Ile sherehe kabambe ya wanafunzi wote waliomaliza shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim miaka ya nyuma, imeahirishwa hadi Jumamosi ya Juni 30, 2012 katika ukumbi utakaotangazwa baadaye. Mabadiliko haya ni kuitikia maombi na kutoa nafasi kwa wenzetu wengi walio mikoani na nje ya nchi ili waweze kushiriki kikamilifu katika sherehe hii hiyo.

Lengo kuu la mkusanyiko huo ni kukutana, kufahamiana, kujua nani yuko wapi na anafanya nini ili hatimaye tuweze kuunda mtandao na kuendeleza mema yaliyopo.

Kamati maalum ya muda ya kuratibu mkusanyiko huo pamoja na kuangalia taratibu nyingine imeshaundwa. Vikao vya wadau vyenye kulenga kufahamiana, kuandikishana majina ya wanaopenda kushiriki na kupanga mikakati ya kufanikisha tukio hili, inafanyika kila Ijumaa kuanzia saa 11:00 hadi saa 1:00 jioni, katika ukumbi wa New Happy Hotel - juu ghorofani, iliyopo mtaa wa Ungoni na Kipande, jirani na zamani mgahawa wa Chef's Pride, maeneo ya Lumumba, Kariakoo hapa jijini Dar Es Salaam. Karibuni sana tukumbukane na tufahamieni zaidi.

Ukisikia au kusoma taarifa hii unaombwa uwaarifu na wengine.

Kwa mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana na kamati ya muda kupitia:
Bi. Mambo Tambaza (0713236110) Mwenyekiti
Bw. Abou Liongo (0762298087) Mjumbe
Cast Vumi 0756 232821, 0713 232821(Mjumbe)
Abbas Mbonga 0767606970 (Mjumbe)
Barua pepe: kinondonireunion@gmail.com

USIKOSE NAFASI YA PEKEE YA KUKUMBUKANA NA KUFAHAMIANA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Wazo zuri mno na limetulia, jamani Juma Mkele (Magereza1) Fatuma Muya, Hoya (Nyau) wako wapi!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2012

    kaka umenikumbusha mbali sana siyo HOYA pekee jee MAKAKALA.displine master MR SHARIF WAKO WAPI?MAANA HUWEZI KUITAJA KINOSESCO BILA HAO WAHESHIMIWA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2012

    kwa wale waliomaliza mwaka 1980 mtakao jariwa kufika msisahau kututumia picha za ukumbusho.Barry white

    ReplyDelete
  4. Hawa YakubJuly 01, 2012

    Hello Jamani. Asantani sana kwa tafrija hiyo ya kukumbushana enzi ya 1978 I was a.student in those days Ms Usha. Mr Malik.Mr kambrudeen .Mrs Chaya I missed u all and thank you all for organizing the reunion. ..
    ..Though I missed it but I pray for everybody from Kinondoni Muslim High Secondary school. My name is Hawa Yakub mail add malytz1@gmail.com

    ReplyDelete
  5. Hawa YakubJuly 01, 2012

    Miss mihogo maandazi maharage from mzee Shoka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...