Na Mwandishi Wetu.

KIWANGO kilichoonyeshwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, katika mechi dhidi ya Msumbiji, kimesababisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kutamka kuwa amekerwa na kiwango hicho na kulitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanya maamuzi magumu ya kuvunja timu hiyo.

Stars inayonolewa na Kocha Jan Poulsen ambayo hivi karibuni ilivaana na Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuambulia sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2013), ilishindwa kuwafurahisha mashabiki baada ya kutoonyesha uwezo mzuri.

Akizungumza muda mfupi baada ya mechi hiyo, Zitto alisema kuwa kuna haja ya TFF kufanya maamuzi ya kukibadili kikosi hicho ambapo kwanza wanapaswa kusitisha mkataba wa Poulsen ambaye ameonekana kushindwa kusonga mbele.

Aliongeza kuwa mbali na kuondolewa kwa Poulsen, pia timu inatakiwa kuvunjwa na kuitengeneza upya kwa kutafuta vijana wadogo kwa kuwa wachezaji waliopo wameshindwa kuonyesha uwezo wa juu.

“Nimechukizwa sana na kiwango kilichoonyeshwa na timu yetu, nadhani kuna jambo linahitajika kufanyika haraka na kwa kuanzia TFF waangalie ni namna gani wanaweza kumtimua huyu Poulsen, ni dhahiri ameshindwa kuibadilisha timu,” alisema Zitto na kuongeza:

“Pia waivunje hii timu kwa sababu wachezaji wengi wameshindwa kubadilika hali inayowafanya kila siku kuwa na matatizo yaleyale. Kwa hali hii kila siku timu itazidi kutengeneza mashabiki wa kuichukia kuliko wa kuipenda.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Acha siasa katika mpira. Wachezaji TZ hakuna unategemea nini?

    ReplyDelete
  2. Naunga hoja 100%

    ReplyDelete
  3. je akitokea mbunge mwingine akataka timu ya Taifa isivunjwe tutamskiliza nani? Sioni busara yoyote kwa kuifanya hii rai ya Mbunge kuwa ni mada. Hakuna timu yoyote duniani ikavunjwa kutokana tu na anavyoona mbunge. Yeye ni Nani?
    Timu huvunjwa kwa udikteta wa Raisi au kwa ridhaa ya wataalamu wa michezo na siyo kila siku wajitokeze waliokuwamo na wasiokuwamo waongelee Timu ya Taifa.Waacheni wataalamu wa michezo waongee na nyie wabunge nendeni Dodoma mpiganie nchi iwe na maji na umeme na mkishafanikiwa huko ndiyo mje huku kwenye michezo.

    ReplyDelete
  4. Mhe,Mpira ni maandalizi,hivyo hata vijana unaowataka waje bila maandalizi hutavuna chochote.

    Lima,panda,palilia.vuna.We wataka mavuno tu itawezekana wapi.Siasa katika hili hapana.

    Unataka timu ya Taifa ivunjwe,halafu iweje!Ulete malaika wacheje maana wao wamebarikiwa na wanamiujiza hawahitaji maandalizi.

    Nenda jimboni mambo mpira mwachie Ngoswe.

    ReplyDelete
  5. Huyu Zito Kabwe imekuwa ni hulka yake kulaumu tu. Hebu atwambie kuna timu gani toka Kigoma katika Premier League. Jamani wanasiasa wetu kazi yao ni kupayuka tu. Kusma na kulaumu ni jabo rahisi sana. Soka la Tanzania limeshaelezwa mara lukuki kwamba tunahitaji kuwek msingi imara wa soka la vijana. Huyu zito mara posho za wabunge, mara urais uwe miaka 35, mara mambo ya madini alimuradi waswahili wamesema mpanda farsi wawili lazima ataanguka.Yeye anapapanda farasi wengi kwa wakati mmoja. Namuona huruma masikini Zito hajui anataka nini.Na kama anatafuta kitu kwa kudonoa donoa kila kitu ajue hafiki popote. Hebu chukuweni mfano wa Dk. Shein hakupata uongozi kwa kuhonga magazeti ili kila siku uonekane bal fanya kazi kwa uadilifu na kuwa mkweli na muwazi na kumini Mungu.

    ReplyDelete
  6. Safiii sanaaa!

    Wazo zuri la Mhe. Zitto Kabwe.

    Nafikiri wapo Wadau wenye kutakia maendeleo walikuwa nalo dukuduku la wazo kama hili mioyoni akiwemo Mhe. Raisi JK aliyefanya mengi kuitakia mafanikio nchi yetu ktk Soka lakini hatukupata kitu.

    Tatizo hii timu imekuwa kama Mzimu wa Tambiko kwa Wajanja na Wadau wa Maslahi kuitumia ili kufikia malengo binafsi badala ya Maendeleo ya Soka ikiwemo TFF na Wadau Vinega wa Maslahi.

    Kufuatia Mafanikio ya Chipolopolo ya Zambia mwezi uliopita wapo Wadau kwa ghadhabu walipendekeza tuipandishe TAIFA STARS ktk ndege mbovu ianguke wafe Wachezaji wote ili tuanze upya kwa kutafuta Wachezaji wapya kama ilivyowatokea Zambia mwaka 1993 labda na sisi tutapata mafanikio ya Soka!

    ReplyDelete
  7. Anachoshauri Mhe. Zitto Kabwe ni sawa.

    Mnaompinga nafsi zenu zinawasuta. Hata nyinyi hamfurahishwi na uchezaji wa timu yetu ya Taifa Stars. Yaani ni uchezaji unaoudhi, unaokera na unaokatisha tamaa kweli kweli.

    Kilichomfanya Mhe. Zitto aseme hivyo ni uchungu na uzalendo alionao tu. Katika hili hakuna mambo ya siasa kama mnavyodai.

    Ni kweli kocha huyo atimuliwe kama zinavyofanya nchi zingine na timu hiyo ivunjwe ili iundwe nyingine upya kwa kuchagua vijana wengine kwa umakini mkubwa.

    ReplyDelete
  8. Naunga mkono likocha hilo lifukuzwe na mjitimu huo usambaratishwe iundwe timu mpya, maana tumechoshwa na maudhi ya kutocheza vizuri ya kila siku. Hivi tunashindwaje kupata vijana wenyesifa wakutuwakilisha katika timu yetu ya taifa stars katika mamilioni yoooote haya ya watu tulivyo??? Kocha atimuliwe na timu ivunjwe HAKUNA MJADALA. Full Stop.

    ReplyDelete
  9. Mh. Kabwe ni ukweli ulio sahihi, na nina kuunga mkono 100%. Tatizo la mpira wa Tanzania ni kwamba wachezaji wetu wengi (Simba na Yanga, Azam, n.k) wameweka uchawi mbele kwa manufaa yao wenyewe. Wewe angalia tu wale waliocheza ile siku, hakuna hata mmoja mwenye akili ya mpira na kipaji. Yaani watu wanakimbia tu uwanjani, hakuna cha formation wala nini. Tanzania mbona mpira hupo jamani? Wewe unategemea nini kama unaweka wachezaji dizaini ya Ngassa? Ngassa huyu huyu alifeli Marekani, uchawi jamani kwenye mpira umepitwa na wakati lazima tutizame mbele. Kinachosikitisha pia hata raisi wa TFF anachekelea tu kuwa eti vijana wetu wana uwezo, seriously...huyu mtu ana akili kweli ama yupo tu pale kwa ajili ya mlo? Tema Ngassa, Nsajigwa (tena huyu ndo feki sijuwi kwa nini amekuwa captain, hana technics zozote wala kipaji yeye kukimbia tu). Temeni wachezaji wote, wachawi wale, tunataka vipaji na ndiyo maana raisi Mwinyi aliwatukana Taifa Stars miaka ya nyuma kuwa kichwa cha mwenda wazimu. Ni kweli kwani mchawi afundishiki kwa sababu hana kipaji cha uchezaji. Bongo wachezaji wanaroga mpaka kocha ili wapangwe, s ujinga huu?

    ReplyDelete
  10. aliyeComment namba 1,3,4,5 inaelekea kama sio watanzania. mnaona rahaaaa taifa stars kutosonga mbele. Mh. Zitto hajaamuru timu ivunjwe bali amependekeza kwasababu hili litimu pamoja na Kupewa support zote kifedha na mazingira bado nimambumbu ikiwa pamoja na nyie mnaowasupport.. vichwa venu vilaza kweli.. Timu ivunjwe watafutwe vijana wenye uwezo.. eti Zito akapambane na umeme kwani yeye Tanesco?? nyooooo!! Taifa stars ivunjwe.

    ReplyDelete
  11. ukweli tunaitaji vijana wadogo kama zambia tutao wafua adi kufika hiyo 2013 wanakuwa wameiva, come ebu tuwe serious ata kidogo basi , tff ni wababaishaji hata makocha wanao wachakua ni wababaishaji tu , mimi naona hata TFF viongozi waote wajiuzuru , kwani awafanyi kazi zao poa kabisa, ni wachawi na wana njaa na kujali matumbo yao awana uchungu kabisa na timu yetu ya taifa .

    mdau paris

    ReplyDelete
  12. Tatizo sisi wa TZ maneno mengi, vitendo sifuri. Hatukuwahi kuwa na kiwango cha juu cha mpira hapa TZ, hao akina sijui MAnara, Sembuli, Mogella, Gaga, waliipa stars kombe gani?

    Ethiopia, Sudan, Zaire(Kongo ya sasa)na hata Uganda wanaweza sema zamani walikuwa juu sasa wameshuka.

    Mimi tangu nakua miaka ya themanini mpaka leo nina miaka 40 nasikia hadithi tu, mara kocha atimuliwe mara timu ivunjwe, mara viongozi wabovu na mambo mengi yasiyo ya msingi.

    Sijasikia mtu akisema yafuatayo
    1. Tuwe na academy za michezo mbalimbali mf. ya footbal iwe Kigoma, riadha (Arusha ama Singida), ngumi (Mbeya), indoor games (maeneo ya pwani) n.k.
    2. Umitashumta, Umiseta, michezo ya majeshi na vyou viimarishwe na sio mabonanza kama SHIMIWI.
    3. Sera itayosema michezo ni ajira na sio afya ama ujirani mwema kama ilivyo sasa.
    4. Serikali na vilabu wawekeze kwenye academy.
    5. Simba na Yanga zendeshwe kisomi, wawe na shule za watoto(elimu ya kawaida na mpira). Sio sasa kuna vi-academy vinafundisha mpira tu.

    6. Serikali igharamie watu waende wakafifunze mfumo wa Arsenal ama Ajax.

    Kuna mengi naweza kuchangia lakini watu kama sisi hatupewi nafasi japo tunaweza kabisa kuisaidia nchi.

    Waziri wa michezo kama anaona nina hoja na ninaweza kumsaidia awasiliane nami kwa namba 0654 864017

    ReplyDelete
  13. It's about time someone should talk about this! Welldone H.E

    ReplyDelete
  14. wzo zuri hilo naunga mkono

    ReplyDelete
  15. NAKUUNGA MKONO TANZANIA INATAKIWA MABADILIKO SANA KIMPIRA KWANI HAKUNA MAENDELEO KABISA KATIKA NCHI YET , ZAMBIA ILIKUFA TIMU NZIMA NA MATATIZO YA UCHUMI NDIO HIVYO NI MAKUBWA LAKINI WANA MOYO HAKUNA MCHEZAJI MLEVI KULE WALA ALIKUWA MPENDA MALAYA. WACHEZA WA BONGO WAKITOKA MAZOEZINI KWANZA KITUO NI BAR , UTAFIKIRI NI MAMENEJA WA CRDB,AU NBC, HAKUNA NIDHAMU HILO TU HAKUNA MCHEZAJI ANAWEZA KAZI KATIKA FORMULA HIO POMBE NA WANAWAKE. TATIZO LINGINE KUJUANA KAMA HUONGEI VIZURI NA TENGA BASI WEWE HATA KAMA NI MARADONA HUCHAGULIWI! KUNA SO MANY TALENTED PLAYERS AMBAO TFF HAWATAKI KUWAJUA, MIKOANI . TIMU YA UNDER 17 ILIOSHINDA BRAZIL MIAKA YA NYUMA TFF IMESHINDWA KUMCHUKUA HATA MMOJA KWA SABABU WENGI WALIKUWA WACHEZAJI KUTOKA KIGOMA, BASI HILO NI KOSA- HUYO RAIS WA TFF LEONALD TENGA HATAKI KUWASHIRIKISHA WACHEZAJI WAKONGWE KAMA KINA SUNDAY MANARA KIBADEN,ALOO MWITU,KATIKA KUZALISHA MATUNDA BORA HATAKI KAZI NI VIJEMBE TU SASA SAA NGAPI MPIRA UTAENDELEA TANZANIA? HUYO KOCHA POULSEN SIO KOCHA WALA HANA WADIFA WOWOTE ULE KATIKA NCHI YA DENMARK WALA HAULIKANI KUTOKANA NA WAKAZI WANAOISHI DENMARK KUSEMA KWAMBA HANA SIFA YOYOTE YA KUWA KOCHA WA NATIONAL TEAM. ANGALIA UONGOZI WA TIMU YA TAIFA MPAKA SASA HAPO ETI KIT MANAGER NI MTOTO WA KIGOGO FULANI HAPA TANZANIA AMBAYE HAJUI LOLOTE LILE KUHUSU MPIRA, WALA DANADANA HAWEZI KILA SIKU YUKO BAR ZA MIKOCHENI KULEWA ATI NI KITTY MANAGER. MAFANIKIO YA MPIRA NI COMBINATION YA VITU VINGI. IDEA KUTOKA KWA WAKONGWE,HISTORY,HESHIMA NA KUSIWE NA SIRI SIRI NA ULAJI WA PESA KIJINGA NA KUDHULUMU HAKI YA WACHEZAJI WALIOKUWA NA UWEZO HAPO TU NDIO TUNAWEZA ATLEAST KUONEKANA NI AIBU MIAKA YOTE MAENENO MANENO TU YANGA,SIMBA WAKATI HAKUNA LOLOTE WANALOLIFANYA . UJUMBE WANGU KWA TENGA WAHUSISHE WACHEZAJI WENZAKO WA KALE ILI KUFANYA TANZANIA BETTER KATIKA FANI YA MPIRA HATA RWANDA NA BURUNDI WANATUSHINDA KUZALISHA WACHEZAJI PROFFESIONAL MAKLABU MAKUBWA UKAYA NI AIBU, AU TUVUNJE KABISA MPIRA WA MIGUU KWA WANAUME WAENDELEZWE WANAWAKE AMBAO NINAAMINI WANAWEZA FANYA VIZURI-

    ANGALIA NCHI ZOTE ZA MAGHARIBI UTAWALA NI KUTOKA KWA WACHEZAJI WA ZAMANI AMBAO WANAFAHAMU NINI MATATIZO YA MCHEZA MPIRA NA PSYCHOLOGIA YA MWANA FOOTBALL. NDUGU TENGA WAHUSISHE WACHEZAJI WENGINE BORA WA TANZANIA ILI KUZALISHA MATUNDA BORA,ACHA KASUMBA ZAKO ZA KIAFRIKA AFRIKA JAPOKUWA UMEKWENDA SHULE HIO ELIMU YAKO TUNATAKA TUONE MATUNDA YAKE KWA JAMII NZIMA YA TANZANI

    ReplyDelete
  16. badilisha mfumo mzima kuanzia utawala wa walarushwa na mafisadi walioko katika uongozi huo wa mpira tanzania wapeni wachezaji waliokuwa wakicheza mpira miaka ya 70,na 80 ndio wanoweza kuongoza timu na kuleta mafanikio, ni aibu hata somalia wanatufunga ,burundi , rwanda sisis hivi tumetoka wapi? Rais Kikwete kajitahidi kwa hali na mali kunyanyua soka tanzania lakini wapokeaji ni wanafiki kazi kujinufaisha wao tu . hayo malipo yao na pesa wanazoiba kila siku ni jasho la kila mtanzania mlipa kodi, na wazungu walipa kodi ambao sasa wananza kutustukia kwa misaada kila kukicha na hakuna chochote cha maana kinachofanyika kwa sababu za hao Kina Tenga kula pesa zote za TFF na hakuna kazi yoyote nzuri inayofanyika,kudhulumu watu viwanja vyao, huko mbezi beach, tegeta kwa ajili ya pesa za ufisadi za TFF, na hakuna lolote linalofanyika kwa kumfurahisha mtanzania, PLEASE MR PRESIDENT kwa uwezo wako pangua uongozi huo wa TFF ndio nchi itaendelea kimpira

    ReplyDelete
  17. Mdau wa ajali una hulka za kichawi! Hata hivyo hata hiyo timu ya Zambia iliyopata ajali ilikuwa ni timu nzuri pia, sio mbofumbofu kama hii ya akina Juma Kaseja!

    ReplyDelete
  18. je nani anafuatilia mafundisho ya kocha huyu na wachezaji?inawezekana wachezaji ndiyo hawafundishiki,ukiachia mbali lugha.mpira wa miguu unahitaji nidhamu ya hali ya juu,mazingira na maelewano.timu ya mpira wa miguu kinachotakiwa,itafutwe sababu kwa nini soka la Tanzania aliendi mbele? hii ni kuangalia mazingira tunavyowandaa wachezaji,nadhani imefika wakati wa kutumia mazingira tofauti kijiografia katika kuandaa timu zetu kwa kipindi kirefu,hii ni pamoja kuendeleza vijana kisoka wakiwa shuleni kuanzia shule za msingi.Na serikali pia kuangalia kuondoa ushuru au kodi kwa vifaa vya michezo ili watoto maskini waweze kuvitumia kirahisi.

    ReplyDelete
  19. MndengerekoMarch 03, 2012

    Halafu sisi wabeba boksi tukikosoa viongozi wa kibongo inakuwa nongwa, tunaonekana wajivuni. Wakati ukweli unabaki pale pale kwamba viongozi wabongo wengi vichwa maji, na sisi tuliowapigia debe halikadhalika. Sasa ikiwa lengo tegemezi ni kuwa viongozi vijana ndio tegemeo, huyu Kabwe tutegemee nini kwake? Anashindwa na simple analysis kama hii, akijaaliwa kuongoza nchi itakywaje? Kiongozi wa hadhi yake si aropoke bali ashauri kiboreshwe nini kabla mechi ya marudiano ili ushindi uwezekane. However, all in all, this is typically CHADEMISATION, na ndio tulichoona straight baada uchaguzi, instead of regrouping it was chaos and violence. These people don't have a second more sensible thinking

    ReplyDelete
  20. Jamani tujitahidi kutumia zaidi weledi badala ya hisia.Zito kama mtanzania na mpenda michezo mwingine yoyote yule ana haki ya kutoa maoni juu ya mtazamo wake kulingana na mwenendo wa timu ya taifa.
    Ikiwa mtu kamfuata na kumuuliza au kujadiliana nae ana haki ya kueleza mtazamo wake. Au nyie mlitaka asijibu au asiongelee kabisa timu ya taifa kwa sababu tu yeye ni mbunge. Ingekuwa ameita vyombo vya habari ndio akatoa maoni hayo hapo kweli mngeweza kudadisi hilo.
    Tukae tujue hawa waandishi wa habari wanataka kuvutia wasomaji/wasikilizaji na na watapamba habari hata kama wamensikia tu mtu akiwa anabishana na wenzie baa alimradi ni maarufu.

    ReplyDelete
  21. Waanzie kuvunja TFF kwanza na mengine yatafuata...!

    ReplyDelete
  22. Sikubaliani na wale wanaosema eti kwamba tunahitaji mikakati ya nguvu katika kukuza mpira TZ. Si kweli kabisa kwa sababu; Africa tuna il kitu kinaitwa raw talent...mtu ana kipaji cha kucheza chandimu toka shuleni then mitaani. Cha kusikitisha unakuta wale wachezaji wa kweli hata kama wako Simba ama Yanga wanakaa benchi wale wachovu dizaini ya Nsajigwa, Ngassa, Lunyamila, Moh'd Hussein, na maozaoza mengine ndiyo wanapangwa, hivi mnategemea nini? Siku zote huwezi kupanda uozo ukategemea kuvuna mazuri. Tanzania mpira wetu unauliwa na Simba na Yanga kwani hizi klabu ndizo zinazoongoza kwa uchawi na wachezaji wao wote ni wachawi, hii I guarantee you people...! Katika hizi klabu uchawi unarithishwa toka viongozi mpaka wachezaji. Hebu tutafakari kidogo bila kuleta ubishi; hivi Ngassa ana mpira gani? Ama Lunyamila, Mohammed Hussein Mmachinga, Waswa, Zamoyoni Mogella, Tenga (rais wa TFF), na wachezaji wote wa sasa wa Taifa Stars, wana mpira gani? Kama nilivyosema, ondoeni ubishi wa kipuuzi tuzungumzie vipaji tu hapa! Mogella kwlei alikuwa mkali lakini si mchezaji wa kimataifa. Mpira wake ulikuwa wa utatanishi kiasi kwamba unaweza kuhisi alikuwa anatumia kitu fulani cha asili kwani hata talent alikuwa hana ila alikuwa ni mfungaji kama walivyokuwa Mmachinga na Lunya, na alivyo Ngassa hivi sasa. Lunya na Ngassa walitembea Ulaya, Marekani, mpaka na Marekani Kusin kusaka timu za kuchezea za kulipwa wapi? Lunya alichemsha mpaka venezuela wakati kule hawana hata historia ya mpira, mchezo wao wa taifa ni baseball (mpira wa magongo). Alijaribisha timu za daraja la pili akaonekana hafai ila TZ kwenye mizizi yake ni tishio na kama hapangwi mashabiki wako radhi kujiua. Ngassa, sijui niseme ama nisiseme? Huyu dogo ndiyo hafai kabisaaaaaaaaa! Hana talent yeyote zaidi ya kupiga danadana na kukimbia, ilibidi awe mwana riadha kwa spidi yake ila hafai kuwa mchezaji maana hana sifa zozote za uchezaji zaidi ya kukimbia. Sisemi zaidi ila najuwa mnajuwa kuwa alienda Marekani, na Uingereza kujaribishia bahati yake...kilichotokea niseme? Nimemtaja Tenga rais wa TFF kwa sababu hata kipindi kile niko kijana naifuatilia Pan African sikuona ujuzi wake. Tenga namfananisha na Nsajigwa, jamaa alikuwa kila sehemu kukaba watu lakini sidhani kama alikuwa anajuwa anafanya nini pale uwanjani. Na ndiyo maana hata ubovu wa hii Taifa Stars ya sasa yeye haoni kasoro anaona wako fiti kwa sababu Tenga hakuwa mchezaji bali msindikizaji. Msidhani kama nawadharau, lahasha ni ukweli ambao inabidi niuseme kwani kuficha maovu ni sawa na kujiua huku unajiona. Tukitaka mpira wetu uwe juu tuachane na uchawi tuwekeze kwenye vipaji. Mbona TZ mpira upo jamani? Hivi hamuendagi kuangalia menchi za mchangani? Kule mtakuta mpira wa uhakika wenye formations sio kubeza Simb na yanga tu kila kukicha wakati wanaua mpira wetu.

    ReplyDelete
  23. Hivi hawa wanaomsema Zitto kichwani hamnazo? Kwani kakosea nini kusema ukweli? Mimi mwenyewe nilienda uwanjani mbona nilitaka nirudishiwe pesa zangu. Cha kushangaza hata maelfu ya watu waliokuja pale wote walilalamika kwamba kiwango cha Stars ni finyu na wazo la ile timu kuvunjwa mbona sie sote pale uwanjani tulisema hivyo? Hawa wachezaji wa Stars kwa kweli si wachezaji ila wanalewa sifa bure, yaani hakuna hata mchezaji pale. Binafsi naona baada ya kuvunjwa hii timu wachukuliwe wachezaji wanaotoka mikoani ila si kwa Yanga na Simba. Nawakilisha, Stars ivunjwe. Thanks Kabwe!

    ReplyDelete
  24. Mimi sisemi chochote!

    ReplyDelete
  25. Kwa mtindo huu tutavunja timu kila mwaka mpaka karne ijayo hakutakuwa na mafanikio. Dawa ni kuandaa wachezaji wetu wakiwa wadogo na uratibu huo uwe endelevu la sivyo tutavunja timu sana hata kama tutachukua vijana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...