Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Chuo cha Polisi mjini Moshi leo tayari kwa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Shamsi Vuai Nahodha na kushoto kwake ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Saidi Mwema.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akizindua mojawapo ya vitabu vya muongozo wa Jeshi la Polisi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Chuo cha Polisi mjini Moshi leo.Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Shamsi Vuai Nahodha wa kulia kwa Rais ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Saidi Mwema akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh. Leonidas Gama.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Chuo cha Polisi mjini Moshi leo.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Chuo cha Polisi uliofunguliwa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Moshi leo.PICHA NA IKULU
Hawa polisi waingezewe mishahara na marupurupu ili waache kupokea rushwa....
ReplyDeleteMdau wa kwanza ni kweli kabisa,
ReplyDeleteJamani Baadaya ya Wabunge, Madakitari na wengineo kuongezewa maslahi hebu tuwageukie akina Ras Makunja (Askari) nao !
Masikini wee Polisi wana njaa sana na ndio maana wanapoza makali kwa kuomba chohcote Mfano nimesikia Rufiji Askari wa Usalama Barabarani wanadai ruhswa hadi za kuku, nyama na mikate kwa madereva wa mabasi madogo Hiace!