Wajumbe wa Bodi Mpya ya Utalii wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mhe. Waziri , Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Bibi Nuru Millao mara baada ya bodi yao kuzinduliwa rasmi jijini Dar es salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ezekiel Maige akizungumza wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini TTB alioufanya Aprili 04,2012 jini Dar es Salaam katika jengo la Mpingo makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii. kulia kwako ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Balozi Charles Sanga na anayefuatia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Dkt Alloyce Nziku ambaye ni Katibu wa bodi hiyo na Mhe. Abdulkarim Shah Mbunge wa Mafia ambaye pia ni mjumbe wa bodi hiyo.
Balozi Charles Sanga akitoa shukurani kwa Waziri Maige mara baada ya kuizindua rasmi bodi yao .
Balozi Charles Sanga akisikilizwa na Waziri Maige na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarishi.
Wanaoonekana pichani ni wajumbe wa bodi hiyo wakichukua maagizo ya Mhe Ezekiel Maige Waziri wa Maliasili na Utalii wakati akiizindua bodi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...