Bank za kiIslam ni mipangilio mbali mbali na tofauti tofauti ya kibenki kama vile kuhifadhi pesa, kuchukua pesa, kusafirisha pesa kutoka bank kwenda bank nyengine na kutoka nchi moja kwenda nchi nyengine , kufanya biashara kati ya mtu na mtu kwa msaada wa bank, kufanya biashara kati ya mtu kwa kushirikiana na bank, kuuza bima za kiislam, kutoa mikopo kwa njia za kiislam, Kuuza na kununua hisa kwa utaratibu wa kiislam na mengine mengi. Ni vyema tukakumbushana kwamba bank za kiislam zinatoa huduma kwa waIslam, wasiokua waIslam na hata wale wasiokua na dini yoyote.
Uhakika ni kwamba bank za kiislam zinakua kwa kasi sana, bado kuna wataalam wachache ktk fani hiyo na hakuna sehemu nyingi ambazo watu wanaozungumza Kiswahili wanaweza kupata maelezo mbalimbali kwa lugha yao, tumeona upo umuhimu wa kuanzisha blog maalum ambayo wataweza kupata huduma hizo Kwa kutumia lugha tatu kiSwahili, KiIngereza na kiarabu.
Ni muhimu kukumbushana kwamba mafanikio ya uchumi wowote yanategemea uwiano kati ya maadili na mahitaji ya binadamu, mshikamano wa vitu viwili hivyo ndio ambavyo vinajenga misingi ya uchumi wa kiislam. Kuna wachumi wanaoona kwamba maadili ya uchumi wa kiIslam yanawafanya washirika kugawana hasara na faida kitu ambacho kinasaidia sana kuhamasisha kufanya biashara kwa maslahi ya jamii nzima.
Ukuaji wa bank za kiIslam duniani wenye muelekeo wa kukataa riba ulioanza kujitokeza ktk kipindi takriban cha miaka thalathini iliyopita, umetokana na muelekeo wa kimataifa wa kuzikumbatia banki zinazokubali riba. Kwa mfano sifa kubwa ya mfumo wa uchumi wa banki za kiMagharibi ulitegemea riba kwa kiasi kikubwa sana ambapo ilifikia kiwango hata cha kupuuza dini zao. Kitendo hicho kilizidi kukua kwa kiasi ambacho riba ilikua kama uti wa mgongo ktk uchumi wa Magharibi, kwa upande mwingine uIslam uliendelea kung’ang’ania kwamba riba sio sahihi.
Inatosha kua (Judaism, Christianity, Hinduism na Islam), zenye wafuasi zaidi ya theluthi mbili za watu duniani zimeharamisha Riba. (For the Judaic and Christian views on interest see Johns, et. al., and Noonan (1957) and for the Hindu view, see Bokare (1993), p. 168). Uislamu umeharamisha riba (2:278-279) Pia angalia Biblia, Deuteronomy 23: 19; Leviticus 25:36; Exodus 22:25; Ezekiel 18:5-9. Luke 2:34-35.
Inadaiwa kwamba presha iliyotokana na mfumo wa bank za kiMagharibi na ombwe lililokuwepo ktk uchumi wa kiIslam, viliwahamasisha wasomi wa kiIslam kujaribu kuulezea uchumi wa kiislam ktk njia za kitaalam zaidi. Wasomi wa kiislam ktk masuala ya kiuchumi waliamua kufuata misingi ambayo ilikubalika ktk dini yao kama vile (Mudarabah), (Muraabaha) ambazo zina maana ya kushirikiana, (Leasing) ambayo ina maana ya kukodisha na aina nyingine nyingi za kiuchumi ambazo zinakubalika kiIslam.
Kwa maelezo zaidi: soma www.ijuebankyakiislam. blogspot.com
Hio ni juhudi muhim sana na tungependa kuona hizo bank za Kiislam zinatatua haya mattzo yetu.
ReplyDeleteTabia ya kutukopesha pesa kwa kuweka riba sio nzur, yaani badala ya kumsaidia mtu lile ttzo lake ndio kwanza unataka kumuongezea mariba tu. Huu sio mfumo mzur. Uislam uje utukomboe na huu ustaarabu wa dhulma wa magharib.
Mungu utupe nguvu.
Ni kitu kizuri kwani ni kweli kwamba bank hizo zinaenea kwa kasi sio tu hapa nchini bali duniani kwa ujumla lakin maelezo zaidi bado yanatakiwa kuhusu nature ya bank hizo
ReplyDeleteJazzakAllah Khairan!Aloweka mpango huwo!Kweli Waislam wa TZ tumekuwa tunakula Moto(Riba) kwa miaka mingi sana,Sasa Allah Kareem Katuonyesha njia.Hapa UK ni nchi ya Kikristo lakini wameanzisha A/C za Kiislam katika baadhi ya mabank miaka mingi sana,na wakristo wanaoitambua Riba kuwa ni haramu wamefungua A/C hizo,,,,
ReplyDeleteAhlam,,,London
Ni kheri manake naona nchini kwetu muda si mrefu madhara kama yaliyotokea marekani yatatokea.Mfano nyumba za shirika la nyumba la taifa wanashirikiana na mabenki,ukikopa toka benki unaweza kurudisha mara mbili ya ile uliyokopa.Kama ukifa inawezekana mtu mafao yake yote yakachukuliwa na mabenki kufidia hela zilizokopwa,na wajane na watoto wanaweza kubakiwa na hakuna cha kurithi.Kwa hiyo watu wawe makini katika kukopa.
ReplyDeletetunashukuru kwa taarifa hii njema, tunawaunga mkono,...
ReplyDeleteMdau, hongera sana kwa blog yako yenye mlengo chanya kabisa katika kuleta mapinduzi ya kibenki, hasa hasa Afrika na Tanzania. Ningependa sana ugusie maendeleo ya ukuawaji wa benki za kiislam Afrika ya Mashariki kwani kuna maendeleo makubwa,na benki nyingi tu zimeanzishwa, na ingekuwa vizuri kama ungezitaja katika blog yako, lakini naona mdau bado upo kinadharia sana pia umejikita sana Ulaya! Lakini hongera sana kwa hatua hii muhimu! Mdau Tanzania.
ReplyDeleteMimi ni mkristo na hakuna sehemu yoyote kwenye biblia ambayo imekazata kutoa au kupokea riba. marejeo ambayo umetoa hapo juu hayana uhusiano wowote na kukatazwa riba. Luka 2:34-35 inasema hivi:
ReplyDeleteLuke 2:34-35
34 Then Simeon blessed them and said to Mary, his mother: “This child is destined to cause the falling and rising of many in Israel, and to be a sign that will be spoken against, 35 so that the thoughts of many hearts will be revealed. And a sword will pierce your own soul too.”
kwahiyo huu ni upotoshaji wa makusudi!badala yake bwana YESU ilitoa mfano kwamba unapopewa Talanta (fedha) lazima uizalishe! Mathayo 25: 15-29:
15 To one he gave five talents of money, to another two talents, and to another one talent, each according to his ability. Then he went on his journey. 16 The man who had received the five talents went at once and put his money to work and gained five more. 17 So also, the one with the two talents gained two more. 18 But the man who had received the one talent went off, dug a hole in the ground and hid his master's money. 19 "After a long time the master of those servants returned and settled accounts with them. 20 The man who had received the five talents brought the other five. 'Master,' he said, 'you entrusted me with five talents. See, I have gained five more.' 21 "His master replied, 'Well done, good and faithful servant! You have been faithful with a few things; I will put you in charge of many things. Come and share your master's happiness!' 22 "The man with the two talents also came. 'Master,' he said, 'you entrusted me with two talents; see, I have gained two more.' 23 "His master replied, 'Well done, good and faithful servant! You have been faithful with a few things; I will put you in charge of many things. Come and share your master's happiness!' 24 "Then the man who had received the one talent came. 'Master,' he said, 'I knew that you are a hard man, harvesting where you have not sown and gathering where you have not scattered seed. 25 So I was afraid and went out and hid your talent in the ground. See, here is what belongs to you.' 26 "His master replied, 'You wicked, lazy servant! So you knew that I harvest where I have not sown and gather where I have not scattered seed? 27 Well then, you should have put my money on deposit with the bankers, so that when I returned I would have received it back with interest. 28 " 'Take the talent from him and give it to the one who has the ten talents. 29 For everyone who has will be given more, and he will have an abundance. Whoever does not have, even what he has will be taken from him.
Ukweli siku zote utawaweka huru! Tatizo la ndugu zetu hamataki kuujua ukweli aidha kwa kwenda shule au kujisomea.
Niwahimize tu kwamba bado hajachelewa KUMKUBALI NA KUMPOKEA YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YENU......
Tatizo tunajaribu kuwasiliana na hiyo benki huko TZ ili tuhamishie pesa zetu kutoka kwenye mabenki yenye riba lakini hawajibu email, sasa tufanyeje?
ReplyDeleteMimi ni mkristo tena wa maombi na ninaunga mkono benki hizi za kiisalam zipo kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu na sio kumkomoa kama ilivyo kwa mabenki hapa duniani.
ReplyDeleteBwana mwandishi wewe uelezee umma nini maana ya ISLAMIC BANKING sasa unaanza kunukuu IMANI za watu wengine uki quote huku na kule ina HUUUU?
ReplyDeletekama zitawasaidia wananchi ni vizuri ila isijekuwa wanataka kuleta terrorism kwenye nchi yetu ya amani afadhali tubaki maskini na amani yetu
ReplyDeleteni maneno tu riba na faida ni yaleyale tu, kama wanatoa neno riba wanaweka faida tofauti iko wapi? biashara ni biashara tu.. ingekuwa kunatofauti ukikopeshwa kitu cha milioni moja kwanini usirudishe hiyo hiyo amount unarudisha zaidi ya hy millioni moja?
ReplyDeleteTunapenda watu wanaosaidia wengine, lakini pia ni muhimu kwa bank hizi kuwa na transparency system ili ziangaliwe kama kuna mambo mengine yanayoendelea. Mara nyingi bank kama hz hependelea nchi ambazo sheria za bank zimelala, ili kuweza kufanya mambo ya kisiri siri. tafadhali angalia bank iliyoitwa Bank fo credit and commerce international ilivyokuwa-kwani nayo ilikuwa islamic bank, hii bank ilitaka kuchukua dunia na mpaka mataifa kama UK na US yalidanganyika, lakini mwishowe ndo ukawa huo, tafadhali angalieni hiyo bank kwa kifupi ilikuwa inaitwa inaitwa BCCI.
ReplyDeleteMi si mtaalamu wa benki ila napenda kutoa tofauti ya riba na faida. Riba hutozwa mtu anapouza pesa yaani kwa mfano ukichukua SHILINGI MIA, UNARUDISHA MIA NA ISHIRINI, haijalishi ulifaidika na hiyo mia au la, benki lazima uirudishie mia NA ishirini ya riba yao.
ReplyDeleteFaida ni pale unapoingia ubia na benki katika mradi wowote na kufanya biashara, ile faida (au hasara) mnagawana. Mwisho wa siku nyote mnafaidika. Ni hayo tu
Kuna nduu yetu mkristo ambae alijaribu kukanusha kwamba riba haikukatazwa kwenye bible na akataja kwamba bwana YESU amesema kwamba unapopewa talanta (fedha lazima uzizalishe Mathatyo 25: 15-29. Baadae akasema kwamba tatizo la wengi ni kukataa kujua ukweli au kutokwenda shule.
ReplyDeleteAmejibiwa kama ifuatavyo: Ni kweli kwamba riba imekataza zaidi ya aya moja ktk Bible na kama labda aya zilzotajwa hazikuwa wazi basi rudia aya hizi.
Prohibition in the Bible
“Do not charge your brother interest, whether on money or food or anything else that may earn interest.” (Deuteronomy 23:19)
“Do not take interest of any kind from him, but fear your God, so that your countryman may continue to live among you.” (Leviticus 25:36)
“If you lend money to one of my people among you who is needy, do not be like a moneylender; charge him no interest” (Exodus 22:25)
Righteous servant of God doesn’t take interest
5 "Suppose there is a righteous man who does what is just and right.
6 He does not eat at the mountain shrines or look to the idols of the house of Israel. He does not defile his neighbor's wife or lie with a woman during her period.
7 He does not oppress anyone, but returns what he took in pledge for a loan. He does not commit robbery but gives his food to the hungry and provides clothing for the naked.
8 He does not lend at usury or take excessive interest. He withholds his hand from doing wrong and judges fairly between man and man.
9 He follows my decrees and faithfully keeps my laws. That man is righteous; he will surely live, declares the Sovereign LORD. (Ezekiel 18:5-9
Inadahaniwa labda ndugu hakumuelewa pale bwana YESU aliposema kwamba ukipewa pesa ni lazima uizalishe. Kwa hakika alikusudia biashara na sio riba kama muandishi alivyo jaribu kudhania. Kwa maelezo zaidi rudia ktk blog iliyotajwa kuna sehemu ya maswali na majibu. Unashukuriwa kwa mchango wako huo.
Kuna ndugu mwengine nae alidai kuani maneno tu riba na faida ni yaleyale tu, kama wanatoa neno riba wanaweka faida tofauti iko wapi? biashara ni biashara tu.. ingekuwa kunatofauti ukikopeshwa kitu cha milioni moja kwanini usirudishe hiyo hiyo amount unarudisha zaidi ya hy millioni moja?
ReplyDeleteAmejibiwa kama ifuatavyo Kuna tofauti kubwa kati ya riba ba faida. Faida inatokana na biashara na kama biashara isipofanikiwa basi walioshirikiana wanagawana hasara na hivyo hakuna aneumia ktk jamii na kuna faida nyingi. Riba ni kutaka ziada ambayo haina sababu wala haijulikani ziada hiyo itatoka wapi. Madhara yake ni mengi ikiwemo haya yanayo onekana ktk matatizo ya kiuchumi. Kuna maelezo ya kina zaidi kwenye blog iliyotajwa na kuna sehemu ya maswali na majibu unaweza kufahamishwa zaidi. shukran kwa mchango wako.
MUHIMILI MKUU WA TOFAUTI KATI YA ISLAMIC BANKING(Zero interest banking) AND NON-ISLAMIC BANKING(interest based banking):
ReplyDeleteNI: KATIKA BEI YA MTAJI AU MSINGI:
INTEREST BANKING/NON-ISLAMIC BANKING:
''The Price of Capital rate of interest with given prion of 't' time ''
SASA WATOA MAKALA WATUPE KWA NJIA YA 'ISLAMIC BANKING' AU NON-INTEREST BANKING MSINGI AU MTAJI UNAAINISHWA VIPI?
Anonymous said..
ReplyDelete.
Mimi ni mkristo na hakuna sehemu yoyote kwenye biblia ambayo imekazata kutoa au kupokea riba. marejeo ambayo umetoa hapo juu hayana uhusiano wowote na kukatazwa riba. Luka 2:34-35 inasema hivi:
Ukweli siku zote utawaweka huru! Tatizo la ndugu zetu hamataki kuujua ukweli aidha kwa kwenda shule au kujisomea.
Niwahimize tu kwamba bado hajachelewa KUMKUBALI NA KUMPOKEA YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YENU......
Swali la juu limejibiwa kama ifuatavyo: kuna ushahidi mwingi tu ktk Bible wa kukatazwa riba na aya zinazokuja chini zinafafanua zaidi.
Prohibition in the Bible
“Do not charge your brother interest, whether on money or food or anything else that may earn interest.” (Deuteronomy 23:19)
Maana ya maneno haya ni ‘usimtoze ndugu yako riba ikiwa ni pesa au chakula au kitu chochote ambacho kitaingiza riba’.
“Do not take interest of any kind from him, but fear your God, so that your countryman may continue to live among you.” (Leviticus 25:36). Maana ya maneno hayo ni usichukue riba ya aina yoyote kutoka kwake ispokua muogope Mungu ili watu wa miji yenu waendelee kuishi nanyi.
“If you lend money to one of my people among you who is needy, do not be like a moneylender; charge him no interest” (Exodus 22:25). Kama ukimuazima yoyote ktk watu wangu ambae ana shida usiwe kama wale wanaoazima pesa usimtoze riba. Na nyingine nnyingi.
Righteous servant of God doesn’t take interest
5 "Suppose there is a righteous man who does what is just and right.
6 He does not eat at the mountain shrines or look to the idols of the house of Israel. He does not defile his neighbor's wife or lie with a woman during her period.
7 He does not oppress anyone, but returns what he took in pledge for a loan. He does not commit robbery but gives his food to the hungry and provides clothing for the naked.
8 He does not lend at usury or take excessive interest. He withholds his hand from doing wrong and judges fairly between man and man.
9 He follows my decrees and faithfully keeps my laws. That man is righteous; he will surely live, declares the Sovereign LORD. (Ezekiel 18:5-9
NGURUWE HARAMU ILA POMBE NAKUNYWA.....FAIDA NA RIBA NIKAMA SOKSI NA KIATU
ReplyDeleteWAKRISTO RIBA HAISTAHILI MSILAZIMESHE MNAIKUBALI KWA TAMAA NA MAZOEA TU.
ReplyDeleteBIBLIA INAWAKATAZA LAKINI MNAKUWA WABISHI,,,MPO KAMA MARASTA JUU YA SUALA LA KULALALISHA 'BANGI' NA NINYI MNATAKA KUHALALISA 'RIBA'...!
Unajua hili ni somo adimu, ambalo huwezi kulipata shuleni. Hapa uingereza kuna wataalamu wa Islamic Banking ambao ni wakristo na wanalifurahiya sana. Elimu haina mwisho, na ndio maana unaona waislamu watoa quotes kutoka biblia kwa sababu katika vitabu vya mwenye enzi Mungu Biblia kwa waislam lina heshima yake. Wenzetu someni Quran muielewe, haina ubaya, elimu haina mwisho. Wenzenu Vatican kuna Islamic and Quran Studies
ReplyDelete