WAZIRI wa Ujenzi Dokta John Magufuli ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanamwandikia majina ya wakurugenzi na watendaji wanaotumia fedha za barabara katika kulipana posho na wale wanaokaa nazo bila kuzifanyia kazi ili apeleke kwa Rais na kuhakikisha wanafukuzwa kazi ikiwemo chato na longido.
Magufuli alitoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam katika ufunguzi wa kituo cha mabasi Mbezi mwisho wilaya ya kinondoni ambapo alisema kuwa serikali imekuwa ikitenga fedha kwa halmashauri lakini watendaji wake wamekuwa wakizitumia kwa shuguli nyingine.
Aliiagiza Tanroad akisema “Nyie Tanroads nawapa siku tano muhakikishe hakuna gereji bubu yoyote ,nyumba wala wafanyabiashara walioingia katika hifadhi za barabara wanaondoka hata kama bendera ya CCM imewekwa barabarani ondoeni lazima kufika mahali sheria ifanyiwe kazi lasivyo msongamano hautaisha na katika hili swala siasa liwekwe pembeni” alisema Magufuli.
Magufuli pia alitoa agizo la kuhakikisha ujenzi wa choo,uzio na ofisi katika kituo hicho unamalizika mapema na kuipa Tanroads mamlaka ya kukisimamia kituo hicho ikiwemo daladala zote kutolipishwa.
Aidha alitumia fursa hiyo kupandisha hadhi baadhi ya barabara kujengwa kiwango cha lami ikiwemo ya barabara ya Malamba mawili mpaka tabata na ya mbezi mpaka Tegeta.
Aidha aliwataka wananchi kuhakikisha wanatunza kituo cha mbezi na vinginevyo ikiwa ni pamoja na kutokutupa uchafu katika mitaro na kutovamia hifadhi za barabara kwa kujifanya hawajui sheria kwani huo si utetezi.
Kikwete angekuwa na mawaziri angalao 5 wa namna ya Magufuli Nchi hii ingenyooka.
ReplyDeleteTatizo baraza la mawaziri ni la 'kiushikaji' sana na hawatimizi wajibu wao kumsaidia raisi badale yake ni kila mmoja 'anachumia tumbo'
Watu wenye roho mbya kwa kisingizio cha kusimamia sheria inaelekea wanapendwa sana. Je kama nyumba inayobomolewa ni yako ungeshangilia?
ReplyDeleteAcheni ujinga. Pimeni mambo kwa makini. sheria ibadilishwe iwe kama serikali inaona mtuanajenga na haikuchukua hatua muda wote basi haina haki ya kubomoa baada ya ujenzi kukamilika. waliokuwa na wajibu huo nao ni lazima wachukuliwe hatua za kisheria. Kwa nini watumishi wa serikali waliotakiwa kusimamia sheria hiyo na wakazembea hawajachukuliwa sheria? Huu undumila kuwili utaisha lini?
Kwa kweli Magufuli nakufagilia sana, kila sekta unaimudu, Ingekuwa uwezo wangu URAIS 2015 NINGEKUPA BABA.. TANZANIA INGENYOOKA.. LONGOLONGO INGEKUWA STORY.
ReplyDeleteYou go brother!
ReplyDeleteChukua fomu kamanda 2015
ReplyDeleteDavid V
usipogombea wewe uraisi 2015 sitapiga tena milele kura kwann na wewe tusikujaribu tukaona yakwako mbna tulimuamin uyu tukamchagua na sasa bei kla ktu khari na mambo yanaenda kombo si kma tulivyozania gombea magufuri na wewe sisi tpo tutakuchagua
ReplyDeleteWewe unayesema roho mbaya kwa kisingizio cha sheria unatakiwa utembee nchi za wengine uone sheria zinavyofanya kazi, Inaonekana ni jinsi gani ulivyo ignorance, Kama unajua eneo hAliruhusu kujengwa lakini unajenga kwa kusubiri ati serikali ikuambie hapo haparuhusu kujengwa basi utakuwa unabomolewa kila kukicha, Kwanini usifuate sheria za ardhi mara unapopata ardhi mahali popote, WATANZANIA TUNATAKIWA TUAMKE, MAGUFULI KAZA BUTI.. URAIS 2015 CHUKUA FORM. KILA KONA PATANYOOKA..
ReplyDeleteMAGUFULI NI KWA SABABU TU SISI WATANZANIA WABEBA BOX TUKO MBALI NA UPEO HUO LAKINI HONGERA SANA KWA KUKAZA BOOT BILA WEWE NAONA MAWAZIRI WOTE KIGUGUMIZI, WALA USIOGOPE KAMA UTAKUFA KWA AJILI YA HAKI YA MWANACHI MTANZANIA ROHO YAKO ITABEBWA KIKAMILIFU NA MALAIKA WOTE WALIONA NEEMA, UOGA UMEZIDI, MAFISADI WANAKULA TU PESA ZA WATU MASIKINI AMBAO NDIO WANAHITAJI ZAIDI MALEZI MAZURI NA PESA HIO. SIO KILA KUKICHA WANAJENGA MAJUMBA MBEZI NA KUNUNUA KILA KONA NZURI YA NCHI, HONGERA SISI WATANZANIA TUNAOISHI UGHAIBUNI TUNAKUPA 5 UP! UZI UWE HUO HUO NA KAMA UNAUWEZO WAIBUE MAFISADI WOTE WEWE NDIO MKOMBOZI WETU. TANZANIA HAINA DAWA, HAINA SHULE WALA MADAWATI , WANAFUNZI WANAKAA CHINI KWENYE MAWE MBONA NYIE MLISOMA KATIKA MADARASA? NDIO MAANA MKAPATA ELIMU. HIVI SASA MADARASA VIJIJINI NI AIBU TUPU ETI NA WAZIRI WA ELIMU TUNAO LAKINI HAMNA LOLOTE LIFANYWALO PESA ZOTE MIFUKUNI MWAO. UMEME HATUNA , MAJI MGOGORO. KWELI HATUWEZI KUFIKA HUKO TUNAKOENDA. WAAMBIE HAO WENZAKO: TAIFA LIJALO LITAKUWA SILO NI UOZO MTUPU, KWANI HAKUNA NGUZO ZINAZOJENGWA KIUFASAHA NA WAO HAO VIONGOZI WATAKUWA NI WAZEE TAYARI AMBAO WANAHITAJI MSAADA KUTOKA KIZAZI HIKI SASA HATA HIZO PESA ZAO WANAZOJILIMBILIKIZIA ZITAKUA NA FAIDA GANI? KAMA WAO HAWAKUJENGA MISINGI MIZURI YA NCHI WATABEBWA NA PILOT GANI WA NDEGE KUTOKA VIJIJINI KWAO KWENDA MAHOSPITALINI WAKATI HAWAKUACHAA BARBARA ZINAZOJULIKANA?
ReplyDeleteTUKO NYUMA YAKO KWA HALI NA MALI USICHOKE KUTETEA HAKI YA WATANZANIA WENZAKO AMBAO UNAWAJALI KWA MOYO WAKO WOTE
Hongera Sana wote mliochangia maoni kwa kumpongeza huyu Kiongozi ambae anaonekana anawajibika kiasi chake.
ReplyDeleteBado kuna watu wanapenda sana kuoneana huruma huku wanavunja sheria, hii imesababisha Dar Es Salaam kujengwa ovyo ovyo bila utaratibu. Kumbukeni "kutokujua sheria haikupi haki ya kuvunja sheria".
Makongoro Wassira