Michuzi Media Group Ikishikiriana na Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya bure ya kutembelea tovuti ya Michuzi Blog. Kwa kupitia mitambo yao ya “Wifi Mesh” iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa na tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa za punde bila gharama yoyote.

Akikaririwa katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema hivi, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo Watanzania wanachukua hatua katika kuleta taarifa mbalimbali kwa wananchi katika viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba  Michuzi Blog itakua huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”.
Akiwa ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone imejikita katika kutoa huduma kwa jamii na tumegundua kwamba taarifa za kijamii zinatakiwa kuwafikia wanajamii kwa urahisi. Tovuti nyingi zinatembelewa na Watanzania waliopo nchi za nje kuliko wananchi waliopo nchini na hii siyo haki. Kama nina uwezo kupata taarifa kwenye tovuti ya Michuzi ni jukumu letu kama kampuni kuwawezesha watanzania waliopo nchini pia kupata huduma. Watanzania tunatakiwa kuwa na utamaduni wa kusaidiana na kupeana moyo na hii itasaidia kukuza uchumi wetu sio tu kununua na kuuza bidhaa kutoka nje.

Kwa pamoja Bwana Michuzi na Katunda wamesema huu ni mwanzo tu na wanaamini kwamba hili wazo litafuatwa na wengine. Kwa msisitizo Bwana Michuzi aliongea “Lazima tuonyeshe mfano kwa vitendo sio maneno tu. Tumechukua hatua ya kwanza katika kufanikisha ndoto, wengine wanatakiwa kujiunga kwenye mapinduzi haya na kufanikisha”
Kutembelea tovuti ya Michuzi bila gharama washa Wifi kwenye Ipad, Tablet, Simu au Laptop. Tafuta MichuziBlog Wifi, Unganisha ,fungua browser yako uipendayo mfano Chrome, Internet Explorer, Safari au Firefox na nenda kwa Issa Michuzi.blogspot.com.
Kama hautapata  MichuziBlogWifi, tafadhali wasiliana na Uhuruone kwa email ifuatayo, issa.michuzi@uhuruone.com au piga simu namba 255779477477 ili uweze kuunganishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ankal,
    Hizi ni habari njema kwa wamiliki wa simu, ila kwa wenye vimeo mh! naona mazonge mie. Nikinunua simu na hii mitaa yetu ya mburahati barafu, Kigogo, manzese, tandale, Tandika si wataiba?

    ReplyDelete
  2. Congratulations, this is great. I hope others will follow your example and provide hot spots in hotels, bars, restaurants etc. You are always a pioneer.

    ReplyDelete
  3. Nakubali kaka, na kila la kheri.

    ReplyDelete
  4. mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe.kazi nzuri sana ya kizalendo unkali.sio ufisadi wa wachache kwa maslai binafsi.kuna msemo "ukila na kipofu usimshike mkono" big up michuzi.
    mdau washington

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi,
    Hongera sana kwa kufanikisha jambo hili. Ni matumaini yetu kutakuwa na mwendelezo mzuri kutufikia hata wa nje ya Dar.
    Kazi Njema.
    Maggid Mjengwa.

    ReplyDelete
  6. Ankal inabidi kwa Mapinduzi haya juu ya Msaada huu walau wewe na hao Uhuru One tuache unafiki angalau mfikiriwe kupewa 'Ubalozi wa Hiari'

    ReplyDelete
  7. Kila kuendako hisani hakurudi nuksani bali shukrani.Asante sana ankali wetu wa ukweli Issa bin Michuzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...