Asalaam Aleyikum Ankal Issa Michuzi.
Ninaitwa Wilbald. Ankal nina jambo ambalo naomba unisaidie kuliweka katika blog yako ili Watanzania wenzangu waelewe. Mnamo tarehe 25/01/2012 Indian High Commission Office ilitoa tangazo la Indian scholarships katika fani mbalimbali kwa Watanzania katika gazeti la Kiingereza la Daily News kwa vyuo mbalimbali vya India.
Tarehe ya mwisho wa kutuma maombi kwa mujibu wa hilo tangazo ilikua ni tarehe 20/02/2012, candidates walishauriwa kupiga simu Indian high Commission kati ya tarehe 07 na 08 March kuulizia status ya maombi yao. Kwenye tangazo zilitolewa namba za simu kwa ajili ya waombaji kupiga simu kwa tarehe tajwa kuulizia majibu ya maombi yao.
Nilituma maombi yangu tarehe kabla ya tarehe ya mwisho ya kutuma maombi. Ilipofika tarehe 07/03/2012, siku ambayo kwa mujibu wa tangazo waombaji walitakiwa kufuatilia majibu ya maombi yao, nilipiga simu ubalozi wa India kuulizia majibu ya maombi yangu.
Mtu niliyezungumza nae (Jina namuhifadhi)aliniambia kwamba majina ya waliochaguliwa yapo getini pale ofisi za ubalozi wa India hivyo kama ninaweza niende kuangalia. Nikaenda kuangalia, kweli nilipofika pale ubalozi wa India, nilikuta list ya majina kama 59 kwa mlinzi wa getini. Kwa bahati nzuri jina langu lilikuwepo katika waombaji waliochaguliwa.
Mlinzi akanielekeza niende kumwona ofisa anayeshughulika na mambo ya elimu (Jina namuhifadhi kwa sasa) kwa maelekezo zaidi. Nilipofika mapokezi nilizungumza na ofisa elimu wa Indian High Commission kwa simu na kunipa maelezo kwamba nirudi saa nane mchana kwa vile mda huo alikua na kazi ya kukusanya fomu za waombaji ambao tayari wameshazirejesha. hivyo akaniambia nije kuchukua fomu yangu saa nane mchana.
Kama nilivyoelekezwa nilirudi saa nane mchana. Mlinzi akampigia tena simu yule ofisa wa elimu kumjulisha kwamba nimerudi. Mlinzi akanipatia simu nizungumze na yule ofisa wa elimu. Yule Ofisa wa Elimu akanieleza kwamba samahani sana watu waliorejesha fomu wameshatosha hakuna tena nafasi.
Nilifadhaika sana. Kuna waombaji wengine walifika mda huo wa mchana kuja kuangalia majina, kwani walipopiga simu waliambiwa majina yapo getini. Cha ajabu mda ule walipofika ile list ya waombaji waliochaguliwa ilikua imekwishaondolewa pale kwa mlinzi. Na kila aliyeulizia aliambiwa tu hajachaguliwa kwani waombaji waliochaguliwa wameshapigiwa simu. Walipouliza kuhusu list waliambiwa listi imechukuliwa na Mheshimiwa Balozi.
Sasa najiuliza kama waombaji tayari wameshapigiwa simu, walipigiwa lini? kwani tangazo lilisema waombaji wapige simu kati ya tarehe 07 na 08 March 2012. Zaidi ya hapo nilimtumia barua pepe huyu ofisa wa elimu tarehe 06/032012 kuulizia majibu ya maombi yangu lakini sikujibiwa.
Hiyo ndio hali halisi Ankal Michuzi, nimeshakata tamaa na ninaomba uma wa Watanzania ujulishwe namna hizi scholarships zinavyoendeshwa. Niliomba kufanya appointment na Balozi nimweleze yaliyojiri, sikupewa nafasi na wala sikujibiwa lolote la maana.
Nakutakia kazi njema Ankal Issa Michuzi
EEEhh Pole sana kaka yangu,,Yaani ina maana hao waliokuja baadae kuangalia katika ile list na wenyewe walijibiwa kama wewe?kama ni hivyo basi hakuna aliyepigia simu hivyo wanakusugeni tu,,labda hiyo scholarship waliicancel,sasa kuwambia ukweli walishindwa,,itakuwaje nyie wote mliokuwa katika list msichaguliwe,na wakati mliambiwa kama umechaguliwa uko katika list hapo getini,,Yaani mambo kama haya yanakuzidisha mtu mawazo,,bora wasingetangaza kitu kama hicho na bora usingejikuta katika list,,ukawa unadeal na mambo yako mengine,,Nimekuonea huruma sana,,hao wahindi hawajatulia,,na niliona hapa katika Michuzi eti wanazidi kuekeza nchini Tanzania,,wakati Railway iliwashinda..
ReplyDeleteNakutakia kila la Kheri,,jaribu Scholarships zingine,,Mbona niliona Dada mmoja anatangaza humu katika blog kuwa kuna offer ya wanafunzi wa kitanzania hapa UK inaanza mwezi wa Nne kwa nini usjaribu hiyo?
Ahlam,,UK
Kama hakuna ubabaishaji, itakuwa vizuri kutangaza majina ya waliochaguliwa ikiwezekana kwenye gazeti lilelile mana hata mimi ninawasiwasi nao kutokana na uzoefu wa mwaka jana. Kama hawana nafasi au wanawatuwao tayari wasipotezee wengine muda!
ReplyDeleteduh pole sana. hapo kuna wajanja wameshachakachua hizo nafasi kwa kuweka ndugu zao au watoto wa maswahiba zao.
ReplyDeletepole sana usikate tamaa ndugu jaribu kwengine.
Mdau wa Masomo ya Scholarhsip pole sana na matatizo ambayo ni Kansa na Ukoma wa Maisha kwa Jamii yetu ya TANZANIA!.
ReplyDeleteUpendeleo na Rushwa umeota mizizi nchini!,,,hivi kweli tutafika?
Kama hakukuwa na umuhimu wa hawa Watahiniwa ni kwa nini majina yawekwe Getini kwa Mlinzi?
Na kama wapo waliochaguliwa kwa nini majina yao yasianikwe na vigezo vya stahili zao viwe wazi ili wengine wasilalamike?
SUALA HILI ITAFAA LIFIKISHWE WIZARA YA MAMBO YA NJE ILI WAWASILIANE NA HUKO UBALOZI WA INDIA KUTAKA WAWEKE WAZI UTEUZI HUO WALIOUFANYA ILI KUONDOA LAWAMA KAMA KWELI HAKI ILITENDEKA.
wameshachakachua hao but komaa nao iwe fundisho kwao
ReplyDeleteNdio maana wana ficha listi ya waliochaguliwa.
ReplyDeleteUtaona hao waliochaguliwa ni ''Vilaza'' na ''Vihiyo'' wenye vyeti vya kughushi!
Hii ndio Tanzania bana!
Kwa bahati mbaya viongozi wetu wanazaa watoto bongolala na ndio hao wanaopewa nafasi kama hizo na kubanwa watoto wa wananchi wa kawaida.!
ReplyDeleteUkisikia mambo ya Bongo Tambarale ndio haya sasa.!
Ungetumia mbinu kumuomba Ofisa Ubalozi namba yake ya simu ya mkononi ukampigia simu kwa wakati wako, nafasi ungeipata kwa kuwa mngemalizana nje ya Ofisi.
ReplyDeleteTanzania ndio kama uijuavyo!
Nafasi ungeipata kama:
ReplyDeleteDAIMA USITEGEMEE HAKI 100% KWA 100% KTK NCHI YENYE SERA ZA KILIMO CHA KISASA NA CHA KI MUJINI MUJINI KAMA TANZANIA!
Ungepanga nae Ofisa mkutane bar ya karibu nje ya Ofisi,,,mfano pale Kinondoni Makaburini karibu na Ubalozi wa India!
Mimi nashauri atafute anuani au namba ya simu ya huyo balozi amjulishe jinsi machakato wote ulivyoenda na kuelezea malalamiko yake ikiwezekana iwe kimaaandishi. Inasikitisha sana pale ambapo mtu stahili anaponyang'anywa nafasi yake na kupewa mtu mwingine ambaye huenda hata hastahili.
ReplyDeletePole sana Wilbald,usikate tamaa, nami yalinikuta kama yako miaka ishirini iliyopita,lakini sikukata tamaa na sasa ni Daktari ughaibuni, nakushauri andika barua kwa Balozi nakala kwa afisa Elimu, nakutakia kila la kheri.
ReplyDeleteUsiwe na shaka, riziki yako utaipata tu.
Pole sana mdau, nimeguswa sana na hili. Huo kweli ni ubabaishaji. Mie nijuavyo wanaopata nafsi/ufadhili hupigiwa simu au hupata barua pepe ya kujurishwa na kupewa maelekezo zaidi manake si waombaji wote wanaishi Dar. USIKATE TAMAA. Jaribu tena kuomba ufadhili mwingine katika nchi zingine.
ReplyDeletewewe usikate tamaa bado sema unataka kuonana na balozi au viongozi wengine wa hapo ambao sio watanzania.
ReplyDeletehao wanataka kuchomeka watu wao au wamehongwa
sasa inabidi tuma e-mail elezea kwa kizungu kwenda katika e-mail ya embassy ya india nchini mwao as copy ukiwa umeituma kwa hao wa tz
sasa waki ignore itaonyesha wenzao umewatumia na imepita
ni vizuri ukaiweka hilo jina la maafisa kwani sio siri kwa kilichotokea au sijui kwanini umeficha majina yao.
wasukume tena usichelewe wiki hii usilale wakome kuchukua rushwa
Hao kama vile Abdalla Abeid na Mama Ubaya!!
ReplyDeletePole sana mdau, hiyo ndiyo hali halisi ya hizo scholarships kwa miaka mingi hapo Tz hata kabla ya wewe, sisi wengine tulipata scholarship kama hizo baada ya kutiliwa kifua na ma GODfather, vinginevyo hata mimi ningekosa, nazungumzia hayo 20 yrs back.Na utakuja kuniambia,utakuta watoto wa wakubwa serikalini na wengi wao hawana hata qualifications ndiyo watapelekwa huko, mimi binafsi yalinipata kama nilivyosema hapo awali na baada ya kufika huko kwa kweli niliona maajabu ya watoto wa wakubwa ndiyo walikuwa wengi huko na wengi wao walikuwa wakifeli mitihani na kurudishwa nyuma sisi wenzao tukipeta kilaini, na hata wengine baada ya kufeli sana basi wazee wao waliwahamishia nchi za ulaya kwenda kusoma.Kwa hiyo nasema kuwa huu ni uozo na roho mbaya ya baadhi ya viongozi wetu ambao hawana uchungu na nchi hii na wala hawawajali watoto wa wakulima.
ReplyDeleteJamani hizi contacts zipo kwenye website yao
ReplyDelete(ILA HAO ULIOONGEA NAO WALIKUWA WA NCHI GANI WA TZ AU?)
MUWE MUNAANGALIA HAYA WAPIGIE SIMU DIRECT
USHINDWE WEWE/NYIE
High Commission of India
Dar-es-Salaam
Telephone list
S. No.
Name[s] & Designation
[Mr./Ms./Mrs.]
Office
Phone [s]
Fax Nos.
E-mail [s]
*************************8
1
VACANT
High Commissioner
266 9044
266 9045
266 9043
hci@hcindiatz.org
hc.desalaam@mea.gov.in
****************************
2
Hemalata C. Bhagirath
Acting High Commissioner and
Minister/Director Indian Cultural Centre
266 4545
266 4547
266 4631
director@iccdartz.org
********************
3
Kunal Roy
Counsellor
266 9047
266 9043
couns@hcindiatz.org
****************
4
Tarunvir Chaudhary
First Secretary [HOC]
266 9048
266 9050
hoc.desalaam@mea.gov.in
fspol@hcindiatz.org
hoc@hcindiatz.org
**************
5
G.K. Pant
Attache [Pol & Eco]
266 9047
266 9043
hco@hcindiatz.org
*********
6 VACANT
Attache [Press & ITEC] 266 7017 266 9050 pic@hcindiatz.org
********
7 Pawan Kumar Garg
Attache [Culture] 266 4545 266 4631 icc@iccdartz.org
*******
8
V. Rajagopal
Attache (Admn & Cons)
266 9049 266 9050
admin@hcindiatz.org
cons@hcindiatz.org
admin.desalaam@mea.gov.in
Pole sana, ile ni taratibu tu. Wanatangaza wawe safe side kuwa taratibu zote zilifuatwa ila kwa kweli huwa wanakuwa na majina yao tayari. Yaani watoto wa mawaziri na wafanya biashara wakubwa.
ReplyDeleteNilishangga uliposema umepata scholaship na kwenda kusoma India ni vitu viwili tofauti.Ngoja nikupe hii ya mwaka, kuna Doctor alichaguliwa kwenda India kufanya kazi kwenye ubalozi wetu wa Tanzania kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wanaopelekwa India. Basi taratibu zote zilifanywa, aliaaga ndugu na jamaa, na familia ikawa tayari kwa kuondoka. Nyumba pia alishalipiwa. Wiki hiyo akaingia Wizara ya Afya kama Katibu Mkuu, basi akasitisha uhamisho wa yule Dr. kwenda India bila kujali ni kwa kiasi gani ataifadhaisha familia ya Dr na doctor mwenyewe, au nu gharama ngapi serikali ilishapoteza kuandaa safari ya Dr. Sawe. Yeye akaamua apelekwe cousin wake yaani Dr. Chale. Hii ndio Tanzania bwana. Ndio hivyo yule Dr wa kwanza alikuwa affected sana Pyschologically, lakini hakuna kiongozi yeyote aliyejali wala kumchukulia huyu mama Nyoni hatua.
Tuendelee kumwomba Mungu. aendelee kuwagusa viongozi wetu wawe na upendo kwa nchi na si kujali maslahi binafsi. Sasa balozi wa India hapo hana la kufanya, yeye kapewa majina na maelekezo hivyo anatekeleza tu. Ndio maana hupewi appointment ya kumwona kwa vile hana cha kukueleza.
India na Bongo ni baba mmoja mama mmoja!
ReplyDeletemkuu pole sana ,achana na scholarship za India angalia NUFFIC za Netherland na nchi nyingine ....
ReplyDeletePOLE KAKA HILA NDO HALI HILOVYO NCHINI KWETU , AKUNA VYA BURE WATU WAMESHA WEKA MAKIJINA YA NDUGUZAO , NA WENGINE WAMESHAONGA! POLE SANA
ReplyDeleteMDAU PARIS
Pole ndg yangu mtanzania, lakini kaka mpaka leo bado unawaamini Sunche.Kwanza ungeenda kula Kilipili mpaka upate saratani ya koo. Achana nao hao, kama wewe ni Mcha MUNGU basi amini tuu nafasi yako ipisehemu ambayo huijui. Nchi hii kaka Full usanii.
ReplyDeletePole sana inauma kwakweli.
ni kweli watu walipigiwa simu labda kama ulichelewa kureport kujaza form na nakuhakikshia jamaa hawana uchakachuaji wa aina yoyote kwa sababu nina rafiki yangu alikuwa anasita kuapply akihofia uchakachua ila amepigiwa simu na ameamini hakuna uchakachuaji....labda kama ulipigiwa simu halafu hukupokea or hukuiona!!!! but jamaa wapo serious sana na kazi yao!!!
ReplyDeleteJamaa hawana uchakajuaji wala nini...na kiukweli ukilinganisha ubalozi wa India na Wizara ya Elimu ..ubalozi wa India wako makini na hawana mambo kama hayo anayosema Wilbald...huwa wanapanga watu kutokana na points za ufaulu kuanzia form four hadi form six..na kama hukupata Division one form four au Six kupata hizo Scholarships za India huwa ni haiwezekani maana wengi ni vijana ambao huwa wamefaulu vizuri sana....
ReplyDeleteIla mdau usikate tamaa unaweza tafuta scholarships zingine za nchi zingine..jaribu marekani uingereza,sweeden,china na Japan..
KAKA POLE SANA,ACHANA NA WAHINDI TAFUTA ZA HUKU EUROPE AU AMERICA UTAFANIKIWA TU.
ReplyDeleteAma kweli ukisikia Mpira unachezwa wanakaba hadi kona ndio hapa!
ReplyDeleteScholarship za India inakuwa kama za Canada au Marekani?
NAMI PIA NILIOMBA SCHOLARSHIP HIZO ZA INDIA KWA MWAKA HUU, MAJIBU NILIYO YAPATA YALIKUWA KAMA YAKO MDAU
ReplyDeleteKIKUBWA NILICHO JIFUNZA: Kutokata Tamaa na Kuangalia Scholarship za Mataifa Mengine hasa ya Ulaya. Wadau wengi walinieleza nikifanikiwa india basi mie nina bahati. ie hiyo ndio michezo yao.
TUTAFIKA