Home
Unlabelled
MSIMAMO JUU YA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Inasikitisha kuwa na madaktari lakini hawana busara
ReplyDeleteHapa mawili. Mawaziri husika hawaitendei Serikali haki. Kwa kiasi madai ama tuhuma za madaktari hawa zimesababisha hatua za kuwaweka kando Katibu Mkuu na Mganga Mkuu, mawazir nao pia ingepaswa wachukue hatua za kumwomba Rais wajiuzulu kutoa nafasi ya uchunguzi. Hiyo ndiyo maana ya utawala bora na uwajibikaji. Vinginevyo wanakuwa na ubinasi bila kujali maslahi ya Serikali na Rais.
ReplyDeletePili, madaktari nao wanavunja miiko ya viapo vyao vya kazi. Kuyaweka maisha ya wagonjwa wao rehani kwa madai yao ni kujifanya wanasiasa pia. Taifa letu lisiyape makundi haya mawili huruma yeyote ile. Rais amewaomba wafanye subira. Hatua ya mgomo haina msingi wakati huu.
Ninyi Madaktari angalieni maana tunaanza kuona lengo lenu sio maslahi tu bali mna chuki binanfsi baadhi yenu na viongozi wa wizara. Hebu tuambieni mkipata hayo maslahi mtaacha kwenza kwenye hosptali binafsi kama mlivyozoea? serikalini manafanya masaa machache sana. Rushwa mtaacha? Nadhani kuna haja ya kuwafuatilia hawa madaktari ipasavyo. Sisi tunalipwa hiyo mishahara mnayoidai lakini hatufanyi kazi kama ninyi. Tunamenyekeka kwelikweli. Hakuna ujinga wowote, kosa kidogo nje. malalamiko yoyote ya mgonjwa yanachunguzwa kikamilifu. msiuchezee huo uhuru mlionao.
ReplyDeleteLengo ni kuwafukuzisha kazi hao tajwa au kuboresha maslahi?
ReplyDeleteHey!..kumbe huu mzozo haujaisha tu.Rais Kikwete ingilia kati tafadhali.angalau wewe kwa sasa tuna imani kwako..siyo hao wasaidizi wako.
ReplyDeleteDavid V
SAFI SANA....HEKO,WATU WANAFANYA MADUDU HALAFU HAKUNA KUWAJIBISHWA...HII NDIO TUNATAKA SASA.NA VILE VILE MAFISADI WOTE WAWAJIBISHWE.
ReplyDeleteI think this is a unique opportunity for President Kikwete to prove his commitment in the well being of his citizens. He has enormous power on his hands in terms of executive orders and legislative controls. He can not continue to avoid the controversy at the price of patients souls. Its very un ethical and and it can trigger a lot of chaos in this state. My advise to the President is STOP PASSING THE BALL TO YOUR SUBORDINATES ,THEY WILL FAIL YOU. Be responsible and take actions. Its time to stop these usual politics of asking for subira while your neighbours are conducting funerals . Be strong and start acting now so you can be remembered for something great .
ReplyDeleteSasa basi madaktari wamwambie Rais ni nani wanamtaka awe waziri wa afya na naibu wake baada ya hawa wa sasa kujiuzulu. Maana madaktari wanataka kufanya kazi alizopewa Rais kwa mujibu wa katiba. Nawashauri madaktari wadai haki zao bila kuingilia kazi za Rais wa nchi. Kazi za kuteua mawaziri ni kazi ya Rais wa nchi zi madaktari.
ReplyDeletePointi kuu ya madaktari kuhusu mawaziri hawa ni kwamba wameshindwa kufanya nao kazi kwa hiyo hawana imani nao tena. Walipotosha ukweli mwingi na kumweleza uongo waziri mkuu. Ni rahisi kwa mkuu wa nchi kuwaondoa mawaziri hawa kwa sio lazima wawe mawaziri wa wizara ya afya, kuliko kuacha mgomo utokee na watazania wafe.
ReplyDeleteHakuna mtu wa kujiuzulu. Ni wizara gani isiyo na migogoro? mbona mawaziri bado wapo? kama ni hivyo, basi bora baraza lote la mawaziri livunjwe ili tuanze upya.
ReplyDeleteHawa madaktari wafukuzwe kazi tujue moja. Kila zama ina mikiki yake. Labda huu ndio mkiki mkubwa wa Rais Kikwete. Naamini raia wengi hatimaye watamuunga mkono Rais pale atakaposema sasa basi hatuna budi kukabiliana na watu wenye ubinafsi na wasiojali maisha ya wananchi wenzao. Mhali pengine wito wa udaktari ni kujitolea hata bile kulipwa ili kuokoa maisha. Kwanini vijana wetu hawa wamegeuza mwiko huu na kufanya elimu tunayoigharamia kuwa ni kuweka maslahi yao mbele kuliko ya raia wenzao? Heri wafukuzwe tujue moja kama taifa!
ReplyDeleteUkiangalia kwa makini pamoja na madakitari nao kutaka kuonyesha kuwa wana nguvu(Jambo ambalo siliafiki mana ni hatari), lakini serikali yetu imezidi kuingiza siasa kwenye masuala ambayo siasa haihitajiki hata kidogo.Madakitari wote wa Tanzania ambao ni asilimia kubwa ya watekelezaji wa sera za wizara ya afya wamesema waziri mponda hafai kufanya kazi nao kwa nini wasisikilizwe? sio mtu mmoja aliyekurupuka na kusema hamtaki waziri huyo.Serikali inatakiwa kuliangalia hilo, Hebu serikali onyesheni kuwa mnaweza kumuwajibisha mtumishi pale anaposhindwa kuwajibika.Mbona serikali hii jamani haina historia hiyo?? anzeni jamani, maana tumezoea kuunda tume,na tume na tume mpaka wananchi nawasahau mnafukia, sasa hili halifukiliki, ukifukia linafufuka!! Fanyeni jambo kidogo!
ReplyDeleteKweli hatuna Madaktari sikuhizi bali Wanasiasa wanaovaa makoti ya madaktari. Hata kama hao viongozi wanastahili kuwajibishwa hiyo ni sababu ya kugoma kweli?na kuwa tayari kuhatarisha maisha ya maelfu ya watanzania?? Nani amewaloga Madaktari wetu!
ReplyDeleteBasi na wafanyakazi wa sekta ya nishati nao wote wagome,maana wizara ile nayo ina madudu kibao. Tanesco hebu gomeni basi na nyie tukae kwenye giza kidogo. The motive of these doctors is malicious na wameweka personal feelings kuliko maslahi. Hata wananchi sasa watawashangaa. Hivi ni nani mshauri wenu madaktari,mbona maamuzi yenu yanakosa busara?
ReplyDeleteTatizo kubwa la Watanzania hasa mnaotoa maoni bado hamthamini haja ya kuwa na serikali inayojali maslahi ya umma. Acheni ushabiki, hao mawaziri pamoja na rais wao wanawajibika kiasi kikubwa kuhusiana na mgomo wa madaktari ambao mie binafsi nadhani ni kichocheo kikubwa cha uwajibikaji wa serikali.
ReplyDeleteHao viongozi wa wizara ya afya ambayo ni nyeti ni jukumu lao kila siku kuhakikisha kuwa madaktari na wafanyakazi wote wa sekta hiyo wanafanya kazi zao katika mazingira yenye standard ya karne ya 21. Mbona wao viongozi wa serikali wa juu wanaishi na kufanya kazi katika mazingira mazuri? kama mbunge anaendesha gari la fahari kwenda bungeni, kwanini Daktari asiwe na vitendea kazi vya kisasa na maslahi mazuri? Mazingira mabovu ya kazi na ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi na maslahi madogo yamewafanya madaktari kutumia muda mwingi kufanya kazi kwenye mahospitali ya watu binafsi kuongeza kipato chao.
Vifo hutokea pale muhimbili kwasababu ya mazingira mabaya kwa wagonjwa na ukosefu wa vitendea kazi. Fanyeni ziara hapo muhimbili ambayo inaitwa hospitali ya Taifa bila hata aibu mtayaona wenyewe!!!. Inazidiwa hata na hospitali za County za nchi za wenye uongozi unaojali wananchi wao. WAKULAUMU HAPA SIO MADAKTARI BALI NI VIONGOZI WETU AMBAO NI WABINAFSI KIASI KWAMBA HATA HAWAONI KAMA NI WAJIBU WAO KUENDELEZA NCHI. WaTanzania bado mnaimani kuwa matatizo kama haya ni kawaida.
Wasi wasi yangu kubwa ni kwamba mnao walaumu madaktari mnauhusiano na hao wanaojiita viongozi au hamjali maslahi ya watanzania wengi ambao hawana sauti.
TUWAUNGE MKONO HAWA MADAKTARI ILI WAPATE NGUVU YA KUBADILISHA WIZARA HII MOJA YA AFYA, ZINGINE ZITAFUATA. UMAOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU.
Ni mie mwananchi
Makongoro Wassira
Ndugu Makongoro, mimi siwaungi mkono madaktari n'go kwenye mgomo. Hizo changamoto zote ulizozisema nakubaliana nazo asilimia miamoja. Hizo zipo kitambo, na si katika sekta ya afya pekee ila je mgomo ndio utaleta ahueni pale muhimbili? Au roho zitakazopotea kipindi madaktari wamegoma ndio itakuwa sacrifice ya kuboresha mazingira ya huduma za afya? Hivi hakuna jinsi nyingine ya kufikisha ujumbe kwa serikali bila kuathiri maisha ya watanzania?
ReplyDeleteNarudia tena, mabadiliko katika sekta ya afya na sekta nyinginezo nayataka sana ila madaktari siwaungi mkono kwenye mgomo.
Ni mie mwananci mwenzako
Kwahiyo ndugu Makongoro upo tayari kumpoteza ndugu yako kwa kukosa huduma hospitali ili kuleta mabadiliko katika wizara ya afya na wizara nyingine?
ReplyDeleteSERIKARI IFANYE MAAMUZI MAGUMU
ReplyDeleteMADAKTARI WAFUKUZWE TUANZE MOJA
Waziri wa Afya na Naibu walitakiwa Wajiuzulu kwa busara wao wenyewe kabla ya kuwajibishwa!
ReplyDeleteWalitakiwa walewe Bosi wao Waziri Mkuu aliongea nini ktk Kikao na MADAKITARI.
Unapoharibu unatakiwa ujitoe mwenyewe kwa busara na sio mpaka Ufukuzwe!
TATIZO LA MADAKTARI NI KUWAFUKUZA KAZI WAZIRI NA NAIBU WAKE, JAMANI HILO NDIO SABABU YA KUONA NDUGU ZTEU WANAPOTEZA MAISHA , JE ATAKAYETEULIWA MSIPOMPENDA? KWA KUWA SEKTA YENU NI MUHIMU KWA AJLI YA AFYA ZEUT MMEONA MCHEZEE MAISHA YETU? KWELI MNA WITO? JE WAGI=ONJWA WATAKUWA NA IMANI KWENU?
ReplyDelete