Na Moahammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Zanzibar 


Jeshsi la Polisi Zanzibar limewataka wananchi kutovunjika moyo na kuacha kushirikiana na Jeshi hilo katika kukomesha vitendo vya kihalifu kwa kuwaona watuhumiwa waliokamatwa wakiwa nje kwa dhamana.


Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Kamishna Msaidizi Aziz Juma Mohammed, wakati akitoa elimu juu ya utii wa sheria bila shuruti na Ulinzi Shirikishi.

Kamanda Aziz amesema kuwa idadi kubwa ya washukiwa wa wanaokamatwa hutuhumiwa kwa makosa yanayotoa uhuru wa dhamana kisheria kwa mtuhumiwa.

Amesema mtuhumiwa anaweza kukamatwa na kupewa dhamana akiwa katika kituo cha Polisi ama Mahakamani kwani hiyo nayo ni haki ya mtuhumiwa

Hata hivyo Kamanda Aziz amesema kuwa kila mwananchi hasa waliotendewa matukio ya kihalifu wanayofursa ya kwenda kituo cha Polisi ama mahakamani kuulizia maendeleo ya kesi inayomhusu.

Lakini amesema watuhumiwa wengi wanapopewa dhamana ya Polisi ama ya mahakama wamekuwa wakitamba mitaani kuwa wametoa hongo jambo ambalo amesema limekuwa likiongeza idadi ya tuhuma za rushwa katika taasisi za Polisi na Mahakama.

Amewahimiza wale wote wanaoshuhudia matukio ya kihalifu kuwa tayari kwenda Polisi kutoa maelezo yao na baadaye kwenda Mahakamani kutoa ushahidi wa yale aliyoyashuhudia ili kuiwezesha Mahakama kutoa uwamuzi wa haki kwa pande zote mbili.

Kamanda Aziz amesema hakuna mtuhumiwa atakayepatikana na hatia mahakamani pasipokuwepo kwa ushahidi wa kutosha kuwezesha mahakama kuthibitisha kosa.

“Ukitoa maelezo yako Kituo cha Polisi na ukaacha kwenda kuielezea mahakama juu ya kile ulichokishuhudia haitoshi na hivyo mtuhumiwa anaweza kufutiwa shitaka lake”. Alisema Kamanda Aziz.

Hivi sasa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar kupitia kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa wakiongozwa na Kamishna wa Polisi Visiwani humo CP. Mussa Ali Mussa, linaendelea na mkakati wake wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya utii wa sheria bila shuruti pamoja na haki za watuhumiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ni ukweli kabisa hongo ipo mbele kwa sababu kwanza ukichukulia mfano mtu kutoka bara akipatwa na matatizo mfano. kuibiwa na mtu mwenyewe unamjua ukienda kushaki hawafuatilii kesi inapuuziwa kwa nn wasituchukulie kama watanzania. Wabara tuliopo Zanzibar hata tukitendewa vitendo vya uhalifu tunashindwa hata namna ya kwenda kwenye vyombo vya sheria maana utaambiwa huyu ni mjomba, mtoto wangu unadhani hapo sheria inatendeka na kwanini ss wazanzibar waliopo bara hatuwa nyanyasi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...