Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Mbinga mjini,SSP Geofrey Ngu'hubi (kushoto) akiwasikiliza wafanya biashara ya kuuza pombe za kienyeji katika baa ya manzese wilayani mbinga baada ya kuwakamata wakifanya biashara hiyo saa za kazi huku sheria ikiwataka kufanya biashara yao baada ya saa za kazi
Baadhi ya wazee waliokutwa wakinywa pombe katika baa maarufu ya manzese wilayani mbinga,wakimsikiliza mkuu wa kituo cha polisi mbinga,SSP Geofrey Ngu'hubi (kushoto) baada ya kukamatwa na jeshi la polisi wakinywa pombe saa za kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. ANGALIA HUYU MKUU WA KITUO ANAVOONGEA NA HAWA WAZEE KWA HESHIMA>. KAMA HALI INGEKUA INAFANYIKA SEHEMU ZOTE WALLAHI KUSINGEKUA NA CHUKI KATI YA POLISI NA WANANCHI.

    ReplyDelete
  2. Swali la kizushi

    Je inaruhusiwa kunywa pombe bar saa za kazi?

    au ni kunywa pombe za kienyeji saa za kazi ndio kosa?

    mbona hawakamati wanywaji pombe za viwandani kwenye mabar ?


    pia kuna watu wengine , wanafanya kazi usiku, mchana ni muda wa mapumziko, hawa wanafikiriwajwe?


    mbeba box wa Dubai

    ReplyDelete
  3. Safi sana! Watanzania wenzangu hebu tujifunze. Ulevi si sifa wala ushujaa. Hasara za ulevi: (1)Matatizo ya kiafya kimwili na kisaikolojia: k.m. cirhosiss ya ini, kisukari, matatizo ya ventriculars zote za moyo, uharibifu wa mucuos lining ya ubongo (na kuathiri kumbukumbu), kuongeza uwezekano wa saratani/cancer, n.k. na kuongezao uwezekano wa mtu kupata UKIMWI (tazama ripoti za WHO kuhusu uhusiano kati ya UKIMWI na ulevi. ((2) Kutupa pesa ovyo badala ya kuzitumia kimaendeleo na kwa maslahi ya familia. (3) Matatizo ya kimahusiano ya kijamii (heshima, n.k.).Hapa Tanzania, ulevi+uvivu=economic and social backwardness. Sisi kama taifa tutaendelea kubaki nyuma as long as vichwa vyetu vinatawaliwa na ulevi na uvivu. Tutafakari na tujifunze ndugu zangu.

    ReplyDelete
  4. Hata pombe ina muda wao wa kunywa kwa wazee kama hao, what about shift workers on a day off,wake up Mbinga. Mko century gani huko. Nendeni ulaya mapombo yanauzwa 24/7/365. Huyo polisi hana priorities?

    ReplyDelete
  5. Suala hili linategema mtu anafanya kazi gani na saa ngapi. Mfanyakazi wa zamu ya usiku atakunywa muda gani?

    ReplyDelete
  6. Jumamosi na Jumapili nilikuwa kazini kesho Jumanne niko off. Ukinikuta nakunywa saa saba mchana usinikamate kwa sababu nitakuwa niko off kazini wakati wengine walikuwa majumbani Jumamosi na Jumapili wakati mimi nipo kazini.

    Halafu naomba nimkumbushe afande asisahau kupita majumbani kwa siyo wote wanaokunywa wanaenda vilabuni wengine wananywea nyumbani.

    Kuna upumbavu mwingi sana ndani ya jamii yetu.

    Mdau, Helsinki, Finland.

    ReplyDelete
  7. Aise mkuu wa polisi pekee asiye na kitambi, nimeipenda

    ReplyDelete
  8. ama kweli tanzania tambarare!!! mnyonge hata hana haki ya kunywa pombe wakati anaotaka? sasa kama hawana kazi, na wamechoka kutafuta kazi kwa siku hiyo bado wasubiri hadi waheshimiwa watoke makazini ndio wakakate kiu?

    Na polisi nao wameshinda na vituko vyao, badala ya kutumia nguvu zao na uzoefu wao kukamata wala mali za umma, waharibifu wa mali za umma na majambazi yaliojaa tele nchini wanakwenda kuwakamata waliokuwa hawana na hatia ila kunywa pombe!

    ReplyDelete
  9. Nyie mlio nje ya TZ mbaki na mambo ya huko mlipokimbilia tuacheni tulio huku nyumbani tuendeleze mambo vile tuonavyo inafaa.

    Sio kila kitu mlichoiga nyie na sie tuige. Hata kama upo Off siku ya kazi (kwa wengine) si usubiri mpaka jua lizame unywe na wenzio. ninavyojua mimi mtu akiwa Off anakuwa off siku nzima, so anaweza akafanya shughuli nyingine mchana ikiwemo kupumzika kisha baadae akaungana na wenzake. hii inakaa vyema pia

    Pongezi kwa mkuu wa kituo

    Tumezidi kuendekeza ujinga na inakera kuona ujinga unatetewa pasipo na ulazima. kama Upo off na unataka kunywa pombe mchana nywea nyumbani kwako. huoni aibu kunywa pombe peke yako jua kali.


    Mume wangu

    ReplyDelete
  10. HONGERA !

    Kamanda Afande SSP Geofrey Ng'umbi kwa kazi nzuri!

    Hatuwezi kuwa na maendeleo kwa kunywa pombe muda wa kazi iwe Pombe za Viwandani ktk (Bar) na za Kienyeji (Vilabuni).

    DAIMA TANZANIA HAIWEZI KUWA TAIFA LA WALEVI KAMA AFRIKA KUSINI NA ZAMBIA!

    ReplyDelete
  11. Hamna kifungu chochote cha sheria Tanzania kinachokataza (1) kunya pombe (2) kuuza pombe wakati wa kazi. Labda hapa wamekamatwa kwa kuuza pombe haramu ndio itakuwa kosa au wanauza bila leseni.

    ReplyDelete
  12. @Mon Mar 05, 04:23:00 PM 2012

    1.Kuishi nje hakuninyimi haki yangu kuzungumzia ustawi wa nchi yangu.

    2. Kuishi nje hakumaanishi kwamba umekimbia nchi yako. Umepata kusoma katiba ya Tanzania? Kama hujaisoma kaisome kwani imeweka wazi uhuru wa Mtanzania kwenda popote. Ndiyo maana kuna meli, ndege, na magari yanayoleta na kuchukua Watanzania kwenye sehemu mbali mbali duniani. Na Idara ya Uhamiaji inatekeleza hilo kwa kuwapatia Watanzania pasipoti.

    3. Saa za kazi ni zipi?

    4. Kila mtu ana uhuru wa kufanya lolote ili mradi asivunje sheria. Unaweza kuniambia kifungu kipi cha sheria walichokivunja?

    5. Tafadhali pita kwenye mahoteli makubwa au hata kwenye mabaa uone pombe zinauzwa na zinanywewa saa ngapi na siku gani.

    6. "..tuacheni tulio huku nyumbani tuendeleze mambo vile tuonavyo inafaa.." Nyumbani tumewaacha wazee wetu, ndugu, jamaa, marafiki, na Watanzania wenzetu na sisi tunaendelea kuwa Watanzania na sehemu ya jamii ya Tanzania. Kwa hiyo yasiyofaa hayafai hata tukiwa nje ya nyumbani.

    Kwa kumalizia tu. Hili jambo limenikumbusha wakati nasoma shule ya msingi Kisutu. Siku moja niliwaona pale Mtaa wa Mkwepu mgambo wanawakimbiza "wasio na kazi". Nilipoangalia maghorofani nikawaona Wahindi wamesimama vibarazani wanatazama. Nikamwambia rafiki yangu "..Wale kule maghorofani nao hawana kazi mgambo waende kuwakamata.." Rafiki yangu akacheka sana tena sana. Baadaye akawaita wale mgambo akawaambia "..Wengine wale kule juu saa za kazi wao wapo majumbani kawakamateni!.." Mmoja wa wale mgambo akamjibu kwa kumtukania mama yake na kumwambia "..N'takunasa vibao watu tupo kazini wewe unatukejeri.." Tukakimbia. Nadhani wale mgambo waliupata ujumbe.

    Mdau, Helsinki, Finland.

    ReplyDelete
  13. Mimi naona ndio vizuri wazidi kunywa, kwani pombe ni sehemu inayotuletea pato kubwa katika nchi yetu. Waacheni wanywe!!! maisha yenyewe ni stress tupu tu

    ReplyDelete
  14. Mdau wa Helsinki pamoja na analysis yako nzuri in a way, naomba nikukumbushe kwa ufupi kwamba, vifungu vya sheria kwenye katiba mama hutafsiriwa pindi vinapokuja kwenye utekelezaji katika grassroot level. Na kwamba vikitafsiriwa hupatikana kanuni na taratibu za kiuendeshaji, iwe kwenye kampuni, taasisi au hata katika jamii. Tafsiri hizi hutofautiana kulingana na mahali, wakati na mahitaji. Hivyo sishangai utaratibu wa unywaji wa pombe waliojiwekea mbinga ukatofautiana na wa DSM, Arusha na sehemu zingine. Swali la msingi ni je Afande natekeleza utaratibu waliojiwekea!?! Kama ndivyo basi anafanya vizuri, na hata kwa muonekano wa nje anaonekana anatekeleza kazi yake kwa nidhamu na heshima, jambo ambalo kimsingi linahitaji kupongezwa.

    Eddy
    Vancouver.

    ReplyDelete
  15. Hapa afande anafanya kazi yake lakini hakuna sheria iliyovunjwa. Huwezi kukataza pombe kuuzwa wala kunywewa. Tungependa kujua sheria gani imetumiwa hapa kuwakamata watu hawa.

    Uchumi wa Tanzania unategemea uuzaji wa pombe, simu za mikono, utalii na madini. Angalia milioni ngapi makampuni haya yanatoa kila siku kwa jamii mbali ya kulipa kodi na kuwapa kazi Watanzania. Wananchi wengi hawana uwezo au wanakwepa kodi.

    Wakati wa maofisa wa serikali wa kujifanya mama zetu an baba zetu umekwisha. Tanzania ni huru sasa na kama watu wanataka kunywa pombe saa mbili asubuhi, waachieni, ninyi pokeeni kodi yenu. Hii ndio demokrasia, tumeitaka wenyewe.

    ReplyDelete
  16. HUYO MDAU ANAYESEMA TULIOKO NJE YA NCHI TUSILETE TABIA ZA UKU KWA TANZANIA MAMBO MANGAPI MMEIGA HAPO SIWEZI KUYATAJA UNAJUA MWENYEWE! NA BAYA SANA KILA HOTEL ZENU HAPO MMEWEKA BEI KWA DOLLAR ,SHILLINGI IMEENDA WAPI BADILISHA HILO KWANZA NDIO UJIVUNIE UTANZANIA .

    ReplyDelete
  17. hii inanikumbusha enzi za nyerere ambapo akija mkoani basi huduma zote zinasimamishwa!!!now we see how primitive this was,ninacho taka sema ni kwamba there is better solution than that,viongozi acheni kula kodi za hao wavuja jasho without finding better solutions for their problems.

    ReplyDelete
  18. nataka kumjibu mdau hapo juu kuhusu sheria ya pombe:
    kwa uelewa wangu una sheria tanzania inayosimamia utoaji vibali na musuala mengine yanyohusu pombe inaitwa the Intoxicating Liquors Act,Chapter 77 Revised edition 2002 (unless imekuwa repealed baada ya mwaka 2000)
    katika sheria hiyo pamoja na mambo mengine inamlinda mtoto wa chini ya miaka 16 kuwa eneo lla uuzwaji pombe au kutumwa na inatambua pombe za aina mbili na kutoa tafsiri yani local liquor (inayojumuisha ulanzi,pombe zinazotokana na asali n.k) na intoxicating liquor (yaani beer,wine ,cider n.k).

    lakini cha kushangaza sheria hii imetoa muda maalum wa kunywa local liquor na waziri mwenye dhamana anweza kuongeza muda wa kukaa maeneo hayo na kunywa lakini as for the intoxicating liquor ambayo inauzwa kwenye hotels via hotel licences sheria inaruhusu kuuzwa muda wote!

    ukiangalia sheria hii unaona inawabana watumiaji wa pombe za kienyeji tuuu!! very discrimanatory ., it needs ammendments (that's if kama bado ni operational) na nina shaka kama watanzania wengi wanajua kama kuna sheria hii.

    Masiwo.

    ReplyDelete
  19. since tumeamua kuwa Capitalist society inayofuata mkondo wa soko huria nadhani ni kinyume cha ubepari kuanza kuingilia taratibu za kibiashara eti kuwe na muda maalum wa kuuza na kunywa pombe. My fellow country men, we can not have it both ways..hatuwezi ku practice ujima kwa ku enforce hizi sheria za nini au kipi kiuzwe saa ngapi na nani wakati tunakumbatia mihimili ya kibepari..NEVER.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...