Rais wa Baraza Kuu la Usalama kwa mwezi wa Machi, Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa, Bw. Mark Lyall Grant akifafanua jambo mara baada ya kukamilika kwa mkutano wa Baraza hilo ambalo pamoja na kulaani mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, pia lilielezea hali tete ya kukidhiri kwa ukame, uhaba mkubwa wa chakula, kuongezeka kwa makundi yenye silaha, ugaidi na kusambaa kwa silaha katika eneo la kanda ya Sahel hali inayotishia siyo tu usalama wa eneo hilo, bali imesababisha pia mamia ya wananchi kukimbilia nchi jirani kutafuta misaada ya kibinadamu. Katika kikao hicho, Baraza hilo limezitaka jumuia ya kimataifa yakiwamo mashirika ya kimataifa kuharakisha misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.
Wajumbe wa Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa walipokutana siku ya jumatatu kujadili hali ya Usalama katika Kanda ya Afrika ya Sahel ambapo pia walijadili mapinduzi ya kijeshi nchini Mali na kutoka na taarifa iliyolaani mapinduzi hayo na kuwataka wanajeshi kurejea makambini na kurejesha utaratibu wa katiba pamoja na kufanyika kwa uchaguzi kama ilivyopangwa.

Na Mwandishi Maalum - New York

Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, limelaani vikali mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na askari wa chache dhidi ya serikali ya kidemokrasia nchini Mali. Na limewataka wanajeshi hao kuachana na vitendo vya kihalifu na fujo na kurejea katika makambi yao

Taarifa iliyotolewa na Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Marchi Balozi wa Uingereza Bw. Mark Lyall Grant amesema. “ Baraza la Usalama linalaani mapinduzi hayo na linawataka wanajeshi kurudi katika makambi yao na linatoa wito wa kurejeshwa kwa utaratibu wa Katiba na kufanyika kwa uchaguzi kama ilivyokuwa imepangwa.

Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana siku ya jumatatu ambapo lilijadili kuhusu kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika Kanda ya Afrika ya Sahel, ambapo lilisema kwamba kuongezeka kwa makundi yenye silaha na magaidi pamoja na kuzagaa kwa silaha kumeongeza hali ya wasiwasi katika kanda hiyo.

Wiki iliyopita baadhi ya wanajeshi wa nchi Mali wakiongozwa Kapteni Amadou Haya Sanogo walitangaza kuipindua serikali ya Rais Amadou Toumani Toure ambaye mpaka sasa hajulikano aliko.

Katika mkutano huo ambao uliwahusisha wajumbe 15 wanaounda Baraza Kuu la Usalama, Baraza hilo pia limelaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya makundi ya waasi ya kuvivamia vikosi vya serikali na kuwataka waasi hao kusitisha aina zote za vurugu na kutafuta ufumbuzi wa amani kwa njia ya mazungumzo ya kisiasa.

Aidha Baraza hilo limesisitiza haja ya kuzingatia na kuheshimu uhuru, umoja na mipaka ya nchi.

Tayari Umoja wa Afrika ( AU) umekwisha kutanga kutoyatambua mapinduzi hayo, huku baadhi ya nchi ikiwamo Marekani ikitangaza kusudio la kusitisha misaada kw anchi hiyo , nchi ambayo uchumi wake kwa asilimia kubwa unategemea sana misaada kutoka nchi wahisani

Kuhusu hali tete ya kanda ya Sahel, Baraza limebainisha kuwa hali ya ukame , uhaba wa chakula na kurudi kwa maelfu ya watu kutoka Libya kumeongeza hali ugumu wa maisha kwa watu wa eneo hilo. Hali ambayo imesababisha maelfu ya wananchi wa eneo hilo kukimbilia katika nchi za jirani kutafuta hali bora ya maisha.

Kutokana na hali hiyo, Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, limetoa wito kwa mamlaka za kitaifa na kimataifa, kikanda na masharika ya misaada ya kibinadamu kuchukua hatua za haraka kuimarisha juhudi za kuwasaidia wananchi wa eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hawa UN wa ajabu wana authorize mapinduzi ktk nchi mbalimbali lakini leo wanapiga vita mapinduzi ambayo hawakuhusishwa. As long as they have their interest met it's okey but....

    ReplyDelete
  2. BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA ni wanafiki na wapo kwaajili ya masilahi ya nchi zao chache, tofauti na interest zao watakulaani.

    Serikali ya Libya imeondolewa madarakani na waasi, tena hao waasi wakifadhiliwa vifaa vya kivita na nchi zao, kisa Gadafi anazuia maslahi ya nchi zao Libya. Hali ni hiyo kwa nchi nyingi tu za africa na mashariki ya kati zilizo ondolewa madarakani kwa viongozi wao.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  3. Hawa jamaa UN SECURITY COUNCIL wa ajabu kweli kweli mbona Mapinduzi ya nchi za Kiarabu na nchi zingine Duniani hawakuyalaani leo wanalaani ya Mali?

    -Tunisia?
    -Misri?
    -Libya?
    -Yemen?

    -Zimbabwe(yamekataa)?
    -Liberia?
    -Suerra Leone?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...