MWANAFUNZI wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya St. Anthony Mbagala, mkoani Dar es Salaam, Franco Donald Kisongo (18), aliyepotea jijini humo Machi 18 mwaka huu, amepatikana Mbinga mkoani Ruvuma.
Kijana huyo aliyekuwa mgeni jijini Dar es Salaam alipotea siku nne tu tangu ajiunge na shule hiyo kuanza masomo ya kidato cha tano. Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia ya Franco, kijana huyo alifika kwao Mbinga mkoani Ruvuma Machi 23, akiwa peke yake.
Inadaiwa kuwa, baada ya kufika kwao, alisema kuwa hajui alifikaje huko akiwa ametumia takribani siku sita njiani kutoka Dar es Salaam. Machi 18 asubuhi, Franco aliwaaga wanafunzi wenzake kuwa alikuwa anakwenda kwa shangazi yake, Adela Kisongo, Kariakoo jijini humo, hakufika huko, pia hakurudi shule, na haikufahamika alikuwa amekwenda wapi.
Walimu na walezi wa kijana huyo, walitoa taarifa Polisi, na wakatumia RB namba 3343/2012 ya kituo cha Msimbazi kumtafuta. Wazazi na wanafamilia ya Franco wanawashukuru wote ambao kwa namna moja au nyingine walishiriki kumtafuta kijana huyo, aksanteni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ''Sijui nilifika fika vipi Mbinga''

    Sasa haya si ndio Maajabu ya MUSSA?

    Huyu Dogo inaonekana kwa kauli yake hiyo hapo juu anataka kukwepa RB iliyoandaliwa isimwangukie na kuburuzwa ktk Mikono ya Sheria !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...