    ReplyDelete
  11. huyu jamaa hana maana kabisa ,kuna KITU KINITWA ON JOB TRAINING ambazo kila mwajiriwa mpya lazima apate kwenye kipindi cha mwanzo wakati wa kuajiriwa ,na pia waruhusu wanafunzi wafanye FIELD TRAINING hapo kama wanataka kuwaajiri baadae,sehem nyingine kama BARRICK GOLD etc wanafanya hivyo kwa wanaosoma mining engineering,kwanini wao hawafanyi??.....aache kudanganya watu

    ReplyDelete
  12. Anonyumous wa 07:43:00 unasupport kitu usichokielewa, kwanza hakuna Engineering isiyo ya vitendo, pia kama umemwelewa huyo mwekezaji nadhani ungekuwa upande wetu. Anadai kwamba wamekuwa hawawezi kuendesha mashine zake, sasa huko Vyuoni nani kakwambia wanafundisha kuoperate hizo mashine? na ikiwa hivyo utasoma mashine ngapi duniani?
    Na swala la lugha, ni mtanzania gani asiyejua kiswahili??

    ReplyDelete
  13. Mimi nadhani mafundi mchundo kazi yao si kuendesha mashine ila kuirekebisha ikiwa na matatizo au hitilafu ndogo,maana hitilafu zikiwa kubwa ni lazima awepo mtaalam maalum wa mashine hizo.
    Kuendesha mashine huitaji elimu kubwa ni job training tu, unafundishwa jinsi ya kuiendesha na hatari zake na jinsi ya kuizima ikitokea hitilafu.
    Elimu na lugha inakusaidia ktk kusoma maelekezo ya mashine na kuwa na upeo mkubwa wa kuamua na kutafakari kwa wepesi zaidi.
    Ni maoni yangu tu!

    ReplyDelete
  14. madhara ya kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia ndiyo yameanza kuonekana sasa. vijana wetu hawajiamini wanapotokea katika interviews zinazoendeshwa kwa kiingereza. serikali inapaswa kutambua hilo na kulinda soko la ajira kwa ajili ya vijana wetu. wawekezaji walazimishwe kuajiri wasomi wetu na kuwapa ON THE JOB TRAINING. Mhitimu wa Mech Eng hawezi kujifunza kuoperate machine za kila kiwanda unachokijua wewe. Pia wawekezaji waanzishe ushirikiano na vyuo vyetu vya ufundi na vya elimu ya juu.

    ReplyDelete
  15. Hapo kuna mgongano wa lugha, mgongano wa habari pia. Kwanza kuna habari ya kiwanga cha cement, pia kuna habari ya kiwanda cha kutengeneza vifungashio.
    Pia kuna mgongano wa lugha kati ya fundi mchundo na mwendesha mashine. Fundi ni technician ambaye ni msaidizi wa injinia. Mafundi wa aina hiyo wapo wengi sana wana FTC zao upande wa mechanics. Machine operators sio lazima awe fundi anaweza akawa mtu yeyote mwenye akili timamu na uelewa mzuri aliyemaliza angalau kidato cha nne mwenye ufahamu wa lugha angalau moja ya kigeni mfano english. Mwendesha mitambo hufundishwa kwa kuambkizwa ujuzi ili ajue namna ya kuzalisha kwa ubora,na kujua mazingira yake ikiwamo usalama kazini na ufahamu wa namna ya kutatua matatizo madogo madogo baaasi, hamna mbwembwe zaidi ila ni jukumu la mwajiri kumpatia mafunzo ya mara kwa mara kuhusu kuzingatia ubora,kuna na enviromnental management nzuri ikiwa ni kuangalia gharama,usafi wa mazingira,usalama kazini n.k.Huyo mpuuzi anataka kumzunguka waziri ili akubaliane nae waongeze idadi ya wageni wanaokuja mara kwa mara kwenye kiwanda hicho.
    Hapa hawa jamaa ndipo wanapowazunguka viongozi wetu wavivu wa kufikiri na kujikuta wakipuuzia kanuni nzuri za uwekezaji ambazo tayari zipo, na lengo la hawa mabwana ni kutorosha pesa ,capital flight ili kuinyima nchi mapato ya kodi. Hii michezo wanafanya sana hapa kwetu na suala la kusema hakuna wataalamu wa kuendesha mashine ni upuuzi, mashine zote watu hufundishwa kwenye commisioning hadi wanapojua nao hufundisha wenzao huo ni utaratibu dunia nzima

    ReplyDelete
  16. Mdau wa Wed Feb 08, 02:16:00 AM 2012 ni kweli unayosema pia nakubaliana na wengine anaopingana na huyu jamaa ati hatuwezi kuendesha mitambo huo ni upuuzi,mama Chiku wamekuongopea tu hao jingas.Hivi hulengesha mfuko wa cement kwenye parker machine ambapo kg zikifika 50 parker inafunga automatically inahitaji degree? Nyie wazee wa kuponda mnajua mnachosema au mnabwabwaja tu? Mitambo mingi sasa hivi ni full automated mbaya zaidi sisi ni tunafanya applications tu za hizo imported technology kazi ya engineers kwenye processing ni ndogo sana na ndio maana process engineers hawapati sab=na ajira viwandani sababu hiyo.Kusimamia mtambo wa kujaza soda au bia kwenye chupa ambao upo automatic kuam=nzia kuzafisha chupa, kujaza kuweka vizibo,kuweka kwenye kreti ni full auto kazi ya binadamu ni kuangalia tu kama series haiendi vizuri anaambiwa zima reset anza tena fork lift operator anasubili kreti zikijaa apange pallets inahitaji degree nyie wazee wa kuponda? Ni sehemu ya quality,schedule maintainace and repair na supervison, budgeting,planning etc ndipo unaweza hitaji skilled labor. Acheti kukurupuka nyie wapondaji
    Pia samahani kwa kuchanganya lugha

    ReplyDelete
  17. Inawezekana kwamba maneno yaliyotumika hapa yametoa sura mbaya ya wafanyakazi wa kitanzania lakini naamini kwa kiasi fulani yana ukweli ndani yake.

    Suala la kuwa na kiwanda nje ya Dar es Salaam ni moja ya sababu inayochangia kukosekana kwa mafundi/wafanyakazi wazuri. Halmashauri zimesema zimekosa kupata 'data clerks' kusimamia data base za HIV services kwakua watu wenye skills za computer hawapo katika maeneo yao. Kuna mambo mengi yamejificha katika haya malalamiko.

    ReplyDelete
  18. Tutazidi kubishana but we have to accept once he is an investor and not a non for profit organization he wants the money he has invested back....Graduates wetu ni bogus have said it na we all know it.mtu anakuja interview hajui kujieleza atawezaje kusoma hata manuscript za kuoperate machine!!!its time we accept our education has our weakness and we do something about it.
    Mdau Nairobi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...