Kaka Michuzi Habari za maisha na Maendeleo,Nilikua naulizia hivi ni Kweli Serikari ya Tanzania inasaidia Raia wake kurudi Nyumbani kutoka Ugiriki?
Kwa kuwa vijana wengi tumeamua kurudi nyumbani kutokana maisha yamekuwa magumu sana na pia tunashindwa hata nauri ya kurudia,tumeshajiandikisha kurudi kwa hiari lakini bado majina yetu kuitwa kutokana kuna zaidi ya watu milioni pia wa mataifa mbali mbali wamejiandikisha ikiwemo Afganistani wao ndio wanaongoza.
Kibaya zaidi imekua hata pa kulala tunashindwa kulipa hizo euro tano tano kwa mwezi kwa kuwa imebidi tukae nyumba watu labda 7 hadi kumi,na nyumba zenyewe kupatikana imekua tabu Chakula tabu.
Nyumba hazina hata umeme,madeni ni makubwa.
Hata wagiriki wenyewe wanasikitika,kula ukipata mara moja tu ushukuru kwa siku.
Na kutoka hapa kuelekea ulaya nyengine gharama zake ni mara mbili ya kutoka Bongo kuja Ulaya kwa kuwa connection ya rahishi angalau kufika Italy tu ni 2500 ukipata chini ya hapo basi ni passport feki unakamatwa unakua ushapoteza hela.
Imebidi baadhi yetu kuna ambao wamejipatisha vitanda hospitalini ili kuweza angalau kupata sehemu ya kuweka ubavu na chakula,huku Omonia kuna foleni chakula cha bure lakini hadi ukiifikia kishamalizika.
Je ni kweli kuna utaratibu unaofanywa na serikali ya Tanzania kutusaidia kurudi?
Maana tulipita hapa kutafuta maisha lakini hao ndugu zetu wa zamani hapa bichi wao wanasikitika na wengi wanarudi kwa vile wamekua na akiba ila sisi ndio tunaofika hapa tunapata shida ni balaa tupu na pia wametushauri tuondoke ijapokua baadhi wanatusaidia saidia.
Ahsante
Mdau wa Ugiriki
Nakumbuaka kuna mtu aliwahi kutoa comments kwenye hii blog kuhusiana na ndugu zetu mloko ugiriki kwamba mje nyumbani mkamnanga sana sana sasa imekuwaje tena?!!
ReplyDeleteNawaonea huruma sana natumaini Sirikali yetu imesikia kilio chenu japo na yenyewe ipo hoi.
Jamani hawa ndugu zetu wanahitaji msaada wa haraka.i hope selikali itachukua hatua.wizara ya mambo ya nje mpo? as long as wameamua kurudi nyumbani selikali ijitahidi.other wise jamani kaka michuzi si unaweza arrange something like emergence fund kwaajili ya ndugu zetu hawa,watu tunaotaka kusaidia tuwasaidie waliotayari kurudi home.mfuko utangazwe kwenye blogs nyingi na hata vyombo vingine vya habari,jast like kuwachangia waliopata mafuriko au mabomu aula.am sure kama fund itapata usimamizi mzuri tutapata ya kutosha na wengi walio tayari kurudi home watarudi.umoja na uzalendo jamani.poleni sana ndugu zangu wa ugiriki.hiyo hali imenifanya nitoe machozi.ni wazo jamani.
ReplyDeletemdau toka Houston.
Kweni wakati mnaenda huko mlituuliza wadau??si mlienda kutafuta maisha sasa komaeni na si kulialia hapa!!si mlisema bongo alosto mkaenda nje,komaeni hukohuko,mwalialia nini hapa!
ReplyDeleteHasa huku Bongo unarudi kufanya nini. Mwanaume hakimbii matatizo anatatua matatizo. Bongo itabidi tukupe jembe ulime. Mbona kuna picha za harusi na Kopa pia alikutembeleeni huko. Au wewe unakejeli wenzio.
ReplyDeleteKwani walifikaje huko? Walifuata nini? Walipelekwa na serikali??? Mambo yao yalipokuwa mswano wameisaidia vipi serikali yangu? Kama kuna walionufaika ni familia zao, basi wacha hao ndugu zao wawarudishe..... Mimi sitaki kodi zangu zitumiwe ovyo ovyo namna hii...Lama ni wanafunzi walipoelekwa na serikali basi hapo niko nao na nitaishinikiza serikali iwarudishe. Otherwise, they took a calculated risk so let them get the consequences. Ng'oo msitumie kodi yangu kwa hili, there are better things to use it for! My grandma bado kijijini hana maji safi yet you guys suggest we use our hard earned tax monry for ma brothermen na wauza unga?????
ReplyDeleteNchi za kibepari tunafundishwa kujiwekea AKIBA, kwani matatizo yako ni yako mwenyewe na HAKUNA wa KUKUSAIDIA.
ReplyDeleteTatizo letu waafrika tumeshazoea BWELELE tukitegemea kuwa ndugu na jamaa watatusaidia wakati wa shida.
Nyakati hizi za utandawazi ni lazima tufunguke macho kuachana na mambo ya UJAMAA.
komaeni huko huko hali itakuwa nzuri hivi karibuni! kumbuka vijijini kwenu mlipotoka kuna umeme? acheni Ubishoo, Bongo kugumu. mtakuta watu wako mbali mtaishia kukata tamaa na kuishia kujiua au kunywa gongo. ikiwezekana hata jilipueni.. na Vueni hata samaki. Ugiriki si kuna Bahari? kama unakosa hela ya kula Ugiriki utaipata bongo?
ReplyDeletePOLENI WANDUGU UGIRIKI:
ReplyDeleteNaungana na Wadau wa hapo juu 1 na 2 , sasa ni wakati muafaka kwa kuwasaidia ndugu zetu kwa janga hili.
Nakumbuka mimi pia ndio niliwashari kupitia humu Globu ya Jamii ndugu Ugiriki warudi nyumbani Tanzania ikiwezekana waje kukata mkaa Kaliua-Tabora.
Tunaweza kujipanga ili kufikisha malengo ya suala hili kwa ufanisi tena sana.
Mfano:
-Huku nyumbani Tanzania ndio kwenye mhimili wenyewe zipatikane akaunti za M-Pesa ili michango itiririke humo kwa kukusanywa.
-Nchi zingine ambako wana nafuu ya Maisha nao hata kama wana Uraia mwingine lakini asili haifi daima, Wana Tanzania wajipange wachangie waliopo huko AMERICA, CANADA, na EUROPE hiyo hiyo angalau ingawa karibuni sehemu zote za Dunia Matatizo ya Kifedha na Kiuchumi yamepiga vilivyo laikini huko Ugiriki ndio zaidi.
-Tulishaona kuwa mnao Uongozi wa Jumuia ya Watanzania huko watoe mawasiliano ili matekelezo yafanyike.
1.Tupate idadi ya waliopo ili tuanze na Msaada wa dharura kwa kuwawezesha ktk suala la CHAKULA na MALAZI hata kama ni vitanda vya Hospitalini huko Ugiriki.
Halafu,
2.Orodha ya majina yenu ndugu kwa majina kamili ikujulikana idadi mpango utafanywa kwa pamoja na kama zoezi likitekelezwa iwe tumemaliza sio itokee mtu asitoe jina lake kwa uzembe wake halafu baadae alalamike msaada haujamfikia.
3.Baada ya kupata idadi kamili ya wahusika tupange mpango wa Usafiri wa group angalau uwe kwa gharama za chini ili msaada uwafikie wengi iwezekanavyo.
DAIMA PAMOJA TUNAWEZA!
MUNGU IBARIKI TANZANIA!
Hivi we mdau wa mada hujasoma Geographia ulipotoka huko? kwani Ulaya ipo mashariki? hata ufanye safari kutokea umangani kwa nini usingeenda moja kwa moja tu unapotaka kwenda?Umangani hali ni shwari tu hao wanaolia ni wageni tu waliosikia kuna visa za ubatani kuingia umangani- Bila kuulizia kuna situation gani ya kutoka hapo kwenda mbele.
ReplyDeleteAnaetaka safari awasiliane nami njia zipo nyingi tu,hela yako tu. anaetaka kurudi kwani alifika vipi hapo?
Next time plan well ahead.Goodluck .
Mdau wa zamani Ugiriki sasa Bradford-UK
KAKA MICHUZI HARAMBEE HIYO FASTA KABLA YA HATARI IELEWEKE KUWA SIO WATU WAZIMA TU KUNA MPAKA WATOTO JAMANI TAIFA LA KESHO HILO LISITEKETEE KWA NJAA NA MARADHI HATARISHI YA BARIDI(KULALA KWENYE NYUMBA BILA YA UMEME HEATER-ON) UGENINI HUKO ULAYA.
ReplyDeleteMhh hawa si ndio uliwarusha hapa juzijuzi wanacheza taarabu na malkia wa mipasho! tena walikuwa wanatunza juu wakadai maisha magumu Ugiriki ila wako bomba wanangaa na kujirusha. Ama nimechanganya habari jamani?
ReplyDeletehuyu mdao aloandika hii habari ni muongo na hayupo greece.
ReplyDeleteulaya hata nchi ikichoka haiwezi fikia bongo.bakini huko huko mkomae.
ReplyDeleteKaka yamewiakuta,Poleni sana,..ila bongo ipo bomba kwa sasa,mlikimbia bure,ngoja chadema wachukue jimbo ndio ataanzisha harambe ya mchango,kwani mda huu wako buzy,.
ReplyDeleteHiyo pesa ikajenge mabweni ya chuo cha mkwawa...wameshajilipua hao...ni wagiriki labda ombeni serikali yenu ya kigiriki iwalete kutalii tanzania...eti kama hauna nauli...utafikia wapi na utaishi vipi mjini....sorry guys...u shud know better...si mlitaka chai..iweje mnalalamika mnaungua.
ReplyDeletedadi na mungi inakuwaje sasa huko nanyinyi mshawekeza na biashara zenu amonio ...mtarudi ama mko katika foleni ya chakula chabure..
ReplyDeletemdau beljam
hiyo pesa bora kusaidia wahanga wa mafuriko au wahitaji nchini...mambo yakiwa sawa hawakumbuki nyumabani bali kuponda na vijembe kuhusu maendeleo...si hukumu...lakini sorry guys, u shud know better.
ReplyDeleteKwani serikali ndiyo iliwapeleka huko hata kuwatwesha mzigo? Ya nyumbani na madaktari tu yamewashinda seuze hayo
ReplyDeleteSio Ugirirki tu. Kwa kweli serikali yetu sijui niseme inaziba macho kwani kuna watanzania chungu nzima wanaumia kwenye ma-nchi ya watu.Balozi zetu nje naona zinashughulika zaidi kusambaza siasa na wala sio kuwasaidia watanzania walioko nje.
ReplyDeleteNasema haya yote kwani hata mie yashanikumba haya
Kama nchi uliyopo hakuna vita au machafuko, SI JUKUMU LA SERIKALI KUKURUDISHA. Labda kama serikali ilikupeleka huko. Lakini kama ulienda kwa harakati zako, maji uliyavulia nguo mwenyewe...
ReplyDeletePoleni sana ndugu zetu, maisha ya nje siyo rahisi na si kama bongo unweza kwenda kwa jirani ukakaribishwa mezani hata kama hukutoa taarifa ya kuwatembelea.
ReplyDeleteMungu atawasaidia mrudi nyumbani salama.
hatari,,,,,,,ndugu zangu msaada msitegeme maana hapo uwanjani mtu unarudi na nauri yako wanakuliza....kuna mijitu mijinga pale....ukisema tuu mi mtanzania wanakwambia kaa pembeni....maswali yanaanza ulikwenda kufanya nini huko? kwanini umerudi na passport ya muda?jamani mi kaa sio raia ...wakati tunaona nchi za wenzetu raia hata kuguswa hawaguswi,,,,,sisi utatiwa maswali kama ndio unaomba visa...hapo yote wanataka dolla 50....ndugu zangu Ugiriki bora mkimbilie ulaya zingine huko bongo nako balaa nchi imefirisika bora hata huko mliko!!
ReplyDeleteNaomba niweke hili swala sawa hapa mimi kama mdau wa serikali ya Tz: Haukuhisisha serikali wakati unaenda hukop Greece au kokote kule sasa iweje leo serikali ikurudishe Tz kwa gharama zake na wakati ulienda kwa mambo yako binafs. Wengi mlioko Greece mko kwa kuzamia hilo pia nitatizo lingine. Kama serikali ya Tz hatuwezi kuanza kutumia pesa eti kurudisha watu nyumbani walioshindwa maisha nje ya nchi kwa kodi za mTz aliebaki nchini, kama ni hivyo basi kila mtu alieshindwa nje ya nchi itabidi tumrudishe na je,mkirudi mtafanya nini huku? Msanii Matonya juzi tu alikua Greece kuperform kwa sherehe ya wabongo kwahiyo pesa za starehe mnazo ila nauli za kurudi nyumbani hamna mnataka serikali. Tuna mambo mengi sana ya kufanya wandugu not that one. THINK BIG
ReplyDeletePoleni jamani wa Ugiriki na wote mliokimbilia nchi za nje kutafuta hayo maisha kisha mkadondokea pua maana mlisahau wahenga waliposema...Mkataa kwao ni mtumwa...na nyumbani ni nyumbani hata kama kichakani...nyie mlidhani maisha bora yapo kwenye maghorofa ya vioo? basi niwang'ate sikio kuwa hata huku kwetu Wachina wanatudondoshea magorofa ya vioo kama hawana akili nzuri vile maana Bongo kama New York ilihali Zenji kama Pueto Rico kwa kina Rihanna ati, nyie mwaililia Serikali? kwani bongo kuna serikali? ishauzwa hivyooo...wenzenu wa Kigamboni waliambiwa na Magufuli kama hawana nauli wapige mbizi sa kama huyo ni waziri wa serikali mnayoililia anatoa majibu hayo kwa walalahoi mnategemea serikali itawajibuje?...simple...PIGENI MBIZI...Mnalo hilo limewaganda!
ReplyDeletekwani siku hizi leseni za kuuza karanga hazitoki huko Ugiriki? au haziusikii tena siku hizi?
ReplyDeletejamani mm ningependa kuitete serikari yetu ya tanzania kwamba ilichatoa matangazo kila zehemu kuanzia huko uliko ubalozi wetu nchini italy na hapa ugiriki iwapo kama kunamtanzania yoyote yule amabae aliyeshindwa maisha anaweza kusaidiwa na serikari ya kitanzania na hata wale waliokuwa mazabe pia iwapo kama maisha yamewashinda pia ubalozi unaweza kuwasidia lkn inakuja kitu kimoja hapa hawa wabongo wengi wanarudi nyumbani ni waganina maisha haya ya huku na njia zipo kibao za kutaka kwenda mbele lkn wasilete sababu kama wanateseka mgiriki anatoa ticket na mzigo mdogo hanakupa na hawa wabongo huku wanataka tiketi za bure na kipumbu chake anacho na kashajipiga soap soap ili hata akirudi home mwajuma amuone fresh hapa ndio shida kwa hii criss lkn sio hivyo kama mnavyozania huko home sio na huu mpango mwingine nitamuunga mkono mdau hapo juu kuhusu wazee wa nondo hapo waachee tamaa jamani ..
ReplyDeletena kama ngomo ngumu mbona wapo jamani mwanaume anastahamili vishindo sio sio bongo -ubatani -ugiriki - mbio bongo kita kidogo ujuwe tamu na chungu
mdau ugiriki
LOL Wadau samahanini inanibidi nicheke kwanza. Hawa watoto (Serengeti boys) wana matatizo sana, Ni nani sijuwi anawatapeli huko Bongo akiwambia waje Ulaya ndio mpango mzima! na kutokana na elimu yao ndogo ya kuchangiwa basi wao mbio wanatafuta hela kwa njia yoyote ile waje Huku, wengine wanauza vyao,wengine wanadhulumu ndugu zao NK ili waje huku, Swali linakuja Utakwendaje sehemu huijuwi wala humjuwi mtu utegemee ukifika tu Utakuwa tajiri? Je ushasahau kama umekuja kuanza maisha mapya? ushasahau kama maisha popote pale sio lelemama? hizo ni miscalculate kwa kuwa mtu akiwa anapanga safari kama hiyo isiyokuwa na mwenyeji inabidi awe na plan A na B. sasa hayo matatizo ndio hiyo plan B sasa jifunze jinsi ya kupambana nayo, sio kuomba misaada Serekalini na kwa usiowahusisha na safari yako. kidokezi Je ikiwa wewe uko hapa unalia hivyo na walioko Sudan huko watafanya nini? Ushawasikia humu? kwa kumalizia nisikuchoshe msomaji Ugiriki ni kama sehemu yoyote tu ya juu ya kukumbwa na crises lakini bado hatujafikia kuomba ticket ya kurudi, labda maisha yamebadilika hiyo ni kawaida ya maisha tu, na Uthibisho mnauona Mtu akifa tunamsafirisha anakuja kuzikwa nyumbani, Mabichi mengine Unazikwa hapo hapo, Wanamuziki wanakuja na watu wanajaa kwenye mashoo, sasa huyo anolia huyo naona mawili Hayupo hapa Ugiriki au Hashirikiani na Watanzania waliopo hapa. Ahsanteni.
ReplyDeleteHuyo aliye-post kuhusu Ugiriki kuna kitu kimemsibu, anaonekana ana mawivu yake na watu wa umangani.
ReplyDeleteMaisha kila sehemu almost yaleyale tu esp. kipindi hiki worldwide matatizo ya kiuchumi yanazikumba karibu kila nchi.
Gangamala mtoto wa kiume sio kupakaza yasiyokuwepo, ulifikiri unaenda, unatengeneza maelfu ya euro halafu unarudi Bongo fresh nini???
Unapenda vya mteremko eeeh...?
Ya nini kuteseka Ugenini huko ughaibuni Ugiriki?
ReplyDelete1.Si bora mrudi Bongo mje kulima?
2.Isiwe tabu maisha ni popote kwa nini msirudi kuja kukata mkaa kufuga nyuki na kupakua asali Kaliuwa ,Tabora?
3.Ebooo kwa nini mnateseka bure mnakufa na tai shingoni kwa nini msirudi kuja kuvulia samaki huku Bongo, huko mmeshakwama hata kama Ugiriki mnavua samaki?
4.Msiwe kama baadhi ya Watu hapa Dar Es Salaam wanao amini maisha bila Kariakoo au Magomeni haiwezekani kitu ambacho sio kweli,,,hii si sawa na ninyi huko Ugiriki?
5.Mpo ugenini na mambo yameharibika 'Ki Uchumi na Ki FEDHA' la muhimu mkikomaa huko msije mkajirahisi maana Giriki na Mwingereza Sera zao ni sawa ktk Mashariti ya Misaada!
Licha ya chakula cha msaada kwa foleni,
ReplyDeleteKazeni buti zaidi na mjihadhari sana na Giriki kwa kuwa kwa mipango ya Ubaazazi, Umende na Ubasha Mwingereza hamwingii mkongwe wa siku nyingi Giriki!