Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, Bi. Gladness Mkamba akionyeshwa malikia katika mzinga wa nyuki wasiouma na Afisa Nyuki, Bw. Chescho Japhety (aliyeshika bisibisi) huku Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mtanzania, Bw. Kambi Mbwana akishuhudia tukio hilo walipotembelea maeneo ya ufugaji nyuki wilayani Manyoni, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, Bi. Gladness Mkamba akiwaelekeza jinsi ya kutoa asali kwenye sega kwa mwaandishi wa habari wa Gazeti la Mtanzania, Bw. Kambi Mbwana (mwenye fulana) na Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima, Bi. Hellen Ngoromera ikiwa ni sehemu ya ziara iliyolenga kuwajengea uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu shughuli za ufugaji nyuki nchini. Katika Ziara hiyo waandishi wa vyombo mbalimbali walipata fursa ya kutembelea vikundi vya ufugaji nyuki katika Wilaya ya Manyoni na Singida mkoani Singida, mwishoni mwa wiki iliyopita.
HAWA SI MABWANA NYUKI BALI NI WAANDISHI WA HABARI WAKIWA WAMEVAA VIFAA MAALUM KWAAJILI YA KURINA ASALI, KUTOKA KUSHOTO NI MWANDISHI WA STAR TV, STEVEN CHEGERE, MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MTANZANIA, BW. KAMBI MBWANA, MWANISHI WA CHANNEL 10,BW. KIBWANA DACHI, NA MWANDISHI WA GAZETI LA UHURU, BW. MOHAMED ISSA WAKIWA TAYARI KWENDA KUJIFUNZA JINSI YA KURINA ASALI KATIKA ZIARA HIYO.
BAADA YA KAZI NGUMU WAANDISHI WALIJIPOZA NA ASALI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Asali imekuwa ni bei juu siku hizi na wauzaji wengi wanachanganya na sukari. Hivyo asali nyingi zinazouzwa ni bandia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...