Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (wapili kushoto) wakimshukuru Mtembi Majebele baada ya kupewa heshimi ya Kuwa Mtemi Masanja na mkewe kuwa Ngole katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Maswa Februari 20, 2012. Walikuwa kwenye ziara ya mkoa wa Shinyanga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakicheza ngoma ya Watemi wa Kisukuma baada kupewa heshima ya kuwa Mtemi Masanja na Mkewe kuwa Ngole kwenye uwanja wa michezo wa Maswa wakiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 20, 2012. Kulia kwake ni Mtemi Majebele ambaye ndiye alimpa heshima hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakicheza ngoma ya Watemi wa Kisukuma baada kupewa heshima ya kuwa Mtemi Masanja na Mkewe kuwa Ngole kwenye uwanja wa michezo wa Maswa wakiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 20, 2012. Kushoto ni Mtemi Majebele ambaye ndiye alimpa heshima hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua tawi la Benki ya CRDB la Bariadi akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 21, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua tawi la Benki ya CRDB nla Bariadi baada ya kulifungua Februari 21, 2012.. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea mfano wa hundi ya sh. 5,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB, Tuli Mwambapa baada ya kufungua tawi la Benki hiyo la Bariadi Februari 21, 2012. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Waiziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kaka, Huyo Tuli huyo mi huwa namzimiaga sana huyo. Una kontaks zake unipatie jamani?

    ReplyDelete
  2. 100% confidence levelFebruary 22, 2012

    Wadau hivi hii ni tabia au ni mashinikizo kutoka kwa wahusika??
    Kwa mfululizo mara tatu sasa ndani ya mwezi huu tunashuhudia watendaji wakuu kabisa wa serikali wakivikwa uchifu na makabila mbalimbali wanayotembelea kwa ziara za kiserikali.
    Ndivyo itifaki ya uongozi ilivyo au wananchi wasimikaji wameishiwa sera kwa hiyo kila wanalolifikiria wanalitekeleza????au ni indirect approach ya kuwakaba wakuu hawa kutimiza ahadi zao za maendeleo maeneo husika???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...