MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ndugu Wananchi,
Naomba sote tumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma kwa kutuwezesha kuzungumza tena mwisho wa mwezi huu. Katika mwezi tunaoumaliza leo taifa letu lilipata msukosuko mkubwa kufuatia mgomo wa madaktari. Nashukuru mgomo huo umeisha lakini makovu yake yatabaki maisha katika kumbukumbu za historia ya taaluma ya tiba hapa nchini.
Leo, Mheshimiwa Waziri Mkuu amenipa taarifa kuwa Kamati aliyounda kushughulikia madai ya madaktari imekamilisha kazi yake na kuwasilisha taarifa yake kwake. Kuanzia kesho Serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na uwezo uliopo. Nawaomba ndugu zetu madakatari kuwa na moyo wa subira.



Hii imetulia sana. Nchi yetu inakwenda pazuri. Busara na hekima vilivyotumika kuzima munkari wa wananchi haswa vijana ni za kupongezwakwa nguvu zote. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa!!
ReplyDeletewhy 15 bara and 15 z'bar?mi naona hapana uwiano hapo, kutokana na kuwa asilimia kubwa ya population ipo bara basi namba ya bara ingekuwa kubwa au ndo kuuenzi muungano? usawa ni lazima
ReplyDelete