Rais wa Riadha Tanzania (RT), Francis John (kati) akizungumza wakati wa utambulisho wa mbio za Tabora Marathon. Wengine ni waratibu wa mbio hizo ambazo zimekuwa gumzo kubwa mjini Tabora

KAMATI ya mbio za Tabora Marathon 2012, leo inatarajiwa kuanika zawadi za washindi wa mbio hizo za kwanza kihistoria kufanyika mkoani humo.
Mbio za Tabora Marathon 2012 zinatarajiwa kurindima mjini Tabora Machi 10 na kushirikisha wakimbiaji kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Magharibi.
Kwa mujibu wa Mshauri wa Ufundi wa Tabora Marathon, Tullo Chambo, leo watafanya jukumu hilo baada ya kufanikiwa kukamilisha maandalizi mbalimbali, ikiwamo wadhamini.
Chambo alisema, licha ya ugumu wa upatikanaji wa wadhamini, lakini wanawashukuru waliojitokeza kufanikisha mbio hizo, ambazo ni chachu ya kuhamasisha mchezo huo na kuibua vipaji.
“Kimsingi hadi kufikia hatua hii, tumehangaika usiku na mchana na ninawashukuru wapenda michezo wote walionyesha mapenzi mema na mchezo huu na Mkoa wa Tabora kwa ujumla, kwa kuweza kufanikisha kufanyika kwa mashindano haya ya kipekee katika historia ya mchezo wa riadha mkoani Tabora na Kanda ya Magharibi kwa ujumla,” alisema Chambo na kuongeza kuwa;
Leo tutawaanika wote waliofanikisha mbio hizi katika mazingira magumu, pamoja na zawadi ambazo washindi watazawadiwa katika mbio hizo.
Pia aliwapongeza viongozi wa serikali mkoani Tabora, chini ya RC, Fatma Mwasa, na viongozi wa Chama cha Riadha Mkoa wa Tabora, kwa ushirikiano wao uliofanikisha kufikia hatua hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni hatua nzuri kabisa katika kuuweka kwenye spotlight mkoa wa Tabora ambao kila siku unazidi kupoteza ushawishi wake katika maendeleo ya nchi hii... nawapongeza sana waandaaji na ninawaombea kila la kheri muweze kufanikiwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...