Ankal asante kwa blogu yetu ya jamii.
Mimi niulize swali la msingi kwa serikali na wadau wa mabadiliko ya katiba ndani ya nchi yetu.

Kwa kuzingatia Ibara ya 21-(1)cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho toka 1977 hadi tarehe 30,Aprili 2000,kinachohusu Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4, Nanukuu,"21.-(1)  Bila  ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya  Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia  utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria" kifungu cha (2) kinaendelea kusomeka kuwa,nanukuu," (2)  Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa".

Swali: Je Serikali imeandaa utaratibu upi wa kuwashirikisha (Wabeba Boxi)  watanzania wanaoishi nje ya nchi kwa shughuli maalumu za kiserikali au binafsi na pengine kuwa na uraia wa kudumu?  wadau wa maendeleo ya Taifa wana mtizamo gani juu ya hili au nini ushauri wao kwa serikali yetu?
Naomba kuwasilisha.
Mdau 
Joachim K. Global.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hwana kitu wanajua zaidi ya kusema "huku ulaya wazungu wanafanya hivi. Mimi naona TZ tufanye hivi"

    Wengi wa wabeba mabox halisi ni wavivu wa kufikiri. Wachaguliwe wale wasiobeba mabox kutoka ulaya

    ReplyDelete
  2. Wapiga box sasa kilichobaki kwenu ni kuzidi kuwapigia box hao wazungu na kwa wale waliokuwa hawajapata makaratasi wasubiri hayo makaratasi ili waweze kuja kuchukua vimada vyao huko ughaibuni.

    ReplyDelete
  3. Haki ya DUAL CITIZENSHIP hamjapata. mnataka na katiba tena. Nawashauri mrudi home. muongeze wingi tupige kura wengi

    ReplyDelete
  4. Mtoto wa CoastMarch 01, 2012

    Katika uteuzi wa Kamati ya kukusanya maoni; Rais asisahau wawakilishi (Watz)angalau wanne walioko nje (Africa & Middle East; US, Canada & Americas; West & East Europe, Asia & Oceanic)kwa zingatio la kigezo cha jiografia kushiriki kukusanya maoni. TEHAMA itasaidia kiurahisi kupata maoni ya Watz walioko ughaibuni kupitia mtandao na baadaye watayaunganisha kwenye Tume kamili itakayokuwa imeteuliwa.

    Mtu awaye yeyote asighubukwe na unyanyepaa wala kiburi cha kuwadharau Watz wawe wanaishi nchini au nje.

    ReplyDelete
  5. Umesema wenye uraia wa kudumu, ina maana kuwa kuwa bado hatujawa na dual citizen mlipata uraia wa huko mlipo na kuukana uraia wa Tanzania. Sasa kwa wale raia wa kigeni wenye asili ya Tanzania ni hivi haturuhusu wageni kushiriki kwenye shughuli za siasa ikiwemo mchakato wa katiba. Huko mliko si mnaruhusiwa kupiga kura na hata kugombea uongozi? Sasa huku mwataka nini tena na nyie mna maganda ya red sijui bluu, sijui meusi. Aah msituchose kila siku huwaga mnasubiri chakula kitengwe mezani muanze kudai share yenu. Njia rahisi ya kushiriki mchakato wa katiba pangeni mje huku likizo wakati wa mchakato, simple mtashiriki bila kuulizwa vitambulisho. Huku mnataka na kule mwataka mwisho mtakosa kote.

    ReplyDelete
  6. We anony wa tarehe 1 march saa 3:42 utakuwa na lako jambo. Watu wa dizaini kama yako ndio huwa wa kwanza kututumia sms na kutupigia simu usiku wa manane kutulilia shida alafu leo unaongea utumbo.Ndio maana tukija holiday tunawaibia mageliflendi wenu.

    ReplyDelete
  7. Heroo!!! wabeba boxi, embu acheni mara moja hiyo tabia yenu ya mkienda bongo kumega wake za watu. ona sasa yenyewe yanavyowachukieni.

    ReplyDelete
  8. La Muhimu kabla ya kutafuta Kushirikishwa ktk Mchakato wa KATIBA, Wabeba Ma BOX ni kuhakikishiwa mambo matatu:

    1.Kuharakishiwa suala la DUAL CITIZENSHIP.

    2.Kuimarishiwa Mpango wa DIASPORA.

    3.Kupewa Uamsho wa Kujiamini kutokana na uvivu wenu wa Kufikiri na Kuridhika na Maisha ya kuendelea kubeba hayo Ma box Kujifedhehesha wenyewe huko na Kututweza sisi Watanzania,,,Angalieni Huko huko UK mnaweza Kujifunza kutoka kwa walichokifanya WAZEE WA KAZI SERENGETI FREIGHT FORWARDERS na Wadau wa UWANJA WA NYUMBANI.

    ReplyDelete
  9. Angalia sasa,

    Unadai Katiba wakati unaota sugu mgongoni kwa kubeba BOX !

    tua chini BOX jikwamue kwanza ndio udai Katiba au siyo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...