Taasisi ya Alice Foundation yenye makazi yao eneo la Sinza jijini Dar es salaam siku ya Muungano Day iliandaa hafla kwa watoto waishio katika mazingira magumu waishio katika kata ya Ubungo ambapo pia iliwakutanisha watoto hao na wengine waliopo shuleni.


Akizungumza na Elimubora Mkurugenzi wa Alice Foundation alisema kuwa hafla hiyo inalenga kuwaweka pamoja watoto waishio katika mazingira magumu kuwafariji na kuwapati ushauri nasaha.



Alisema kuwa watoto 400 walishiriki hafla hiyo iliyoshirikisha michezo mbalimbali kama vile kuvuta kamba, mbio za mayai katika kijiko, kunywa soda, kupokezana vijiti, kukimbia na magunia.



Alisema kuwa watoto walifurahia tukio hilo na alisisitiza kuwa litakuwa likifanyika mara kwa mara.



Taasisi hiyo ya Alice inajishughulisha pia na masuala ya utunzaji wa mazingira, uwezeshaji wa akina mama, haki za wanawake, kusaidia watoto waishio mazingira magumu na  masuala ya Mkukuta.

 Mwanzo wa mbio za mayai
 Shindano la kunywa soda
Shindano la kuvuta kamba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ni jambo zuri ila nshauri ni hatari sana kunywa soda kwa haraka kama hivyo waweza hata kupoteza maisha ikikupalia.waangalie other games rather than that.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2012

    asante sana kwa wote mlioshiriki katika maandalizi ya shughuli hii. ''together we can do this''

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...