Kaimu balozi wa India nchini Tanzania Bi. Hemalatha Burgimath mmoja (kulia) akimkabidhi nyaraka za kusafiria Bi. Neema Msita mmoja wa maafisa michezo 5 wanaokwenda nchini India kujifunza program mbalimbali za Michezo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya ubalozi wa India jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yasoda (katikati).
Kaimu balozi wa India nchini Tanzania Bi. Hemalatha Burgimath akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Michezo na maafisa michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo mara baada ya hafla fupi ya kuwakabidhi nyaraka za kusafiria kwenda nchini India maafisa Michezo 5 kutoka mikoa mbalimbali.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.


Program ya michezo.. India? You must be kidding.. Ndiyo maana hatuendelei kimichezo badala yake tunarudi nyuma.
ReplyDeleteNi vigezo gani vilivyotumika kuwachangua hao maofisa michezo wanaokwenda India?
ReplyDeletemkurugenzi msaidizi huo moba hujamaliza kuulipia?
ReplyDeletena wewe anony Mon Mar 05, 11:43:00 AM 2012 umeambiwa ni program ya michezo na sio program ya mchezo. kwani hujuwi kama india ni nyumbani kwa cricket?
Ni Vigezo gani vilivyotumika ameuliza mdau hapo juu.Na mimi namkingia kifua.Tunaomba majibu haraka
ReplyDeleteDavid V
wakajifunze criket na oak..hiyo mingine haina nafasi India
ReplyDeleteNi mara nyingi nafasi za Namna hii kwa Vile ni Mipango ya Masomo ya nje hugawiwa kwa Wasiostahiki!
ReplyDeleteMichuzi hii kali,nafahamu michezo michache ambayo India imepiga hatua na tunaweza kujifunza,issue ni hawa maafisa waliopelekwa wameenda kujifunza ili waje kufundisha akina nani?maana kazi yao ni kukaa kwenye dawati na nina uhakika wengi wao hata rede hawajacheza,kama mdau uliweza kuitwa ili kutoa habari hii basi naomba wakisharudi miezi miwili baadae wakuite ili tuone wanafundisha nini na wapi aina gani ya mchezo kwa ajili ya wazalendo,maana na uhakika wengi wa hawa hawana chochote wanachokifahamu kwenye michezo na wamekwenda huko kutia aibu maana hata jogging kwao issue.....mdau wakirudi watueleze au huko huko India walete picha zao au video wanavyoshiriki mafunzo hayo ya nadharia na vitendo
ReplyDelete