Na Ripota wetu Marekani
Kwa watanzania waishio marekani jina DJ KAYCEE (pichani) sio geni kwao hasa wale wanaotokea jimbo la TEXAS, na majimbo ya karibu na hapo!! Hivi karibuni nilitembelea moja ya Show za Dj huyu ambae ni moja wa ma Dj wa Tanzania ambao wanafanya vizuri sana kwenye anga za kimataifa nchini Marekani kwa sasa, nimekuwa nikilisikia jina lake siku nyingi na pia nimepata sifa zake nyingi kwa uwezo wake wa ku-control aina mbali ya majumuiko iwe clubs au events tofauti tofauti za nje na ndani. Nilipogongana nae na kupata nafasi ya kuteta nae mawili matatu DJ KAYCEE alikuwa na haya ya Kusema.
Kwa watanzania waishio marekani jina DJ KAYCEE (pichani) sio geni kwao hasa wale wanaotokea jimbo la TEXAS, na majimbo ya karibu na hapo!! Hivi karibuni nilitembelea moja ya Show za Dj huyu ambae ni moja wa ma Dj wa Tanzania ambao wanafanya vizuri sana kwenye anga za kimataifa nchini Marekani kwa sasa, nimekuwa nikilisikia jina lake siku nyingi na pia nimepata sifa zake nyingi kwa uwezo wake wa ku-control aina mbali ya majumuiko iwe clubs au events tofauti tofauti za nje na ndani. Nilipogongana nae na kupata nafasi ya kuteta nae mawili matatu DJ KAYCEE alikuwa na haya ya Kusema.
MIMI: Kaycee, nimefurahi kukutana na wewe Leo
KAYCEE: Mimi pia mkuu
MIMI: Embu tupe historia yako kwa ufupi Mr Dj
KAYCEE: Nimezaliwa Tanzania mkoa wa Iringa wilaya ya Ludewa mwaka 1981, nilikulia iringa mjini na kuhamia Dodoma na wazazi wangu, nilisoma elimu ya msingi na O'level Dodoma na nilimaliza elimu ya Secondari Mkoani Iringa shule ya Mkwawa mwaka 2003, Nilihamia Dar na Kuja Marekani mwaka 2006.
MIMI: Ulianzaje u-DJ na ni lini?


MIMI: Ni Club zipi unakumbuka uliwahi kupiga ukiwa nyumbani Tanzania?
KAYCEE: Nilishawahi kupiga RUAHA DISCO Iringa, IMASCO Dar, NK DISCO Dodoma, Don Bosco na pia sherehe mbalimbali
MIMI: Ni DJ yupi nyumbani ambaye alikuvutia wewe kuwa Dj?
KAYCEE: Kusema ukweli wapo wengi ila wa kwanza ni DJ JD wakati huo akiwa Redio one na East africa Redio, huyu ndio haswa muhusika wa mimi nilivyo hivi sasa.
MIMI: Ulipofika hapa marekani ulikuwa introduced vipi mpaka kuwa international dj na kupiga kumbi maarufu na kubwa mbalimbali Hivi sasa.
KAYCEE: Kwanza kabisa ni msaada wa Mungu. Pili ni jitihada zangu binafsi, Nilisota sana kabla ya Jamii ya Kimarekani kunikubali hususani wakifahamu nimetoka Afrika, Ila kilichonisaidia ni kutumia kila Sec na dakika nilioipata kwenye mashine iwe ni Guest dj au ninaposhikia dj mwingine akienda Restroom (Uani) kujisaidia. Ilikuwa ni vigumu sana mwanzo, na trust me nime dj kwa free mara kibao Just kujenga jina na kuonyesha kipaji. Sikujua watu walikuwa wakiangalia mpaka nilipopata breakthrough, siku moja nilipokea simu kutoka Redio kubwa hapa Houston wakiniomba kushiriki kwenye Djs competition walioandaa, nilikubali na kushiriki na nilimaliza roundi ya kwanza nikiwa namba 1 na round ya pili nikiwa namba 2. Hapo ndipo Houston ilipotambua jina DJ KAYCEE
MIMI: Je unashughulika na Crowd au Clubs za aina gani?
KAYCEE: Nimepata bahati ya ku deal mostly na International Clubs where u find all kinds of races and people, Nasema ni bahati kwa kuwa sio ma dj wengi has a weusi na wa kutoka nje ya Marekani wanapata bahati hii. Pia ninafanya kazi na Clubs na Makusanyiko ya Kiafrika hasa watanzania wenzangu kwa Mialiko maalumu.
MIMI: Unaweza kututajia ni Club zipi unafanyi kazi kwa sasa au umewahi kufanyia kazi hapa marekani?
KAYCEE: Moja ya clubs kubwa ambazo nimeshafanya kazi nazo ni Bikini beach, Brixx, Metro, Jeffs, La Cave, 249 Grill, A.M Lounge, Drillers, Claytons na nyingine nyingi ambazo sizikumbuki (kicheko)
MIMI: Je kwa sasa mtu anaependa kazi zako akupate wapi hapa Houston?
KAYCEE: Kwa sasa napatika JEFF'S LOUNGE kila J4 na Jumamosi, Fast Eddies Billards kila Ijumaa, Na pia ninapatikana kwenye moja ya club kubwa za after hours in Houston inayoitwa La Cave Kila J3, J4, Alhamisi na Ijumaa Kuanzia saa 2am-6am ( saa nane usiku mpaka kumi na mbili asubuhi). Ni club ambayo inachukua watu zaidi ya 500.
MIMI: Mbali na ku dj ni kazi gani nyingine unajishughulisha nayo hapa Marekani?
KAYCEE: Hii ndio kazi pekee ninayoifanya hapa marekani zaidi ya hapo nalala sana, (kicheko) na pia Ninasoma shule na nina major in Management na Video Production.
MIMI: Kwa wadau wengine ambao wanependa kukutumia kwa shughuli zao zingine mabalimbali wanaweza kukupataje?
KAYCEE: Napatika kwa email ya kayceemoreflavor@yahoo.com, www.facebook.com/deejay kaycee, na pia napatikana kwa namba ya simu ya mkononi 281-236-5204 begin_of_the_skype_highlighting 281-236-5204 end_of_the_skype_highlighting na pia waweza kunisikiliza kupitia Bongo Redio kila Ijumaa saa 8pm mpaka 4pm through www.bongoradio.com
MIMI: Mwisho kabisa kuna lolote ambalo ungependa kusema kwa kumalizia Mr Dj?
KAYCEE: Napenda kuwashukuru wote ambao wanapenda kazi zangu kwa support na kwa kunitia moyo. Mungu azidi kuwabariki na pia atubariki sote!
MIMI: Asante Kaycee
KAYCEE: Asante sana mkuu
safi kaycee,keep up,we are with u all the way to 40/40 club
ReplyDeleteNamkubali huyu dogo tangu bongo....yeye alikuwa mkwawa na mimi nilikuwa Tosa, tulikuwa tunatoroka shule kwa ajili ya kwenda kucheza Disco lake pale Ruaha Disco. Na ni kweli ametoka mbali sana!! endeleza libeneke kaka!!
ReplyDeleteSafi sana Mi niko hapa Texas na shuguli ya huyu dogo naifahamu.....akishika mashine hukai mpaka club inafungwa!! Ni bora uende club umeshalewa maana hata mda wa kunywa utakuwa huna tena....Big up kaycee!!
ReplyDeleteSafi sana mpiganaji.
ReplyDeleteWell done u make us proud. nikitembelea america lazima nipite huston ni exprience vibes zako. proud 2 b tanzanian
ReplyDeleteKila jambo likifanywa kwa dhati linazaa matunda.Binafsi nilikuwa naona jamaa anapoteza muda kwa kazi hiyo wakati tunasoma pale Mkwawa toka Mwaka 2001 hadi 2003,labda ni kwa uelewa mdogo wa nini alikuwa anafanya na alikuwa analenga nini.He has now proven me wrong.Kwa hatua aliyofikia,nampa hongera zake na namtakia kila la kheyr hkatika kazi zake za kila siku
ReplyDelete