Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige amemteua Dr. Casta Tungaraza (pichani) kuwa Balozi wa  Hiyari wa Utalii katika Nchi ya Australia kuanzia tarehe 23.3.2012.

Akiwaandikia viongozi wa Jumuia  ya Watanzania (Western Australia), Balozi wa Tanzania nchini Japani anayesimamia pia Australia, Mhe. Salome T. Sijaona alionyesha furaha yake na kumtakia balozi huyu mpya mafanikio katika kuitangaza Tanzania katika nyanja za utalii.

Dr Tungaraza hivi majuzi tu aliingizwa katika Hall of Fame ya wanawake huko Australia na pia kupewa Nishani ya Uwanaharakati katika Jamii huko huko Australia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Woow! congratulations Dada Casta!

    ReplyDelete
  2. Hongera balozi wetu Dr Casta..mwenyenzi mungu akupe nguvu zaidi uendelee kujenga taifa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...