Kutokana na kuwa kila mmoja anaonekana anaharaka kumzidi mwenzie,imezipelekea gari hizi mbili ambazo zote ni za biashara (Taxi) kusimama katika eneo hili huku kila mmoja akikataa kumpisha mwenzake.hali hii imekuja kutokana na upande mmoja wa njia hiyo kusimama lori lililokuwa linashuka mizigo na kuifanya nyia hiyo kuwa ni moja tu.
Home
Unlabelled
Madereva Taxi wetu hawa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hili ni tatizo ambalo linaendelea kukuwa kila kukicha. UBISHI, USHINDANI usiokuwa na faida yoyote!
ReplyDeleteKuna nchi ambazo zina magari maradufu ya BONGO lakini kwa nadra sana utakutana na upuuzi huu.
Kama mwenzako alianza kuingia ama kukuonyeshea ishara ya taa,wenzetu kwa tabia ya kibinadamu kabisa anamwachia mwenzake apite ukizingatia nafasi sehemu yenye nafasi finyu kama hiyo.
Lakini madereva wa BONGO, haswa wa DALADALA na TAXI, wana ubishi usio na maana kabisa. Kama hapo sasa, hao madereva wawili sana sana wanapunguziana muda wa kutafuta mshiko, mwisho wa siku ule muda aliopoteza hapo angeutumia kujazilisha mfuko wake ama hata angepata dakika za kuwahi ugali nyumbani LoL!!
Utamaduni wa kumjali mwenzio una manufaa, kushinda hasara za kutaka kukomoana pasipo na sababu ya msingi. Ingetokea dharura hapo, mfano mgonjwa anataka kuwahishwa hospitali, kwa sababu ya upuuzi huo mtu anaweza hata kupoteza maisha.
TUFIKIRIE kabla ya KUAMUA!!!