Habari Ankal  pole na kazi , naomba unisaidie kunitangazia gari langu hilo nahitaji kubadilishana na mwenye gari aina ya toyota yoyote ile iwe GAIA AU NOAH kwa sababu gari yangu hii haina tatizo lolote isipokuwa kwangu imekuwa hainitoshi mimi na FAMILIA yangu , nahitaji gari kubwa kidogo, nitashukuru sana kama utanisaidia , natanguliza shukurani zangu za dhati ,AHSANTE

kwa anayetaka kuiona gari ipo dsm kariakoo ,Gerezani
na kwa mwenye gari ambayo anaona itanifaa naomba anitumie picha kwenye email nayoweka chini hapa asanteni





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. bei ya gari yako lazima itakuwa chini ya unayoyataka. upo tayari kulipa pesa kufikia unayoyataka?

    Pia kwanini usiende kwa wauzaji ufanye hii kama trade-in na ulipigie tofauti ya thamani ya gari yako na utakayochagua? (kama ili linafanyika TZ hapa)

    ReplyDelete
  2. Kingine kwanini unaficha namba za Gari as if ni la wizi wakati umesema ni gari lako?

    ReplyDelete
  3. Family planning!Duh inabidi tuwe tunaplan hadi aina za magari kulingana na ukubwa wa familia zetu jamani isijekukuta yaliyomkuta mwenzetu.

    ReplyDelete
  4. Ahsante sana michuzi kwa kuweka post yangu na mungu akuzidishie kila la kheri..

    kuhusu gari yangu najua kama thamani yake iko chini kuliko gari ninazozitaka na niko teari kuongeza pesa ili mradi bei iwe fair kote kote.

    ReplyDelete
  5. Mimi ninayo Noah lakini itabidi unipe Tsh 9M na hiyo gari yako. zenj.biz.uk@gmail.com kwa mazungumzo zaidi.

    ReplyDelete
  6. wasiwasi wangu uko kwenye hizo namba,mbona kazificha? ziweke wazi au unaona aibu watu wakikujua!!! hii ni biashara bana na kila mtu anahiari ya kufanya au kutofanya,usiifiche maana kwa kufanya hivyo unazidisha maswari,kitu kingine toa taarifa kamili za gari yako,cc,mwaka,bima,kibari cha barabarani,kilomita ilizotembea,na kila taarifa mteja atakayoitaka.

    ReplyDelete
  7. mimi nakushauri uza hiyo gari halafu nunua unayotaka, najua ujaongeza hela kidogo, lakini kwa kubadilisha sijui kama itawezekana.

    ReplyDelete
  8. Kuna mtu kakupa ushauri mzuri hapo juu...Uza hilo gari,ongeza pesa kidogo vuta gari nyingine kubwa ya hiyo..Preferably NOAH family Size ambazo zinagonga Mil 11-15 TZS kuiweka barabarani,kubadilisha itakuwa ngumu sana..lakini endelea kujaribu mkuu usikate tamaa..

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...